Anguko la Simba lipo jirani

Anguko la Simba lipo jirani

Kila msimu na staili yake .Umuhimu wa Manara kwa Simba umeshapita,wakati hauruhusu.Ila Simba itaendelea kuwepo na kuchukua makombe.
Mpaka sasa imechukua makombe mangapi?
 
Mpaka sasa imechukua makombe mangapi?
Kukosa makombe msimu huu imechangiwa na baadhi ya sababu ulizotaja hapo juu ila sababu ya manara sikubaliani nayo. Kuchanganya mpira na siasa ndio imenishusha morali ya kuipenda timu yangu ya Simba ila sio kutokuwepo kwa manara.

Mimi sikotayari kupigania timu ya Simba kwa ajili ya kutimiza malengo ya watu kisiasa.

Pamoja na hayo Simba haiko kwenye hatua mbaya ila viongozi wa Simba wanatakiwa kubadilika. Isingekuwa makosa waliyoyafanya msimu huu katika nyakati muhimu,Simba alikuwa na nafasi ya kuchukua kombe la shirikisho Afrika.Lakini uchawa na tabia ya wanasiasa kujipendekeza kutaka sifa ambazo sio zao viliingilia kati wakati Simba inakaribia kwenye kilele cha mafanikio.
 
Hata msimu ujao Simba haitapata kombe lolote in fact msimu ujao kwa Simba utakuwa mbaya zaidi
Simba ikivuka robo kwenda nusu club bingwa kwangu binafsi itakuwa imenipa furaha.
 
Wadau wa soka Tanzania salami kwenu.

Kwa waliofuatilia press mbili , moja ya Mo Dewji siku anaonesha Hundi ya Bilion 20 na press ya Leo ya Semaji Lao Haji Manara watakuwa wameona kitu kinaenda kutokea Msimbazi na anguko Lao lipo jirani Kwa sababu zifuatazo.

1. Uwekezaji wa Mo Dewji pale Simba umekaa Kimagumashi zaidi. Moa Dewji yupo Simba kiujanja ujanja sana na moja ya ishara NI kauli anayoirudiarudia kwamba pale Simba yeye hapati faida. Huu ni ujanja na umagumashi.

2. Kuondoka Kwa Haji Manara. Huyu ni kipenzi cha wana Simba kuliko hata Mo mwenyewe. Ushahid NI maneno ya Haji kuwa Mo amewahi mpigia sim na kumwambia watu Wanasema Haji ni maarufu kuliko Mo. Lakini pia ni mara nyingi wanaSimba wamekuwa wakitaka Mo aondoke Simba lakini hawajawahi kutaka Haji aondoke.

3. Uwepo wa Barbra . Huyu bosi inaonekana yupo pale Kwa kazi maalum ya kuhakikisha analinda maslahi ya Mo klabuni na ndio maana anafanya kila analoweza kuhakikisha hili. Barbara anamtumikia Mo na si Simba.

4. Presha ya matokeo. Kuondoka Kwa Haji Manara kumezidisha presha ya matokeo pale Simba hasa katika michuano ya kimataifa. Haji Manara alikuwa na mchango mkubwa wa kuwajenga wanaSimba Kisaikolojia kitu ambacho Kamwaga hana kipaji hicho. SIMBA itapofanya vibaya itaonekana hamasa ndani ya timu imeshuka na Simba imepoa.

5. Utamaduni wa soka la Tanzania. Ilivyo miaka nenda rudi mapacha wa kariakoo hupeana zam za kutamba na hapajapata kutokea mapacha hawa wakawa na mafanikio Kwa wakati mmoja. Hili japo ni dogo Ila linaleta dalili za anguko la Simba.
Mkuu bado unalisubiria anguko la Simba au?
 
Back
Top Bottom