Shida na raha
JF-Expert Member
- Aug 8, 2014
- 3,773
- 3,471
Nilikua na tabia ya kwenda kunyoa salun moja hivi kigamboni kwa bahati nzuri wafanyakazi wa kike walikua watatu, sasa mmoja katika maongezi ya hapa na pale tukagusia habari ya zanzibar.
Kumbe kule alishawahi kukaa mtaa mmoja hivi ninaopendelea kwenda sana kwa bibi yangu mzaa mama, urafiki ukakuwa kwa kasi ya ajabu kwa bahati nzuri hana mume nikaona kuna viashiria vya mahusiano vinaanza kuja.
Anyway nikaona isiwe tabu niendelee kumpa kampan kama rafiki yangu wa kike, kwa bahati nzuri urafiki wetu uliendelea kama wiki moja, akaanza kuniulizia nnapoishi nikamdanganya naishi kwa baba mdogo.
Alijaribu kuniulizia kazi nnayofanya napo pia nikamdanganya navua pale minazi mikinda hapo nikaanza kuona mabadiliko.
Nikimpigia sim hapokei sms hajibu na akipokea yuko buzy ananijibu nimtafute baadae, kumbe tatizo nikumwambia mimi mvuvi akaona loo! Hapa ntaambuli shombo tu.
Aliamini kazi niliyomwambia maana kwavile mi mzanzibar hakuwa na shaka na hilo, nnachowasihi ndugu zangu wa kike penda mtu usipende kazi yake.
Mapenzi na kazi ni vitu viwili tofauti sasa najiuliza imaana ningemwambia kibarua changu angenipenda???.