Acha kupotosha watu. Unatakiawa kuelewa historia ya shule vizuri. Soma mkakati wa shule na kuuelewa. Acha wivu. Fanya kazi upate mapato yako halali. Shule ya Barbro ilianza kwa kusajili watoto yatima tu, ambao hawakuwa wakilipa karo.
Baadaye, shule ya Barbro iliongeza kundi jingine; watoto kutoka familia zenye uwezo kidogo lakini wenye uwezo kitaaluma (bright) kwa wazazi husika kulipa robo ya karo, robo tatu ikilipwa kwa ruzuku ya ufadhili wa shule kutoka Uswidi.
Shule ilipoendelea kukua, hususan kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya kidato cha 4 na 6,shauku ya wazazi, tena wenye uwezo kiuchumi kupepeleka watoto wao kusoma shule ya Barbro, ili-inform sera ya shule ya Barbro kuwahudumia watoto wanaotoka katika familia zenye backgrounds tofauti, hivyo kulipa karo katika viwango tofauti. Kuna watoto wanaotoka familia maskini wanaendelea kusoma bure, kunawatoto wanaolipa robo ya karo wakipewa ruzuku robo tatu, kuna wanaolipa nusu ya karo na kufadhiliwa ruzuku nusu, kuna wanaolipa robo tatu ya karo na kupewa ruzuku robo, na kuna kundi kubwa la watoto wanaotoka katika familia zenye uwezo wanaolipa yoteya Tzs. 4.5m/-.
Lakini ingefaa kujua kuwa karo imepanda mwaka huu (2014) kutoka TZs.3m/-, baada ya Waswidi waliokuwa wakifadhili shule hii kumaliza muda wao wa ufadhili ili shule iweze kujitegemea hivyo kujiendesha yenyewe (self-sustaining entity).
Aidha ni muhimu kufahamu kuwa kiasi cha karo, kwa wazaziwanaolipa Tzs. 4.5m/- inachangia watoto wanaotoka katika familia zisizojiwezawaliosajiliwa shuleni Barbro kutokana na uwezo wao kitaaluma/kumudu masomo.
Huo ndio ukweli. Watanzania tuache uswahili au kuchanganya our political vendetta-motivated politics dhidi ya jitihada binafsi za baadhi ya viongozi wa kisiasa kusaidia harakati za maendeleo.
Professa Tibaijuka amekuwa aki-fundraise kwa ajili ya kupta pesa za kuendesha shule za Barbro Johanssen Trust.
Ukitathmini ubora na thamani ya sasa ya shule za Barbro (DSalaam) na Alexander Kajumulo (Bukoba) utakubaliana na ukweli kuwa Tzs. 1.6b/- ni peanut. Huo ndio ukweli.
Anayetaka kufanya siasa za upinzani awe genuine, siyo kuletavendetta.