Anna Kilango katuma salamu kwa JK,CCM

Mzee wa Gumzo

Senior Member
Apr 21, 2008
197
5
Jana wabunge waliendelea na mjadala kuhusu mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2008/09 na aliposimama mbunge wa Same Mashariki Anna Kilango Malecela nilijua litaibuka jambo.

Tulichokuwa tunataka kujua wengi wetu ni msimamo wa CCM kuhusu fedha zilizoporwa EPA nA KWINGINEKO.Hivi karibuni wabunge wa CCM walikuwa na kikao cha dharura na mwenyekiti wao JK na mada kuu ilikuwa kutengeneza msimamo wa kichama kuhusu fedha za EPA na wale wote waliohusika ama kuhusishwa na uporaji wa 'vijisenti' vyetu.Kilikuwa kikao cha siri kwelikweli na mengi yalijadiliwa lakini vyanzo makini vilitujuza kuwa wale vidomodomo ndani ya chama waliokuwa wanataka fedha zirejeshwe na wahusika wafunguliwe mashtaka 'walitulizwa' kwa mkwara mzito.

Nilijua hata hivyo siyo wote watakaofumba midomo wasiseme ndani ya bunge kile kilichokuwa kimejadiliwa kwenye kikao kile cha siri.Ndiyo maana nasema Mh.Anna Kilango Malecela amemtumia salamu JK kuwa wananchi wake waliompeleka bungeni wana umuhimu mkubwa hata zaidi ya chama chake achilia mbali hao wanaokingiwa kifua.

Kwa mchango wa Mh.Kilango jana tumepata kujua kikiao kile cha wabunge na mwenyekiti wao kilimalizika kwa kuweka msimamo gani.Mh.Kilango ametoa onyo kwa wabunge kuwa 'hapatatosha' pale endapo wabunge hasa wa CCM watakubali kufumba midomo kama chama kinavyotaka.

Hizi ni salamu tosha kwa JK na CCM kuwa busati wanalojitahidi kulivuta kufutika madudu ya EPA,Richmond na kadhalika haliwezi kuzuia harufu mbaya ya uvundo inayotoka na jamii imeshtuka.

Ni ALUTAAAA CONTINUAAA!.HAPATATOSHA HAKI YA NANI!
 
huyu mama inabidi tumtupie macho kwa sana huenda akawa msaada mkubwa kwa sisi walala hoi tunaokatwa kodi kubwaaaaaaaa na kufanya hawa mafisadi kujilimbikizia malundo ya shilingi bila kujali MTZ wa hali chini atapatawapi matibabu, barabara mbolea kwa wakulima nk.
 
Yaani huyu mama Anahitaji dua zetu wote ili aendelee kuwa na afya njema kwa ajili ya kumalizia kazi aliyo ianza. Nimeguswa sana na nime mpenda ghafla!

Na wasii wote waendao kanisani, misikitini, milimani na hata chini ya miti, kila mtu kwa lugha yake amlilie Muumba ili hata hao wabunge wengine wanao kubali kuburuzwa wafungue macho yao na kutimiza wajibu wao.

Ewe Jk angalia hilo kuti ulilo kalia.. watumikie wananchi wako walo kuweka madarakani, acha kuwa kibaraka wa mafisadi 'be your self! watose kaka.


Mungu akulinde mama Ane.
 
nilishasema kuwa huyu JK ni mnafki tuu, anaharibu nchihata kama si yeye aliye weka mkwala mzito kwa nini me ruhusu watu kipigwa mikwala??
 
Hi wajumbe!

Mie nimeguswa sana na huyu mama, anatakiwa kulindwa na kila jicho na sala zote za watanzania wote, huyu mama atatutoa kimasomaso Watanzania walalahoi, tumekosa sauit kwa kipindi sasa na Keki inaliwa na wachache na kujisifu mbele ya watu na kudharau juu.
Mungu mlinde mama Anna dhidi ya maadui wabaya na aendeleze mapambano kwa nguvu zote maana sauti yake ni ya ukombozi dhidi ya utawala mabavu na ya anasa. Pamoja nae namuunganisha Dk Slaa/ Zitto/ Hamad/ Mama Komu/ Manyanya/Sendeka kwa uchache.
 
Nafikiri kwa sasa wanaweza wakawa wanajuta ni kwanini walichukua zile millioni 200 zake,ila huyu mama amekuwa mwiba kwa serikali..

Go mama,GO anne,GO and tell them we need our Money that we are working harder to earn them..

Invisible,kama ikiwezekana mtumie mama huyu E-mail ili awe member wa JF
 
mama ana kilango waambie na hawo mafisadi kuwa siyo tu bungeni hakutatosha, bali hata nchi nzima hii itakuwa haitatosha hadi kieleweke, mweleze huyo mnafiki serukamba wa kighoma mjini kuwa , unafiki hakuna mahali popote ulikofanyikiwa
 
mama ana kilango waambie na hawo mafisadi kuwa siyo tu bungeni hakutatosha, bali hata nchi nzima hii itakuwa haitatosha hadi kieleweke, mweleze huyo mnafiki serukamba wa kighoma mjini kuwa , unafiki hakuna mahali popote ulikofanyikiwa

Siyo Serukamba tu huko, kuna mwingine kipofu anaitwa Msambya. Huyu ni kipofu mwingine anayetamani kuwameza wanajimbo wake.

Bajeti ya leo ni ya kumkamua mtanzania na kumuinua fisadi na wafanyabiashara wakubwa.
Sina uhakika kama kampuni kubwa zinalipa kodi. Kwa mfano nimejifunza kuwa wale wenye tin wanamtindo wa kulipa kodi ambapo inatazamwa balance yake iko vipi. mfano ni kwamba Mimi kama mwenye kampuni inayoitwa ngona Interprises ltd ninawachaji kodi wateja kutokana na huduma ama bidhaa zangu, hiyo natakiwa kuwapelekea TRA. Na mimi pia ninaponunua vitu kutoka kampuni nyingine nalipa kodi ili yule mwenzangu aipeleke kunakohusika. Sasa mahesabu yanavyofanyika ni kwamba ngona ikishalipa kodi huko kwenye kampuni nyingine inakuja kupiga mahesabu kwa kutoa ile iliyowachaji wateja wake na balance ndo inayopelekwa TRA. Kwa hiyo si kodi yote inayokusanywa huwa inapelekwa TRA isipokuwa ya mtumiaji wa mwisho. ni kwa nini na mimi kama mlipa kodi nisitazamwe kwa mtazamo huo huo ili ninapokwenda kupata huduma za mahitaji ya kila siku nisilipe kodi tena kwa kuwa nimeshakatwa kutoka kwenye mshara wangu?

Why??? Kwa nini??? Kuna ukandamizaji kwa mtu wa chini?

Makampuni hayalipi kodi isipokuwa ni wanatumiaji (waliowengi walala-taabani) ndo walipaji wa hiyo kodi na waendeshaji wa shughuli za serikali. Na ndo hao hao wanaokandamizwa na kubezwa na serikali yao kwa kukumbatia ufisadi.

Tunazitaka hela za EPA na waliochukua warudishe na majina yao yajulikane.

Hongera mama Anne Kilango malecela, hutapigana peke yako na sisi tuko nyuma yako.
 
tusubiri tuone maendeleo......manake inaweza mkwala ule wa kikao cha siri haukumtosha. akashushiwa mwengine wa size yake na yeye akageuka bubu.
time will tell
 
mm.jpg


ANNA KILANGO ASANTE MAMA
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom