Anguko la mtu mweusi kwa wakati wake

Khalifavinnie

JF-Expert Member
May 19, 2017
2,761
2,311
Habari za hapa JF sehemu pendwa kabisa kwa kupashana habari mbalimbali na kuelimishana pia, lakini leo nahitaji kuwajuza jambo moja muhimu sana kwa watu woote wenye ngozi nyeusi na machotara wote kiujumla,ni kwanini huwa tunajilaumu sanaa kwamba ni kitu gani au jambo gani limetufanya kuwa nyuma kwa kila kitu kila shuhuri na hata tukiifanya sisi baasi tunaonekana tukiwa chini ya wazungu na si sisi.

Basi swala hilo limetufanya kujidharau sana na kugubikwa na kila namna za propanda na hadithi zisizo na mashiko wala uhalisia juu yetu na hayo yote ni sababu ya kutoelewa sisi chanzo chetu je ni kipi? Pia lakini bila kusahau hata wazungu nao kutoelewa ili hali wanatuburuza kwa shughuli nyingi za kimaendeleo hapa duniani lakini nao hawatambuliki ni wapi wetoka,yote sawa lakini ni kwanini wazungu ndio wamejiwekea kuwa na mvuto wa kila mahala pa historia kwanzia katika maandiko na historia za kimiungu na hata historia za uvumbuzi wa tekinolojia mbali mbali je tunafaham wazungu hao waliopo katika sekta mbali mbali za uvumbuzi wa kiufundi wa vifaa naa mambo ya teknolojia nyuma ya pazia je walijifunza wapi? Mimi na wewe hatujajua na kubaki tuu na kiulizo hivi mtu anaweza akazaliwa na kipawa tuu cha kubuni radio yeye kama yeye akabuni na kuibuka wengine wakaendeleza tuu kwamba sasa akili za vipaji zinaibuka pale mwingine alipoishia kwanini kama ingekua vivyo baasi kisijitokeze kichwa cha mtu mweusi kikaendeleza hapo?kwanini wawe wazungu tuu?

Shida na viulizo vya hayo mambo vipo na haviishi, tumejionea waashia wa uchina hawa nao wamekuwa wazuri sana wa maendeleo, tumewaona wahindi halikadhalika race zote za watu weupe wamekuwa ni watu wa kipekee katika dunia ya sasa kwa utanashati na utimamu wa fahamu zao je unajua staha zote hawa watu walizipata wapi na je wanaweza kuwa na hazina ya utawandawazi wote wanatumia tu kwa hatua fulani na si kuvumbua kama wanavyodai hilo ni la kweli na leo nataka kuwajuza hilo.

Mnamo wa wakati wa mtu mweusi dunia ilijawa na utandawazi wetu tulikuwa ni watu wa kupendeza tulikuwa ni watu wenyw ukaribu na uongozi wetu wa kimwenendo(miungu)tulipata kutawala eneo kubwa la nchi, tulikuwa pia na ngazi elekezi zilizo njema na bora sana hatukujua kitu kijulikanacho pambano, pigo wala vita wala chuki wala kudharauliana wala kunyoosheana vidole,ilikuwa ni nchi ya upendo mmoja yenye kila pumziko safi yenye kila matendo mema, tulikuwa na ngozi za kupendeza zing'aazo kama madini ya fedha,dhahabu na hata tukawa watu wa kipekee wenye uzuri wa kushangaza, wenye nywele za kuvutia na zimelemetazo kama almasi ama hakika tulikuwa watu tulio pata kuwa bora na hata wa kushangaza sana kwa viumbe wageni.

Kwa wakati wetu tulipata kuokota wageni walio na miili dhaifu na walikuwa wadhoofu kwa kila hali kwani maisha yao yalikuwako mapangoni na mabondeni,watu hao walipata kuokotwa katika eneo la mbali na nchi yetu na tusijue ni wapi walipata kutoka bila kufahamu kama walikuwa ni chambo ya viongozi wapinzani wa mbali (miungu mingine) ambao walipenyeza uoto wao katikati pa nchi yetu, tukawapokea tukawaosha kwa kuwaondoa taka za mwili na kuwa nao jirani katika maisha tukaishi nao kwa muda wao na kuwafunza mambo kadha wakadha, pasipo kujua walitulaghai kwa kutuingizia chuki kwa kutufunza gasia na kuanza kuumaliza upendo baasi na damu zikaanza kumwagika taratibu kwa kila upande wa nchi kwani watu wakajua chuki, vita, hasira ghadhabu na hata ukubwa baasi na ikawa vita ya sisi kwa sisi huku tukijisahau tunao wageni ndani yetu ilihali tukiamini wageni wale hawajui chochote maana kila kitu sisi ndio tulikua miongozo kwao,baasi miji ikaharibika kwa ugomvi wetu ghasia kubwa kila mahala.

Wakati wa machafuko ghasia wageni wakabeba kila aina ya faida, ujuzi, maarifa na vitendea kazi kwa kuhifadhi mahala pa maficho ghasia na vita zilizuka kali mpka kufikia hatua ya kumalizana kwa kiasi kikubwa, wageni na wao wakapata kushikirikishana kutumalizia wakapata kutudhibi na kutukusanya kwa kuwa mateka tukadhoofu tukatwaaliwa na kutupwa mbali na nchi na hata tusijue ni wapi pa kuanzia,tukawa na chipuko jipya lisilo na maarifa yeyote zaidi ya kutia mkono kinywani kwani tulishapotezwa na kila kitu hata waanglizi wetu(miungu)...
 
Back
Top Bottom