Anguko sasa ni dhahiri

Anguko sasa ni dhahiri

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,396
Reaction score
829,698
Ngoma ikivuma sana hupasuka na mwenye kiburi akishupaza sana shingo huvunjika mara.

Tuwe na tuo tuwe na tafakuri kwenye maneno yetu...mtu anayejisifia rohombaya wazi wazi sio kwamba hana tu hekima lakini pia hana saburi na hatafakari matokeo ya kauli zake, huyu ni mwovu.

Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri, bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu, huchochea ghadhabu huchochea visasi chuki na ubabe.Dhima ya kiongozi ni kuleta umoja na maridhiano sio kuchochea chuki na visasi
Kiongozi mwenye hekima kamwe hawezi kuongea karaha.Karaha huleta simanzi na majonzi, mtu wa karaha hana ogofyo lolote, ni kiburi na kiburi chake ni anguko.

Nuru ya mtu mbaya huzimika ghafla bila tahadhari bila taarifa. Mtu wa hekima hutengeneza patano kwa njia ya mashauriano.

Je, tunatengeneza ama tunabomoa?
Je, tunahubiri amani ama visasi?
Je, tunaeneza ustawi au anguko?
Je, Tunafundisha hekima au upuuzi?

- Hakuna kitu kibaya kama kuruka mkojo na kukanyaga kinyesi
 
Anguko la Chama Dola? Hahahahah hahahaha hajahah hahahahhh
1472965606393.jpg
 
Yaan nimeshutuka sn.Nikafikiri kuna anguko la chama au anguko la kiongozi,kumbe ni fikira zako na ndoto ndo unaleta hapa.Pole sn ndoto si mahala pake hapa.
1472965671343.jpg

Umefikiri hivyo kwakuwa tayari kichwani mwako una hizo fikra na yale mambo maovu mnayopanga kizani ulidhani tayari yameshafanya kazi...God forbid hilo halitatokea
 
Hata South Africa baada ya uhuru walitengeneza Tume ya usuluhishi na upatanishi lengo ikiwa ni kufuta uhasama na kuleta umoja……hapa kwetu baada ya uchaguzi……???
Tunatonesha vidonda kwa kuvitia chumvi na ndimu..tunahubiri chuki na visasi
 
Ngoma ikivuma sana hupasuka na mwenye kiburi akishupaza sana shingo huvunjika mara
Tuwe na tuo tuwe na tafakuri kwenye maneno yetu...mtu anayejisifia rohombaya wazi wazi sio kwamba hana tu hekima lakini pia hana saburi na hatafakari matokeo ya kauli zake..huyu ni mwovu
Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri, bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu, huchochea ghadhabu huchochea visasi chuki na ubabe....dhima ya kiongozi ni kuleta umoja na maridhiano sio kuchochea chuki na visasi
Kiongozi mwenye hekima kamwe hawezi kuongea karaha..karaha huleta simanzi na majonzi, mtu wa karaha hana ogofyo lolote, ni kiburi na kiburi chake ni anguko
Nuru ya mtu mbaya huzimika ghafla bila tahadhari bila taarifa...mtu wa hekima hutengeneza patano kwa njia ya mashauriano
Je tunatengeneza ama tunabomoa?
Je tunahubiri amani ama visasi?
Je tunaeneza ustawi au anguko?
Je Tunafundisha hekima au upuuzi?
-hakuna kitu kibaya kama kuruka mkojo na kukanyaga kinyesi
Leo Ni siku rasmi ya ibada, umekumbuka kumuombea Bob lakini!?.
 
!
!
nikienda mbali na hapa nadhani nitapata label ya uchochezi. Niache tu
 
Back
Top Bottom