Anne Makinda: Hoja binafsi marufuku kuanzia sasa!

itisheni maandamano wabunge tudai haki zetu za msingi! Upuuzi mtupu huu ccm wanadhani uwingi wa wabunge bungeni ndo kila kitu wanasahau nguvu ya umma ni zaidi yao! Ipo siku tutawachapa bakora wajue tuna uchungu na nchi yetu
 
Kamati ya Uongozi na Maadili ya Bunge imesitisha utoaji wa hoja binafsi indefinitely.

Kwa sababu, baadhi ya wabunge wamekosa nidhamu.

Mbunge gani, kwa kusoma nidhamu gani, katika hoja gani, no details.

Source: TBC
----------------------

Legislators should riot in protest!

baada ya wabunge wa ccm kuwasilisha hoja zao then za wapinzani ni takataka......makinda and the like time will tell
 
Yani CCM wameamua kutumia nguvu kuzuia hoja za wapinzani ili watanzania wazidi kutaabika na mfumo mbovu wa utendaji.
CCM ni wauwaji.
 
Kuna vituko kweli Tanzania! Hivi kweli CCM hamuoni kuwa mnajiaibisha mbele ya Watanzania? Ni kanuni ipi ya bunge spika anatumia kufuta kabisa hoja binafsi? Hata kama ni kubaka demokrasia si kwa jinsi hii. Inasikitisha kuona mtu mzima hakubali kukosolewa na hakubali kuelimisha akijua fika kuwa anayoyafanya yote yako nje ya mstari miaka zaidi ya 50! Tukubali kujibu hoja kwa hoja na kukosolewa, solution siyo kukimbilia kufuta hoja binafsi na kutunga sheria nyingine kandamizi, huu si wakati wake mmechelewa mno.
 
Hatukubali hatukubali bora watu waingie barabarani kupinga huo utaratibu wa wabunge kufungwa midomo. No way watanzania kataeni kwa hali na mali. Tuna haki ya kuwakilishwa bungeni hatuwezi kunyang'anywa hiyo haki na mtu yeyote yule. hii ni uvunjifu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania. tusikubali.

katika kazi yoyote ile nidhamu ni jambo muhimu. hatuwezi kuwa na bunge lilojaa majununi watupu. bunge haliwezi kuwa kama sokoni kkoo. kiti lazima kiheshimiwe.

hongera spika!
 
Watakuwa wanajadili nini sasa?
Wanataka Bunge liwe rubber stamp ya kupitisha miswada ya seikali peke yake, ambayo mingi yake, haina maslahi na watanzania,bali iliyo mingi ni ya kifisadi na ni ya maslahi ya vigogo wa CCM na serikali yao, ikiwa ndiyo mkakati wao mkuu pekee uliobaki wenye lengo la kuhakikisha wanatutawala hadi mwisho wa Dunia!!!!
 
Yani CCM wameamua kutumia nguvu kuzuia hoja za wapinzani ili watanzania wazidi kutaabika na mfumo mbovu wa utendaji.
CCM ni wauwaji.

tumia akili. tatizo na sababu kubwa ni kukosekana kwa nidhamu. bunge limekua kama sokoni. hoja binafsi zisitishwe kwa muda. nawasilisha
 
itisheni maandamano wabunge tudai haki zetu za msingi! Upuuzi mtupu huu ccm wanadhani uwingi wa wabunge bungeni ndo kila kitu wanasahau nguvu ya umma ni zaidi yao! Ipo siku tutawachapa bakora wajue tuna uchungu na nchi yetu
\

toa pumba zako hapa. kawachape wadogo zako kwanza. rais alisema juzi kigoma kuwa anaetaka kumwaga damu akachukue kiwembe na ajikate mwenyewe kwanza ili damu yake imwagike
 
Shame on madame speaker anne, shame on pm pinda, shame on the whole ccm representertives, shame on jk and his party.
 
Kama hii habari ni ya kweli itakuwa aibu kweli kweli kwa Spika! Anavunja taratibu za bunge kwa sababu uwezo wake ni mdogo? Na kwa CCM wataweza kuhimili mapigo kama hoja binafsi zitaletwa mitaani? Mimi naona kama Spika anawaandaliwa CCM bomu!

usiwe unajidanganya dogo. mitaani kwa nani? kawa unataka kumwaga damu kachukue kiwembe ujikate kate itamwagika. kama watoa hoja hawana nidhamu spika afanyeje?

akiwaambia kaa chini wanakaidi. hata ungekua ww spika ungevumilia dharau kama hii! acha ujuha
 
Jamani 2015 tusifanye makosa na matani kama hela zao we kula ila kura peleka CDM haiwezekani mtu miaka 50 mifumo ya kielimu,afya,barabara,kodi,maji ni ovyo halafu analeta ubabe kwa watu wanaotaka kutusaidia........
Ukifanya kosa hakika amini Tanzania itakuwa chini zaidi ya hapa
 
usiwe unajidanganya dogo. mitaani kwa nani? kawa unataka kumwaga damu kachukue kiwembe ujikate kate itamwagika. kama watoa hoja hawana nidhamu spika afanyeje?

akiwaambia kaa chini wanakaidi. hata ungekua ww spika ungevumilia dharau kama hii! acha ujuha

dogo, nani?

Kama spika mwenyewe hafuati kanuni anategemea nani azifuate? anatakuwa aongeze kwa mfano, na kama amevuruga kanuni sasa avune alichopanda. Hoja binafsi or not, CCM wakae mkao wa kuogeshwa maji baridi 2015.
 
tumia akili. tatizo na sababu kubwa ni kukosekana kwa nidhamu. bunge limekua kama sokoni. hoja binafsi zisitishwe kwa muda. nawasilisha

utovu wa nidhamu unashuhulikiwa na kanuni za bunge.
kwa mujibu wa kanuni ya 58 ya bunge aneyeweza kuondoa hoja bungeni ni mtoa hoja pekee na sio makinda wala uongozi wabunge, sasa kwa nini spika anavunja kanuni kwa kutupilia mbali hoja za wabunge wapinzani kinyume na kanuni??
Kilichotokea bungeni kimeonekana na watanzania wameshuhudia jinsi serikali ya CCM inavyowaadhibu wapiga kura kwa kupinga hoja zinazosimamia maslahi ya watanzania.
CCM ni adui namba moja wa mtanzania.
 
itisheni maandamano wabunge tudai haki zetu za msingi! Upuuzi mtupu huu ccm wanadhani uwingi wa wabunge bungeni ndo kila kitu wanasahau nguvu ya umma ni zaidi yao! Ipo siku tutawachapa bakora wajue tuna uchungu na nchi yetu
wananchi wenzangu hivi kuna haja ya kuwa na bunge kwa sasa?
 
Wabunge wa upinzani leteni mashitaka kwa wananchi wataamua
Hoja ya elimu yetu kukosa mitaala tangu nchi kupata uhuru spika anasema isijadiliwe
Mfumo mbovu kabisa wa jiji la Dar es Salaam kuelea kwenye vinyesi na kukosa maji safi na salama spika na CCM yake wanataka hoja isijadiliwe
Hoja ya baraza la mitihani na kushusha viwango vya ufaulu pindi waziri wa elimu na serikali ya CCM inapojisikia na itakapo lifanyia swala hilo kisiasa spika anasema isijadiliwe
Hoja ya asilimia 42 wa tembo kuuliwa kila mwaka spika anasema isijadiliwe
Hoja ya gesi ya Mtwara na mikataba feki spika anasema isijadiliwe
Hoja ya maisha magumu na ukosefu wa kazi kwa vijana na kuundwa kwa baraza la vijana isijadiliwe kwa vile imeletwa na wapinzani njooni mutuambie sisi ndio tutaamua yaani wametufunga wanancchi kupitia wawakilishi wetu yaani inamaana tunakosa uwakilishi kabisa spika anataka tusikilize mawaziri wake tuu hiyo ya hoja kuzifuta ametoa kwenye kanuni zipi anadhani atabaki salama na CCM wanadhani wako salama na serikali wanadhani wametukomoa mawazo yao wananchi sisi ni wakuburuzwa duh kweli tuna spika

Thanks Mkuu.

Makinda anaona wa-Tanzania wote ni wajinga. Wameshiba kodi zetu na bado hawawezi kutuheshimu! Sisi tunawheshimu and they must respect us as well. Nani hatusemee bungeni kama wabunge wetu wamefungwa midomo. Huyu mama amekuwa kibaraka mkubwa wa haki zetu. Nimefuatilia sana nyendo zake bungeni na hazileti matumaini ya mwendelezo wa amani yetu.
 
kweli wameishiwa busara, hekima, na uvumilivu,wanaona bora watibue tu, sasa tutaishije bila maji, tutaishije bila elimu? wao wanaona hizo hoja za hamis na mwigulu ndo za maana? wakati utapataje mikopo bila kupitia shule za msingi na secondar? utaishije bila maji, hayo ni maamuzi ya hasira, na kiongozi yoyote atakiwi kuwa na hacra, busara ndo itumike, angalieni mmekosea wapi, mjiulize kwa nini bunge hili la kutetea chama limekuwa hivi, mbona bunge la spika 6 haikuwa fujo, tuliona mivutano ya hoja?
 
dogo, nani?

Kama spika mwenyewe hafuati kanuni anategemea nani azifuate? anatakuwa aongeze kwa mfano, na kama amevuruga kanuni sasa avune alichopanda. Hoja binafsi or not, CCM wakae mkao wa kuogeshwa maji baridi 2015.

kutokana na maoni yako lazima utakua dogo kwangu. nimekuzidi umri. mimi sizungumzii ccm au chdm. nazungumzia nidhamu pale bungeni. dharau imezidi. dogo jifunze kuwa nidhamu ni silaha ya mafanikio.
 
Back
Top Bottom