Mtela Mwampamba
JF-Expert Member
- Dec 19, 2012
- 537
- 347
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinazidi kupotea katika ramani siasa za Tanzania ,Uchaguzi mdogo wa Arumeru,CHADEMA ilitumia nguvu kubwa na mipango ilizotokana na think tankers wa chama kama akina Dk Kitila Mkumbo,Zitto Kabwe,Samson Mwigamba,Prof Safari,Mabere Marando na Prof Baregu.
Pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutumia njia na mbinu zao za kisomi pamoja na falsafa yao ya Umoja ni Nguvu lakini kura hazikutosha. Mwisho wa siku CHADEMA ilishinda na Joshua Nasari akatangazwa kuwa Mbunge. Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe akiwa katika moja ya mikutano ya siasa.
Baadae uchaguzi mdogo wa Igunga,jeshi na makamanda wakatua Igunga,mikutano mikubwa ikafanyika,wakafanikiwa sana kwa kukubalika kwa wana Igunga,Siku alipotua Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, Igunga ilichafuka haijawahi kutokea kuona umati mkubwa katika mikutano Mkoa mzima wa Tabora uliweka rekodi kwani mapokezi yake yalianzia KM 5 kutoka mahala ulipo mji wa Igunga.
Kipindi hicho CHADEMA ilikuwa na mtaji wa kura 1000 tu, lakini baada ya Zitto kutua Igunga ikapata kura zaidi ya 20000 na kushindwa na CCM kwa kura chache,kiasi cha kumfanya mshindi kuhofu kushindwa uchaguzi ujao mwaka 2015.
Baada ya hapo CHADEMA ikaanza kuyumba huku ikiandamwa na migogoro ya kiuongozi uliosababisha Dk. Kitila Mkumbo,Zitto Kabwe,Samson Mwigamba kufukuzwa uanachama.
Wakati hayo yakitokea kukawa na uchaguzi mdogo wa kata 27 nchi nzima ndipo CHADEMA ilipo ambulia ushindi wa kata tatu tu huku CCM ikinyakuwa kata 23 na NCCR Mageuzi kata moja.
Baada ya uchaguzi huo watu makini ndani ya CHADEMA wakashtuka kwa kulinganisha nguvu ya CHADEMA na matokeo ya uchaguzi yalyopatikana.
Badala ya kutatua mgogoro kwa maridhiano,wenye chama wakadai kuwa Zitto si chochote,na hivyo hata akiondoka Chama kitaendelea kuimarika.
Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa Dk. Wilbrod Slaa akifafanua jambo Katika uchaguzi huo wa kata 27,CHADEMA ikatumia pesa nyingi na zana za kisasa,hila na chuki zao CHADEMA ilitumia nguvu kubwa ili kuuthibitishia umma wa watanzania kuwa Zitto si chochote mbele ya chadema iliyo mioyoni mwa watanzania.
Chama kikatumia chopa tatu na viongozi wote wa kitaifa,lakini bado kikaambulia kata tatu tu kati ya 27. Baada ya uchaguzi huo CHADEMA wakaja na visingizio na kujipa moyo,kuwa tumejitahidi lakini watu wabishi kama Yeriko Nyerere,Ben Saanane na Saidi Kubenea wakaandika makala kwenye mitandao ya kijamii (----------- forums) kuwa watu hawapaswi kubeza mgogoro wa Zitto na Mbowe.
CHADEMA bado wakashindwa kutafari kwa kina suala la migogoro yao ndani ya Chama badala yake wakaingia tena kwenye uchaguzi mdogo wa Kalenga Mkoani Iringa, viongozi wa kitaifa wakajipanga huku Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema na Mwenyekiti wake wakawa mstari wa mbele katika mashambulizi, huku Chopa zikipepea angani lakini bado wakaangukia pua.
Wakati wachambuzi wa masuala ya sayansi za siasa wakiendelea kufanya tathimini zao ili waje na uchambuzi makini uchaguzi mdogo Jimbo la Chalinze ukafika CHADEMA kama kawaida wakabeba migogoro yao na kuidumbukiza ndani ya Jimbo hilo leo hii ushindi kwa CCM tena huku mgombea wao akikimbia kupiga hata kura yake mwenyewe.
Wafuasi wa CHADEMA wanaomtii Mbowe na Dk Slaa,wakimtwaanga mfuasi anaye mtii Zitto Kabwe, nje ya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
Ukiangalia chaguzi nne zilizopita tangu Chama hicho kilipogubikwa na migogoro hasa baada ya Zitto Kabwe kutimuliwa, CHADEMA imechangia kwa kiasi kikubwa kwao kushindwa vibaya kuliko wengi tulivyotarajia.
Hoja ya Ridhiwani Kikwete kushinda kwa kuwa ni mtoto wa Rais si hoja mbele ya watanzania waliochoshwa na CCM, ndio maana CHADEMA ilishinda Arumeru licha ya kwamba Sioi Sumari alikuwa mkwe wa Lowassa moja kati ya wababe wa siasa za Arusha.
Kwa mwendo huu,wa kushindwa katika chaguzi nne CHADEMA wanapaswa kujitathimini na kuweka mikakati thabiti ya namna ya kupambana na dalili mbaya za kutoweka katika ramani ya siasa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015,hii ni kutokana na ukweli kuwa mwaka 2015 kila mmoja atakuwa kabanwa jimboni kwake hivyo huu utaratibu wa kupiga kampeni kwa pamoja hautakuwepo.
Jinamizi la vyama vya siasa kung'ara katika medani za siasa nchini Tanzania kwa kipindi cha msimu mmoja na msimu unaofuata vyama hivyo kubaki na historia ilianza kwa Chama cha NCCR Mageuzi iliyokua na wabunge 20 mwaka 1995 na katika uchaguzi wa mwaka 2000,ikaambulia majimbo sita tu na uchaguzi wa mwaka 2005 ikatoka kapa baada ya watanzania kuchoshwa na migogoro yao ndani ya Chama, huku Chama Cha Wananchi CUF wakiingia katika kinyang'anyoro hicho lakini nayo ikapotea na nafasi yake ikichukuliwa na CHADEMA.
Jeneza inayoonyesha ishara ya mwisho wa maisha ya CHADEMA katika siasa za Tanzania. Historia hii inatufanya tuanze kuiona CHADEMA kubaki na historia ya kufuata nyendo za NCCR na CUF ingawa hali ni mbaya zaidi kwa CHADEMA kwani pengine isifikishe hata wabunge sita mwaka 2015.
Hii inatokana na hatua ya kuwakatisha tama Watanzania.