BekaNurdin
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 2,267
- 2,041
Wee mama wewe! Heri maneno ya kinywa chako yangekuwa machache.View attachment 865905
Mbunge wa Kuteuliwa, Anne Kilango Malecela, akina kwenye mkutano wa kampeni Kata ya Machame Uroki, Wilaya ni Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, amesema CHADEMA hakitakaa kishike Dola katika Nchi hii kutokana na mfumo wake wa utawala kuwa mbovu.
Alisema anashangazwa na Mkoa huo (Kilimanjaro) kuwa ndiyo Pemba ya Tanzania Bara, akisema umekuwa Mkoa wa Upinzani na kuuliza wanapata faida gani?
View attachment 865904
Mama kumbuka:
Danieli 4:32; .............. Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, awaye yote!
Kama una muda mama, soma sura yote ya 4 ya kitabu hicho cha Danieli.
Tena kitabu cha 1Samweli 2:3 kinasema;
Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo;Majivuno yasitoke vinywani mwenu;Kwa kuwa BWANA ni Mungu wa maarifa,Na matendo hupimwa na yeye kwa mizani.
Kama haitoshi vile, 1Samweli 2:6 inasema;
BWANA ndiye huinua juu na pia kushusha chini.
Yatafakari haya.
Naomba unisamehe kama nimekukwaza!