Anguko la taifa laja

Wakati haujafika, hivyo tusipoteze muda kujadili mambo ya Lowassa, japo ushabiki wa kisiasa bungeni umeshtua wengi maana hata Sitta ameonekana akipiga meza kumshangilia Lowassa! Hali hii inaweza kuwa ni kejeli dhidi ya Lowassa! Maovu yake yanafahamika kwa kila Mtanzania, endapo CCM wataamua kumweka agombee Watanzania watamhukumu kwa uhuru wao wa kupiga kura.
 
Lowassa hafai hata kidogo kuwa Rais wa nchi hii.

Kwa sababu ana kashifa nyingi sana za Ufisadi ukianzia na EPA, Richmond. Dowans n.k.

Nadhani mnakumbuka huyu ****** alipoingia ikulu mwaka 2005 kwa kishindo watu wakadhani ataleta maendeleo kumbe hakuna kitu. Mimi sikumbuki kama alishawahi kufanya maamuzi yoyote mazuri kwa taifa hili akayasimamia.

Ili Tanzania tuendelee tunahitaji Rais wa kutoka Chama Mbadala ambacho ni CDM kinachopigania maslahi ya wananchi wote na huyu si mwingine bali ni Mpambanaji Dr. Slaa.

Alipoanzisha hoja ya EPA Bungeni wabunge karibia wote walimzomea; lakini leo EPA inakila kwao.
Na aliwataja hadharani MAFISADI wa nchi hii kwa mara ya kwanza pale Mwembeyanga na jinsi walivyofanya ufisadi wao akiwemo na ******.
 
Mimi naamini Lowassa alikuwa anakaribia kuwa tisìo kwa urais wa JK ndo akampangia zwenge,sina sababu yeyote ya kutoamini hvyo kwani siasa za bongo ni za fitina...Na wewe mleta hoja wewe una mrengo gani? We unadhani nani anafaa kuwa rais after JK? ama na wewe una agenda yako?
 
huo ni mtazamo wako wewe humtaki wengne tunamhitaji sasa usilazime kile unachokiamini wewe ndo kionekane sahihi
Hee siamini hili hivi kunawatu wanamtaka Lowasa au ni sababu ya MALIPO MNAYOPEWA ( NATAMANI CCM IFE HATA SASA)
 
Mimi naamini Lowassa alikuwa anakaribia kuwa tisìo kwa urais wa JK ndo akampangia zwenge,sina sababu yeyote ya kutoamini hvyo kwani siasa za bongo ni za fitina...Na wewe mleta hoja wewe una mrengo gani? We unadhani nani anafaa kuwa rais after JK? ama na wewe una agenda yako?

nitaweka msimamo wangu juu ya nani awe RAIS wa taifa hili na atakuwa pindi nitakapo jiridhisha na taratibu mbalimbali ninazo zifanya. nitamleta mgombea huyo humu humu JF ninapaamini sana na watu wataendelea kuchangia nilichokipendekeza kuwa ni sahihi au nimekurupuka
 
mi naomba kila siku el awe mgombea wa magamba 2015 kwani ndo utakuwa mwisho wa chama hicho katika ramani ya siasa za tz. Wataungana na dovutwa kuunda kambi isiyo rasmi ya upinzani bungeni.
hahahha umemtaja mwenyekiti wangu devota!
 
Ukiona uchaguzi umepita watu wamebaki moto kana kwamba uchaguzi mwingine utakuwa kesho kutwa, ujue uchaguzi uliopita haukuwaridhisha wapiga kura wengi. Hii inajionesha na jinsi watu walivo na hamu ya kupiga kura tena. Loh, hakika tumepitiliza!! Kampeni zaendelea....
 
Mkuu never Lowassa ni muhimu kwa masilahi ya CDM wewe huwajui CDM wanamtaka Lowassa then waje wamalize kazi.
CDM are very strategic.
 
Ed Lowasa alifanywa mbuzi wa kafara tu na JK !na mi naamini ipo siku kila kitu kitajulikana! TUSUBIRI.

Kama alikuwa mbuzi wa kafara kwa nini asiseme?kitendo cha kukaa kimya ndicho kinachofanya akose credibility ya kuwa kiongozi wa tz,atakuwa na kura zake kwa watu kama wewe lakini hakuna mweledi wa kufikiri anayaweza kumwamini EL
 
Mimi kura yangu nitampa dr Wilbroad Peter Slaa. Katibu mkuu cdm basi. Kwa heshima na taadhima,nahaidi mbele ya umma kuwa endapo dr slaa hatopitishwa cdm sitapinga kwa kuwa ndo demokrasia. Lakini akipewa bendera,tangu leo na kuendelea mpaka mwaka 2,020 kila kifika kwenye chumba cha kura, ntakuwa namchagua dr slaa hata kama jina halipo. Ni msimamo wangu tu.
 
Hivi watu huwa hamuunganishi the dots.
Mbona huyu jamaa alishamalizwa na mwalimu.

Piga ua galagaza, kama mwalimu alikwambia hufai hutakaa utufae !

Lowasa aliambiwa na mwalimu kuwa yeye ni kijana mdogo utajiri alionao kaupata wapi ? Alishindwa kujibu na mwalimuu akammaliza hapohapo!

Mwalimu alisema kama mnampenda nendeni mkanywe naye chai lakini hafai kuwa kiongozi wa nchi hii.

Kwa kuwa ccm ya leo si ile ya mwalimu, hata lowasa anaweza kuwa mgombea hainashida. Lakini alishalaaniwa na mchonga hataweza!

Mwenzake pia aliambiwa akae pembeni maana anaonekana bado hajakua haya yako wapi mpaka leo mambo yake yaleyale mpaka nchi imememshinda.

Kwa kifupi ni kwamba Jk na EL walishalaaniwa na mchonga they will never be any good!
 
Ndugu zangu wanawaJF na wasiyo kuwa wanawaJF ambao huwa wanapita humu kwakuperuziiii na kudadisi ASALAAM ALYKHUMUU.

Nimeamua kutoa mtazamo wangu juu ya anguko la TAIFA hili kwa kile ninachokiona kinavyoendelea kwasasa. nimesikitishwa sana na kauli zinazoendelea huku mitaani na maofisini juu ya nani awekiongozi wataifa hili na watu wengi *wa maofisi wamipongeza forum hii kuwa inauwezo wa kumpanga Rais wataifa hili kuliko taasisi yeyote ile ukilinganisha na wnzetu waliyoendelea huwa na taasisi maalum ya kumchagua Rais hata kama wananchi hamumtaki mtamchagua tu kwambinu wanazozitumia kwa ushawishi mkubwa wa hali ya juu.

Hapa kwetu Tanzania hamna mpango huwo ndiyo maana unasikia kila siku tunatengeneza kizazi cha kifisadi, kizazi cha kulipana kisasi na kizazi cha majigambo hili nianguko la taifa kwasasa. ila niendembali zaidi nipale ninapoendelea kusikia watu makini au forum makini kama hii pamoja na uhuru wa maoni au mawazo watu wanao takiwa kutoa eti na kufikiri kwetu kote TUNAWAZISHWA HUMU LOWASSA aje atawale taifa hili, kiukweli tunaanza kumjengea LOWASSA njia ya URAIS bila sisi kujijua kuwa ni watu muhimu sana katika kupanga na kupangua viongozi bora na wasiyo bora.

Naamini kauli hii wengi watanipinga na wengi wataniunga mkono: turudi nyuma uchaguzi uliyopita JF ilichangia kwakiasi kikubwa mno kumpata mgombea URAIS wa CDM na tuliona tulivyochangia kumpata mgombea makini mwenye uwezo mkubwa kuliko aliyeshinda sasa na hata huku AFRICA KUSINI tulipo forum hii inasifika sana kwa hilo. sasa iweje leo hii tuanze kupoteza malengo yetu kwakutaka kuwarudishia madaraka wezi wakuu wataifa hili? kama sikutaka kuliangamiza taifa kwa ushabiki usiyo na tija yeyote ile kwa mwananchi wa kijijini asiyejua kinachoendelea kwasasa ?

Hofu *hii nimeipata leo kupitia humu humu JF nasikia LOWASSA leo alikuwa anachangia hutuba ya waziri mkuu wengi mmemsifu badala ya kuendelea kumkataa kwa maovu yake aliyoyafanyia taifa mmeanza kusahau na wengine kumuonea hata na huruma. hili niaanguko la taifa na JF mtahusika na hukumu hii pamoja na mimi kwa kuwa ni member humu.

HITIMISHO
Tuanndaeni viongozi makini kwa faida ya dada zetu mama zetu watoto wetu waliyopo vijijini ambao nawao siku moja wanatamani kuliongoza taifa hili na anaweza kuwa viongozi bora kuliko kizazi chtu cha sasa. haya ni maoni yangu na wewe unaweza fikri zaidi yangu kwa kulisaidia taifa. MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI JF......

Mkuu hapa hoja yako imeegemea sana upande mmoja.Ni kweli LOWASA amelitendea kosa taifa letu na wananchi pia kwa ujumla.Mimi nakubaliana na wewe uko sawa kutokumsamehe kwa alicholifanyia taifa kwa kuwa huo ni utashi wako wewe.

Hapa ninachopingana na wewe ni kuwa,huyu LOWASA ni mwanadamu kama sisi tulivyo.Hivyo basi kuna wakati kama mwanadamu unakosea na jamii inakuchukia lakini ukijirekebisha jamii inakukubali tena.

Mimi nafikiri tusiwakataze watu kumpa sifa kama amefanya kitu cha maana na pia tumuhukumu kwa mabaya anayofanya pia.

Ni huo tu mchango wangu wapendwa wana JF.
 
Edward Richmond lowassa akiwa rais ,ongeza wafuatao:

Andrew Vijisenti chenge ....................waziri mkuu
Rostam Dowans aziz........................waziri wa fedha.
hao ndio watakaomrithi jakaya mbayuwayu kikwete........................
 
Watanzania tuwe wazarendo na nchi yetu,CCM hi iliyotufikisha hapa kwenye shida na njaa leo hii viongozi walewale wanataka kuwa marais wa tanzania wakati maskini ni wengi na taifa limepoteza dira ya maisha,mafisadi kama kina LOWASSA leo wanautaka urais kwa nguvu yote hili Taifa tunalipeleka wapi?wazazi wetu,watoto wetu,dada zetu,wadogo zetu,leo watumwa kwenye nchi yao,uhuru wa kweli tunaoupigania kweli tutaupata?nation cake ni kweli tutaipata?ndugu zangu mapinduzi ya kweli yanahitajika ni lazima CCM itoke madarakani ili nchi ipate uhuru wa kweli na watanzania waenjoy utajiri wa malaasili zao,tukiendelea na ushabiki huu wa CCM watoto wa MASAKI wataendelea kuishi maisha mazuri kwa kutumia kodi za watanzania,wataendelea kuajiriwa maofisini bila kuwa na sifa na kuacha watoto wa peasant wenye sifa na uwezo wa kichwani mana hawa watoto wa wakubwa wazazi wao wameshika ofisi kubwa kazi zinzpotolewa 200 memo huwa 188 za watoto wao,huku watoto wa peasant wakiachwa mana hakuna anayewajua,TUICHUKIE CCM,TUIOGOPE CCM Kama kweli tuna nia ya watoto wetu waje wale NATON CAKE.
 
Ndugu zangu wanawaJF na wasiyo kuwa wanawaJF ambao huwa wanapita humu kwakuperuziiii na kudadisi ASALAAM ALYKHUMUU.

Nimeamua kutoa mtazamo wangu juu ya anguko la TAIFA hili kwa kile ninachokiona kinavyoendelea kwasasa. nimesikitishwa sana na kauli zinazoendelea huku mitaani na maofisini juu ya nani awekiongozi wataifa hili na watu wengi *wa maofisi wamipongeza forum hii kuwa inauwezo wa kumpanga Rais wataifa hili kuliko taasisi yeyote ile ukilinganisha na wnzetu waliyoendelea huwa na taasisi maalum ya kumchagua Rais hata kama wananchi hamumtaki mtamchagua tu kwambinu wanazozitumia kwa ushawishi mkubwa wa hali ya juu.

Hapa kwetu Tanzania hamna mpango huwo ndiyo maana unasikia kila siku tunatengeneza kizazi cha kifisadi, kizazi cha kulipana kisasi na kizazi cha majigambo hili nianguko la taifa kwasasa. ila niendembali zaidi nipale ninapoendelea kusikia watu makini au forum makini kama hii pamoja na uhuru wa maoni au mawazo watu wanao takiwa kutoa eti na kufikiri kwetu kote TUNAWAZISHWA HUMU LOWASSA aje atawale taifa hili, kiukweli tunaanza kumjengea LOWASSA njia ya URAIS bila sisi kujijua kuwa ni watu muhimu sana katika kupanga na kupangua viongozi bora na wasiyo bora.

Naamini kauli hii wengi watanipinga na wengi wataniunga mkono: turudi nyuma uchaguzi uliyopita JF ilichangia kwakiasi kikubwa mno kumpata mgombea URAIS wa CDM na tuliona tulivyochangia kumpata mgombea makini mwenye uwezo mkubwa kuliko aliyeshinda sasa na hata huku AFRICA KUSINI tulipo forum hii inasifika sana kwa hilo. sasa iweje leo hii tuanze kupoteza malengo yetu kwakutaka kuwarudishia madaraka wezi wakuu wataifa hili? kama sikutaka kuliangamiza taifa kwa ushabiki usiyo na tija yeyote ile kwa mwananchi wa kijijini asiyejua kinachoendelea kwasasa ?

Hofu *hii nimeipata leo kupitia humu humu JF nasikia LOWASSA leo alikuwa anachangia hutuba ya waziri mkuu wengi mmemsifu badala ya kuendelea kumkataa kwa maovu yake aliyoyafanyia taifa mmeanza kusahau na wengine kumuonea hata na huruma. hili niaanguko la taifa na JF mtahusika na hukumu hii pamoja na mimi kwa kuwa ni member humu.

HITIMISHO
Tuanndaeni viongozi makini kwa faida ya dada zetu mama zetu watoto wetu waliyopo vijijini ambao nawao siku moja wanatamani kuliongoza taifa hili na anaweza kuwa viongozi bora kuliko kizazi chtu cha sasa. haya ni maoni yangu na wewe unaweza fikri zaidi yangu kwa kulisaidia taifa. MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI JF......
depending on how you look at it, taifa halianguki ni watu wake ndio wanaanguka
 
Lowasa ni mwizi, tanzania inajua, afrika inajua na dunia inajua.
Lowasa ni fisadi, tanzania inajua, afrika inajua na dunia inajua.
Lowasa na wenzake walituletea rich mond, tanzania inajua, afrika inajua na dunia inajua.
Lowasa hafai kuwa hata mwenyekiti wa kitongoji, tanzania inajua, afrika inajua na dunia inajua.
Ccm haiwezi tena kutoa kiongozi bora na asiye mwizi, tanzania inajua, afrika inajua na dunia inajua.
Chadema ndio tumaini na chama mbadala cha watanzania, tanzania inajua, afrika inajua na dunia inajua.
2015 chadema ndio chama tawala, watanzania wanajua na dunia inajua.
 
Kama hii nchi mlimpa JK ambaye ameivuruga kabis akuna ubaya gani EDWARD LOWASSA AKIPEWA?? kwanza yeye ni mtendaji shupavu na mahiri zaidi ya JK mara mia! Muacheni na usisadi wake lakini kama uwezo anao kwa nini asipewe?? Ngoja nikupe kwa muhtasari nani anaweza kuichukua nchii hiii 2015:
  1. Dr Hussein Mwinyi - Huyu anapigiwa debe kimya kimya na waislamu Tanzania. JK naye anashinikizwa kumuandaa, anaonekana kuwa ni suluhisho la muungano lakini tatizo kubwa kwake ni uwezo wake katika anga za kimataif ana uwezo wa kudhibiti k=bguvu za waislamu! Wachunguzi wa siasa wanamuona kuwa ni mdini na ataleta macahfukao ya kidini!
  2. Edward Lowassa - Ni charismatic leader na mchapa kazi sana! CCM wanamkataa kwa kuwa anahusishwa na ufisadi na kuwa ni miongoni mwa wanachama wanaoijali umaarufu wao kuliko Chama. Hadi leo hakuna aliyeweza kuthibitisha kashfa dhidi yake. Kuna kundi la wana CCM wanamuunga mkono, viongozi wa CCM hawamtaki kwa kuwa wanaogopa atalipiza kisasi! Pamoja na kashfa zake bado ndiye mtu pekee anayeongoza kwa uwezo wa kutawala na kuongoza nchi! Akichaguliwa huyu DSICIPLINE YA WATENDAJI na nidhamu ya kazi itarejeshwa!
  3. Dr Asha Rose Migiro - Migiro ni mwanasiasa na mwanzuoni anayetajwa kuwa katika kinyanganyiro. CCM kuanzia uchaguzi uliopit aimekuwa ikijenga hoja kwamba "mwanamke anaweza" ili kujenga mazingira hayo 2015! Endapo hililitapitishwa basi mama huyu anaandaliwa kuchukua nchi! Ana uzoefu mkubwa wa masuala ya kimataifa; inaaminika hat ahizi juhudi za sasa za UN kusaidia mpango wa maendeleo TZ (zaidi ya nchi nyingine Africa) ni kazi ya huyu mama! Inasemekana pia atakaporejea UN itaongeza kwa kiwango kikubwa sana "footprint" yake hapa nchini! Tatizo kubwa ni kwamba bado watanzani awengi hawaamini kama mwanamke ana uwezo wa kutawala nchii hii, na pia mama huyu katika siasa "fitina" za Tanzania bado hajaimarika zaidi...
  4. Prof Mark Mwandosya - Mwandosya ana uwezo na bado ana nia ya kuwania tena 2015. Ndani ya CCM hana mvuto sana na alitupwa mbali katika mchujo wa 2005 kwa kuwa makundi ya kifisadi ya kina JK yalimbana sana. Ni msomi na tayari matunda ya ubunge na uwaziri wake yanafahamika kwa watu wa Mbeya. Tatizo lake ni mpole na kuna mashaka kwamba anaweza kuwawajibisha watumishi wazembe...ikiwemo mawaziri! Kule Zanzibar hawamfahamu kabisa....
  5. Dr John Magufuli - Ni mtu wa kazi, kila mtu anamfahamu lakini kuna kila dalili CCM hawamtaki maana wanajua akipewa shoka atakata mibuyu yote. Mpinzani wake wa kwanza ni JK mwenyewe amabye inaaminika tayari alishamtupia vijembe kkwamba anataka umaarufu lakini raisi na waziri mkuu TZ ni mmoja tu!!
  6. Samwel SItta - Huyu jamaa anakitaka hicho kiti, ana ajenda zake binafsi na ana nia ya kupambana na mafisadi. Inaaminika CCM wameweka mikakati asiombe nafasi hii! Zaidi ya hayo anaonekana kuwa ni mtu aliyeishiwa kisiasa, hana jambo jipya atakalolileta!
  7. Prof Anna Tibaijuka - Nia y ahuyu mama ilianza 2010 alipostaafu kutoka UN-HABITAT n akuingi amoja kwa moja kwenye siasa kwa kuwania ubunge! Ni msomi na ana uwezo lakini anafunikwa na uwezo na utulivu wa Dr Asha Rose Migiro. Pia wachambuzi wanasema tabia yake ya kukurupuka na majigambo vinaweza kui-cost nchi
  8. Bernard Membe - Ameonyesha nia na kuna kipindi alikuwa anapata support ya bosi wake! Wana uswahiba wa hali ya juu, siri ya uswahiba wao wanaijua wao wenyewe. Ni mwanausalama mwenye network za kishushsushu kubwa na hivi karibuni ameonekana kufany amaamuzi and/or kutoa matamshi yenye utata! CCM ina mashaka naye, kuna wasiwasi akatupwa mbali katika kinyanganyiro..
  9. January Makamba - New generation katika chama, amefany akazi na rais kwa muda mrefu na ni kijana mwenye mtazamao wa mbali, japokuwa anashindwa kuficha hisia zake na nia aliyonayo! CCM imemkumbati ana kujivunia sana uwezo wake, lakini recently uswahiba wake na Zitto na wanasiasaa wengine vijana imekuwa kikwazo kwa chama! Wana-CCM wanamuona kama ni opportunist amabaye anatanguliza mbele zaidi maslahi kuliko chama. Kashfa ya hivi karibuni kuhusu mauaji ya Nyamongo, ambayo hajaitolea maelezo ni mojawapo kati ya issues zinazotia doa kampeni zake! Zaidi ya yote, maisha yake nje ya siasa pia imekuwa ni mambo yanayohojiwa zaidi
  10. Ally Mohammeid Shein - Wote tunamjua Shein, alilazimishwa kwenda Zanzibar kuchukua nchi kulel. Baada y akuwa the longest serving VP, na then rais wa Zanzibar kun adalili kwamba ataitwa kutawala TZ na kumuachia Hussein Mwinyi visiwani...
Ndugu yangu, ukitazama hao watu utaona bado CCM ina kazi kubwa, lakini nikuhakikishie hakuna anguko linalokuja! Kila kitu kiko under control...EL anarudi, believe it or not
 
ndugu yangu jaribuni kuwa nauchungu wataifa hili jamani Sikatai Lowassa alikuwa mtendaji mzuri sana tena sana *ila Kumrudisha Lowassa kwenye madaraka makubwa ni kuliangamiza taifa.

1. lowassa atataka kulipiza kisasi kwakuwa mkuu wa nchi alimtenda vilivyo
2. Lowassa hata kubali demokrasia itawale atawaminya wapinzani na nchi itawaka moto
3.Lowassa hata weza kuliinua taifa kiuchumi

Mwenye macho yanayoona aambiwi tazama.Mkuu sijui umetumia vigezo gani mpaka ukazipata point hizo tatu.
 
Kwangu mimi kwa ccm hata angesimama malaika, baba yangu, mama yangu, shangazi, mjomba,babu au kaka yangu bado wasingeweza kunishawishi kuwapigia kura.dr. Slaa alisema ndani ya ccm hata aingie malaika bado hataweza kupambana na ufisadi.kwangu mimi taifa linaanza then chadema inafuata.
 
Back
Top Bottom