Mzee wa Gumzo
Senior Member
- Apr 21, 2008
- 197
- 6
Jana wabunge waliendelea na mjadala kuhusu mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2008/09 na aliposimama mbunge wa Same Mashariki Anna Kilango Malecela nilijua litaibuka jambo.
Tulichokuwa tunataka kujua wengi wetu ni msimamo wa CCM kuhusu fedha zilizoporwa EPA nA KWINGINEKO.Hivi karibuni wabunge wa CCM walikuwa na kikao cha dharura na mwenyekiti wao JK na mada kuu ilikuwa kutengeneza msimamo wa kichama kuhusu fedha za EPA na wale wote waliohusika ama kuhusishwa na uporaji wa 'vijisenti' vyetu.Kilikuwa kikao cha siri kwelikweli na mengi yalijadiliwa lakini vyanzo makini vilitujuza kuwa wale vidomodomo ndani ya chama waliokuwa wanataka fedha zirejeshwe na wahusika wafunguliwe mashtaka 'walitulizwa' kwa mkwara mzito.
Nilijua hata hivyo siyo wote watakaofumba midomo wasiseme ndani ya bunge kile kilichokuwa kimejadiliwa kwenye kikao kile cha siri.Ndiyo maana nasema Mh.Anna Kilango Malecela amemtumia salamu JK kuwa wananchi wake waliompeleka bungeni wana umuhimu mkubwa hata zaidi ya chama chake achilia mbali hao wanaokingiwa kifua.
Kwa mchango wa Mh.Kilango jana tumepata kujua kikiao kile cha wabunge na mwenyekiti wao kilimalizika kwa kuweka msimamo gani.Mh.Kilango ametoa onyo kwa wabunge kuwa 'hapatatosha' pale endapo wabunge hasa wa CCM watakubali kufumba midomo kama chama kinavyotaka.
Hizi ni salamu tosha kwa JK na CCM kuwa busati wanalojitahidi kulivuta kufutika madudu ya EPA,Richmond na kadhalika haliwezi kuzuia harufu mbaya ya uvundo inayotoka na jamii imeshtuka.
Ni ALUTAAAA CONTINUAAA!.HAPATATOSHA HAKI YA NANI!