Cesar Saint
JF-Expert Member
- Nov 18, 2016
- 423
- 727
Habari zenu wanaJamvi
Ni wendelezo wa habari za anga za juu (Space) Tiangong-1 neno lenye maana ya "Heavenly Palace" kwa tafsiri isiyo rasmi yaani kasri ya mbinguni ina uzito unaokadiriwa wa 8.5 metric tons na urefu wa futi 34 na upana wa futi 11 (10.4m kwa 3.4m)
Kituo hiki cha anga kinajumuisha kitengi ya mafunzo na majaribio ambapo wana-anga wanaweza kufanyia shughuli zao na sehemu ya pili yenye matenki propellant na injini za roketi.
Tiangong-1 ni kituo cha anga kilichopo kwenye mfumo wa single-module kinachosimamiwa na China National Space Administration kilichorushwa mwishoni mwa mwaka 2011 kikiwa kimehudumia na wana-anga wawili wa kichina (taikonauts) mwaka 2012 na 2013. Kutokana na usiri mkubwa wa CNSA taarifa juu ya mission na habari kuhusu Tiangong-1 zimekuwa hazipatikani kwa urahisi.
Tiangong-1 iliwekwa kwenye mzunguko wa karibu na dunia takribani maili 217(350km) na katika mwinuko wa chini kidogo ukilinganisha International space station . Mashine zake zinapewa nguvu na “arrays” mbili za jua na inauwezo wa kutunza na kuhudumia mwana-anga watatu .
Msingi mkubwa wa kujenga module hii ilikuwa ni kusaidia China katika kuendeleza shughuli hizi za uchunguzi wa anga ya juu kuwa endelevu kwa kuweza kufanya “space docking” na kuweza kutengeneza kituo kikubwa kitakachoweza kupokea spacecrafts nyingi zaidi na kwenda Mars na sehemu nyingine za mfumo wa jua .
Mara baada ya kufanikiwa kwa mpango huu China walifanya mission mbalimbali kwa kutumia Shenzou 8,9,10 hii ilitokana na hapo mwanzo kwa Tiangong-1 ilitazamiwa kudumu kwa kipindi cha miaka miwili na hivyo ndio ikapelekea kurushwa kwa mfululizo wa Shenzhou 8 hii ilikuwa haijabeba mtu October 2011, Shenzhou 9 mwaka 2012 ikiwa na watu watatu ambayo iliweka historia ya kupeleka mwanamke wa kwanza wa kichina kwenye Space na June 2013 wakarusha Shenzhou 10 iliyobeba watu taikonauts watatu.
Baada ya kupoteza uongozi wa Tiangong-1 hatimaye September 2016 China wakarusha Tiangong -2 na ikafanikiwa kupokea mwendelezo wa Shenzhou 11 na ilipofika November 2016 likafanyika jaribio la “docking and refueling” ya Tianzhou-1 na ilifanya hivyo tena April,June na September 2017 na tofauti na matarajio ya kufanya hivyo kwa siku mbili docking hii ilidumu kwa masaa 6.5
Kitendo cha kuharibika kwa mzunguko wa Tiangong-1 na kupoteza kwa mawasiliano ya usimamizi wa Tiangong-1 mwaka 2016 kunaweka wazi uwezekano mkubwa wa vipande vya spacecraft hii kuingia katika anga la dunia mnamo March 30 mpaka April 2018
Hakuna wana-anga waliotembelea Tiangong-1 tokea mwaka 2013 lakini taarifa zinazokusanywa kupitia kituo hiki kimewezesha uchina kugundua uwepo wa madini na kupata taarifa za hali ya hewa ambapo inasadikika mwaka 2013 wakati wa mafuriko ya Yuyao na mnamo March 2016 zoezi la ukusanyaji taarifa likasimamishwa bila taarifa zaidi.
Bado haijawekwa wazi hasa kama China imeweza kufanya mahesabu ya kuingia kwa chombo hiki katika anga la dunia kama ilivyokuwa kwa MIR au kitakuja kama Nyati aliyejeruhiwa kama ilivyokuwa kwa Skylab mwaka 1978 na kudondokea maeneo yenye watu huko Australia
Maeneo ambayo inaweza kuangukia ni
Asante

ili iweje mkuu