Anne Kilango Malecela ashangazwa na Mkoa wa Kilimanjaro kuwa Pemba ya Tanzania Bara. Adai CHADEMA haitakaa ishike Dola Nchi hii

Daimler

JF-Expert Member
Sep 11, 2018
556
973
IMG_8283.JPG

Mbunge wa Kuteuliwa, Anne Kilango Malecela, akina kwenye mkutano wa kampeni Kata ya Machame Uroki, Wilaya ni Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, amesema CHADEMA hakitakaa kishike Dola katika Nchi hii kutokana na mfumo wake wa utawala kuwa mbovu.
Alisema anashangazwa na Mkoa huo (Kilimanjaro) kuwa ndiyo Pemba ya Tanzania Bara, akisema umekuwa Mkoa wa Upinzani na kuuliza wanapata faida gani?

IMG_8282.JPG
 
Kwakweli huwa napata shida sanaa kwa PHDs holders kuwa sehemu ya kutotaka kufahamu ukweli ambao darasa la saba wanauona ndani ya CHADEMA kuwa si chama cha siasa bali ni chama cha Mbowe na familia yake. Sasa sijui tunawasaidiaje hawa akina Prof Baregu na Abdallah Safari? Watu kama Sumaye sina mashaka kwani hata uelewa wao na elimu zao ni za mashaka mashaka sana sihitaji hata kuwazungumzia hapa. Lowasa anafahamika ni mpiga dili ndo maana yuko CHADEMA huyu naye sihitaji kutafakari chochote juu yake.
 
Kuna haja serikali kiroho safi kuainisha kwa wananchi majukumu ya viongozi wote wa kuchaguliwa kuanzia Mwenyekiti wa Kitongoji, Kijiji, Mtaa, Diwani, Mbunge n.k maana kiukweli hizi fikra za mbunge ama diwani atakuletea maendeleo zife maana ni shughuli za serikali hizo...viongozi hao wa kuchaguliwa wao wanabaki kufanya kazi ya kuwakilisha wananchi kwenye kuhakikisha serikali inatekeleza mipango yake kikamilifu na kushirikiana na wananchi kuibua vipaumbele vya miradi ya maendeleo ili kiongozi wa kuchaguliwa aweze kuhakikisha mipango inapitishwa na serikali inatekeleza mipango hiyo. Hizi ngonjera za sijui Mbowe hawezi ama ataleta maendeleo hazina tija. (Natamani wanaokuja kwa kujinadi kwa nitajenga shule ama barabara wapigwe chini awe mpinzani asiwe mpinzania)
 
Kwakweli huwa napata shida sanaa kwa PHDs holders kuwa sehemu ya kutotaka kufahamu ukweli ambao darasa la saba wanauona ndani ya CHADEMA kuwa si chama cha siasa bali ni chama cha Mbowe na familia yake. Sasa sijui tunawasaidiaje hawa akina Prof Baregu na Abdallah Safari? Watu kama Sumaye sina mashaka kwani hata uelewa wao na elimu zao ni za mashaka mashaka sana sihitaji hata kuwazungumzia hapa. Lowasa anafahamika ni mpiga dili ndo maana yuko CHADEMA huyu naye sihitaji kutafakari chochote juu yake.
Wataka waje kuwa kama akina Mwakyembe, Kabundi na sasa Basiru, ambao Sasa wanafikiri kutumia tumbo?
 
Back
Top Bottom