Anguko la kidato cha pili. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anguko la kidato cha pili.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Vitendo, Jan 14, 2010.

 1. Vitendo

  Vitendo JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 597
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  FAULU wa kidato cha pili umeshuka kwa asilimia 8.3 mwaka jana, ikilinganishwa na mwaka juzi huku watahiniwa 671 wakifutiwa matokeo kwa udanganyifu.

  Sababu zilizoelezwa kwa matokeo hayo mabovu, ni pamoja na uhaba wa walimu, ukosefu wa vitendea kazi na ubovu wa miundombinu ya kutolea elimu katika shule nyingi.

  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantumu Mahiza alieleza hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana.

  Alisema idadi ya wanafunzi waliojisajili kufanya mtihani huo mwaka jana ilikuwa 394,508, kati yao wasichana walikuwa 167,961 sawa na asilimia 43 na wavulana 226,547 sawa na asilimia 57.

  Alifahamisha kwamba, kati ya idadi hiyo; waliofanya mtihani walikuwa wanafunzi 364,957, wasichana 157,233 na wavulana 207,724, idadi ambayo ni sawa na asilimia 92.5.

  Kwa mujibu wa Mwantumu, wanafunzi waliofaulu mtihani huo ni 238,267, wasichana 95,576 na wavulana 142,691.

  Alisema wanafunzi walioshindwa mtihani huo ni 126,131 ambao ni sawa na asilimia 34.6. Wanafunzi ambao hawakufanya kabisa mtihani huo ni 29,547, wasichana 10,728 na wavulana 18,819.

  "Kuna idadi kubwa ya wanafunzi ambao hawakufanya mitihani, hivyo tumewaagiza walimu wao kutoa taarifa juu ya wanafunzi hao ili tutafute njia ya kuwasaidia," alisema Mahiza.

  Alisema wanafunzi wasichana walioshindwa mitihani hiyo ni 61,374 sawa na asilimia16.8 na wavulana ni 64,757 ambao ni sawa na asilimia 17.7.

  Akilinganisha ufaulu huo na matokeo ya yaliyopita alisema: "Mwaka juzi matokeo yalionyesha kuwa watahiniwa 102,184 sawa na asilimia 26.5 ndio walioshindwa mitihani".

  Alisema kutokana na matokeo hayo, ufaulu mwaka jana umeshuka na kufikia asilimia 65.3, ikilinganishwa na mwaka juzi.

  Alisema katika mtihani wa mwaka jana kulikuwa na vituo 3726 ambavyo ni nyongeza ya vituo 218 ikilinganishwa na vituo vilivyosajiliwa mwaka juzi.

  Waziri Mahiza alibainisha kwamba, wanafunzi waliofaulu kwa alama A, B na C walikuwa 88,636 na alama D ni 149,514.

  Alieleza kuwa watahiniwa 671 sawa na asilimia 0.81, wamefutiwa mitihani kutokana na kufanya udanganyifu na uchunguzi juu ya tuhuma hizo bado unaendelea.

  Alisema matokeo yameonyesha kuwa wanafunzi wengi wamefanya vizuri katika masomo ya Kiswahili, historia, uraia na jiografia na kufeli katika masomo ya Kiingereza na hisabati.

  Alizitaja shule kumi bora katika mtihani huo kuwa ni Kibaha, Mzumbe, Ilboru, Tumaini, Msalato, Kilosa, Kilakala, Kwiro, Musoma Ufundi na Ihungo.

  Mahiza alitaja shule za watu binafsi zilizofanya vizuri katika mitihani hiyo kuwa ni shule ya Feza ya Wavulana na Wasichana, St Francis, Thomas Moore, Don Bosco, Shule ya wasichana ya Marian, Sengerema, Qeen of Apostles, Mtakatifu Joseph Kilocha na Mafinga Seminari.

  Alizitaja shule kumi za serikali zilizofanya vibaya zaidi katika mtihani huo kuwa ni Somangila, Uchindile, Tegetero, Mwanagati, Mole, Selembala, Mnolye, Igusule, Usunga na Kining’ila

  Shule za watu binafsi zilizoingia kwenye orodha hiyo ni Ngateu,Olmotonyi, Tabata Wazazi, Nkuhungu, Dodoma Central, Africana, Uyui, Ujiji, Ali Hassan Mwinyi na Zunzuli.

  Mahiza alisema kutokana na matokeo hayo, serikali imewaagiza wakuu wa shule zilizofanya vibaya katika mtihani huo kutoa maelezo ya sababu zilizohusishwa na tatizo hilo ifikapo Januari 31 mwaka huu.

  Alisema wizara iko kwenye mchakato wa kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya elimu ikiwemo ya kuongeza idadi ya walimu katika shule za kata, kutengeneza maabara za kisasa na kuboresha mazingira ya shule zake ili waweze kuongeza ufaulu, hasa katika masomo ya sayansi, hisabati ambayo wanafunzi wengi wanafeli.
   
 2. Obi

  Obi JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2010
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 376
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hisabati imekuwa ni msiba wa Taifa kila kukicha. Hivi tatizo ni waalimu wanaofundisha hili somo au ni wanafunzi wenyewe kutokuwa na uelewa wa kinachofundishwa?
  Waalimu wabuni mbinu mbadala wa kufundishia ili wanafunzi wawe na uelewa wa somo hili la sivyo litaendelea kuwa ni tatizo sugu kwa wanafunzi wetu.
  Pia serikali iboreshe maslahi ya waalimu pamoja na mazingira ya kufundishia ili waalimu wawe na moyo na kazi yao.
   
 3. r

  rimbocho Member

  #3
  Jan 14, 2010
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wizara ituambie priority zake na mpango kazi wa kufanikisha hayo malengo, si Mungai anayake, mahiza anayake magembe anayake hatutaenda hivi
   
 4. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #4
  Jan 14, 2010
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,216
  Trophy Points: 280
  aisee huko tuendako hata nashindwa kuimagine,soooo sad
   
 5. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #5
  Jan 14, 2010
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,168
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Duh, siku izi matokeo ya form 2 nayo yanatangazwa kwa press (tv, gazet) namna ii! Enzi ze2 miaka ya 90 haikua ivi.
  Na ya darasa la 4 kwenda la 5 nayo yatatangazwa basi!
  Sio mbaya lkn @ least tumeona watoto hawapendi kuhesabu.
   
 6. epigenetics

  epigenetics JF-Expert Member

  #6
  Jan 15, 2010
  Joined: May 25, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  majuzi tumesikia nusu ya watihaniwa wa darasa la 7 wamefeli, leo 30% kati ya waliofaulu darasa la 7 mwaka 2007 wamefeli ktk Form 2 exams. Haya tunasubiri fom foo tusikie data.
  Swali: hao wanaofeli wanaenda wapi? ama ndio ukifeli aidha ukaolewe, ama uoe na kupewa jembe.
  Tuongeze idadi ya shule za ufundi, na ziwe na hadhi kama shule za sekondari. Ili angalau hao wanaofeli japo waje kuwa wakulima wenye taaluma za modern agriculture, makonda, mabucha, ma mekanika, wapaka rangi wote wawe na ujuzi na taaluma ktk fani zao.
  Taifa la watu wasio na elimu karne ktk karne hii ni janga likisubiri kulipuka.
   
 7. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #7
  Jan 15, 2010
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,703
  Likes Received: 8,246
  Trophy Points: 280
  Kweli mkubwa hapo umenena,
  I can imagine vyuo vyetu vya ufundi vingekuwa na hadhi kama enzi hizo tukikua...
  Mungu ibarki Africa, Mungu wabariki wanafunzi!
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Jan 15, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,611
  Likes Received: 82,194
  Trophy Points: 280
  Kwa maoni yangu hii issue ya Wanafunzi wetu kufanya vibaya katika matokeo ya form 2, O' Level na A' Level inabidi iwemo kwenye mambo mbali mbali ambayo yanatakiwa yazungumzwe katika kampeni za uchaguzi huu unaokuja.
   
 9. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #9
  Jan 15, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hisabati Hisabati Hisabati! Kama Quadratic equations zinasumbua hivi ni nani ataweza kusolve Runge Kuta? Hawa madogo nategemea miaka kama tisa au kumi ijayo tupate Wahandisi Miongoni mwao je Taifa linakwenda wapi? Tatizo hasa liko wapi? Mfumo wetu wa Elimu au ni nini? Huwa naamini maths ni moja kati ya masomo rahisi na Mazuri sa inakuwaje?
   
 10. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #10
  Jan 17, 2010
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Prof magembe na wenzio jiuzuluni....u prof wako hauna msaada kwa taifa...hauna jipya
   
 11. PingPong

  PingPong JF-Expert Member

  #11
  Jan 17, 2010
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 933
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  Serikali ingetoa tamko rasmi juu ya mikakati iliyonayo kuhusu hili suala la kidato cha 2 kuchemka hasa hesabu na sio kutangaza tu matokeo then inaishia hapo mpaka next yr, kwa ujumla mtu asipokuwa na msingi mzuri wa hesabu anakuwa amekosa kitu muhimu sana maishani mwake sio tu kwenye fani za kitaaluma ila ktk maisha ya kila siku coz hakuna kitu ambacho unaweza kufanya bila kuapply math, hata mama anapopika ugali lazima apige mahesabu la sivyo unga utazidi, naandika kwenye pc yangu hapa kuna mahesabu yanatumika la sivyo hamtanielewa, wewe chunguza tu kwa makini tukio lolote unalofanya utangundua kuna hesabu ndani yake, hawa wanafunzi wanapofeli hesabu kiasi cha kutisha namna hiyo ina maana wanatengenezewa mazingira ya kufeli kimaisha, serikali ifanye mikakati ya makusudi kama inavyofanya nchi ikipata majanga mengine makubwa ya kitaifa au kama wanavyofanya juhudi za makusudi kuendeleza michezo kama soka basi wapeleke juhudi hizo pia kwenye elimu.....hii ni hatari!
   
 12. Masika

  Masika JF-Expert Member

  #12
  Jan 24, 2011
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 731
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sababu za kufeli ni pamoja na:-
  1:Waalimu kutofundisha vizuri (kutomaliza silabasi) na kuakikisha wanafunzi wanafaulu mitihani ya majaribio kabla ya mtihani wa mwisho
  2:Wanafunzi walio wengi siku hizi kutozingatia masomo na kufanya mazoezi ya kutosha badala yake wanacheza cheza tu
  3:Wazazi na serikali kwa ujumla kutohimiza umuhimu wa elimu kwa watoto
  4:Matatizo ya kiuchumi mfano:kutopata chakula bora, malazi, ada na upatikanaji mwingine wa mahitaji muhimu kwa wanafunzi
  5:Mwamko mdogo wa wa Watanzania katika kujikomboa kiuchumi kupitia elimu na badala yake kusubiri njia za mkato
  6:Wanafunzi kutojua mada wanazotakiwa kusoma na kuzifanyia mazoezi kabla ya mtihani wa mwisho
   
 13. S

  Simeon Member

  #13
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  1.walimu wa hesabu wamekuwa wachache hivyo wanazidiwa na mzigo,hesabu inahitaji ufuatiliaji wa karibu,utakuta shule nzima kuna mwalimu wa hesabu mmoja tu,hivyo efficiency inapungua kwa kiasi kikubwa!
  2.wanafunzi wamekuwa na negative altitude na somo la hisabati,sijui nani kawaambia hesabu ni ngumu...?
  3.motivation kwa walimu haipo,utakuta mwalimu wa kiswahili ana vipindi sita tu kwa wiki,mwalimu wa hesabu anavyo 30,na wapo ofisi moja wanalipwa sawa,kisaikolojia mwalimu lazima atakuwa de moralized
  3.serikali kwa ujumla inajichanganya,wanafunzi waliofeli form 2 mwaka juzi wote wapo form 3,hivyo hakuna kurudia darasa hata ukifeli,hii imeondoa thamani ya mtihani,na wanafunzi hawaoni umuhimu wa kusoma sana,maana hata wakifeli wataendelea tu,hii yote ni siasa yenye kuua taaluma,na hawa wanafunzi ndo watakaokuwa mawaziri kesho,na ndo watakaosaini mikataba mbalimbali.....!kuna nini fella?
   
Loading...