Anna Abdallah: ‘Msaidieni mtoto asipate ujauzito akiwa shule’

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
‘Msaidieni mtoto asipate ujauzito akiwa shule’

Mama Salma Kikwete anakumbukwa kwa kutoa kauli ya kutaka wanaopata mimba wasiendelee na masomo, kauli iliyopingwa na wanasiasa lakini Rais John Magufuli amekuwa akiunga mkono kauli hiyo.



Mwanasiasa mkongwe Anna Abdallah amesema badala ya kuendelea kuishambulia Serikali, jamii inatakiwa imsaidie mtoto wa kike asipate ujauzito wakati wa masomo yake.

Mwanasiasa huyo ameitoa kauli hiyo leo wakati mbunge wa kuteuli Salma Kikwete, akikabidhi kijiti cha nafasi ya Mlezi wa Chama cha Maskauti Wasichana Tanzania (TGGA) kwa mlezi mpya, Samia Suluhu ambaye ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Chama hicho kilianzishwa mwaka 1928 hapa nchini na shughuli zake zikiwa ni kutoa elimu ya ujana na kujikinga na ugonjwa wa Ukimwi, matumizi ya dawa za kulevya na pombe, kuzuia mimba za utotoni na afya bora, elimu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii na kujiamini.

Anna Abdalah alitoa kauli hiyo wakati akimpongeza Mama Salma kwa kuongoza vyema chama hicho kwa miaka 12 huku akieleza mchango wake katika kutekeleza majukumu ya TGGA katika kusaidia maendeleo ya msichana hapa nchini."Nakumbuka baada ya kutoa msimamo wako (Salma Kikwete), watu walishangaa lakini nikupongeze, TGGA inaungana na tamko hilo na Rais John Magufuli ametoa tamko hilo wakati muafaka ili kuongeza uelimishaji zaidi, tusipige kelele tu,"alisema Anna ambaye ni mwenyekiti wa bodi ya udhamini wa TGGA.

Kwa mujibu wa TGGA, idadi ya wanachama wake imeendelea kuongezeka kutoka 97,143(2015) hadi kufikia 100,080 kwa mwaka huu huku wapya 300 wakitarajia kuapishwa.

Asilimia 95 ya wanachama wake ni wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kote nchini.


Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom