Anguko la Mainstream Medias; Ni Teknolojia na sio Siasa.

Distant Relatives

JF-Expert Member
Nov 21, 2020
415
729
Kumekuwa na wimbi la Mainstream medias kama magazeti kusimamisha uzalishaji. Kumekuwa na kambi mbili za mawazo juu ya chanzo. Wapo wanaoamini ni kutokana na Serikali kubinya uhuru wa habari-POLITICS na kambi ya Pili ikiamini ni nguvu ya Social Medias-TECHNOLOGY.

Sasa muda huu nimejikuta nasikiliza Radio One. Kwenye Habari zao za siku hizi ndio habari ambazo wamezitangaza.

1. JPM amfuta kazi DED Igunga
2. Mafuriko mtwara yaathiri nyumba 29.
3. Ziara ya kushtukiza ya 2nd VP Zanzibar bandarini.
4. RC Mgwira aongoza mazishi ya familia iliyoteketea kwa moto huko Moshi.
5. RC Singida aagiza maduka yanayoshamirisha maambukizi ya ukimwi kufungwa
6. PM Kapokea madarasa Ruangwa

Habari 5/6 (90%) nilikua tayari nimezipata kupitia JF, Twitter na YouTube.

Ukichukua kasi ya ongezeko la matumizi ya internet kwa watanzania (TCRA: Mil 23 mwaka 2018), ni dhahiri kuwa Mainstream Medias iko siku za mwisho wa uhai wake na lawama kwa kiasi kikubwa ni Social Medias.
 
Nayo siasa imechangia, nakumbuka magazeti na vituo vya tv au radio kufutwa au kusimamishwa kwa muda pale wanapo criticise serikali.

Hali hii imefanya vyombo hivi kuongelea mazuri tu na kuficha mapungufu kwa uoga wa kufutiwa leseni.

Yani hata kigogo tu kafanya Twitter isipatikane Tz, Kwani tatizo lipo wapi?, mbona kipindi cha nyuma hali haikuwa hivi, mbona hata majirani zetu kenya hawana hali hii?

Sasa nauliza swali, Kigogo akija instagram na facebook inamaanisha kwamba na huko tutafungiwa??
 
Posta nao wajiandae (maana e-government itafanya kutuma barua kukoma)
Posta nimeenda Mwezi Oct kutuma EMS,kabla ya hapo nina miaka mingi sijakanyaga.

Kuna kipindi nilisikia watu wa Wizara ya Sanaa wanataka kuitumia posta kusambaza kazi za wasanii, sijui iliishia wapi!
 
Hv postal wanakaz gan ktk ulimwengu huu wa digital!?
wana kazi kubwa sana

Natumia sanduki langu la post tangu mwaka 2014 kuagiza electronics kutoka mtandaoni ambazo hazipo hapa nchini, nanunua bidhaa mtandaoni ambayo ipo marekani au ulaya, inafika posta baada ya wiki mbili.

Posta ina msaada, ila kama ni mambo ya kutumiana batua haya yalishapitwaga
 
Pengine ni wakati sasa wa Posta kujikita kwa nguvu na 'uwazi' mkubwa kwenye biashara ya bidhaa mitandaoni? Sababu ukiwasoma Jumia kwanini walifunga biashara [na hii ni sababu ya ujumla] ni kuwa watz wengi hawana imani na manunuzi ya mtandaoni.
 
Nayo siasa imechangia, nakumbuka magazeti na vituo vya tv au radio kufutwa au kusimamishwa kwa muda pale wanapo criticise serikali.

Hali hii imefanya vyombo hivi kuongelea mazuri tu na kuficha mapungufu kwa uoga wa kufutiwa leseni.
Hebu tujiulize unaweza kununua gazeti lenye habari kuwa 'CCM YAIBA KURA' na ilhali tayari umeisoma a day before, tena kwa ukamilifu wake kisa tu inakosoa mtawala?
 
Back
Top Bottom