Angalizo kwa WanaCHADEMA - Kufuatia Vyombo vya Habari kuogopa kuripoti habari za matukio ya Lissu, sasa jukumu la kuripoti liwe la kila mmoja wetu

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
18,511
68,141
Wakuu Salaam!

Nimekuwa nikifuatilia muenendo wa vyombo vya habari vya Tanzania katika kuripoti matukio ya mgombea wa Urais kupitia CHADEMA Ndugu Tundu A. Lissu.

Nikiri wazi sijaridhishwa kabisa kwa namna vyombo vya habari vya Tanzania, tena hata vile vya binafsi kushindwa kuripoti matukio yanayomuhusu mgombea Urais huyo wa kupitia CHADEMA. Tukio la hivi karibuni ni lile lillilotokea leo ambapo Ndugu Lissu alikuwa jijini Dodoma kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea Urais.

Jana viongizo kadhaa wa vyama tofauti vya siasa walienda Dodoma kwa ajili ya kuchukua fomu, na nathubutu kusema "coverage" waliyoipata kwa upande wao haikuwa mbaya, kwangu naiona ilikuwa ya kuridhisha.

Ila kwa mgombea wa CHADEMA, hali inaonekana kuwa tofauti, na hili linanishawishi kuwaasa viongozi, mashabiki, wanachama, na wote wenye mapenzi mema kwa CHADEMA na mgombea wake.

Kuanzia sasa wawe tayari popote walipo, kila mmoja kwa nafasi yake, kuanza kumnadi mgombea Urais wa CHADEMA Ndugu Lissu ili kuweza kujaza pengo linaloonekana litasababishwa na vyombo vya habari hapa nchini kuogopa kuripoti habari za matukio yanayomuhusu Lissu.

Nasema hayo nikiamini kabisa kwamba, wingi wa wanachama, wapenzi, na mashabiki wa CHADEMA utatosha kwa kiasi kikubwa kumfanyia Ndugu Lissu kampeni kubwa zaidi, tena hiyo itakuwa ni mara tatu au nne zaidi ya ile ya kuvitegemea vyombo vya habari ambavyo vimeanza kuonesha dalili za upendeleo kwa mgombea wa CCM.

Ikibidi uongozi wa CHADEMA uanzishe media tofauti zitakazoweza kuripoti matukio yatakayomuhusu mgombea wao Ndugu Lissu, ikiwemo pamoja na kuchapisha vipeperushi vingi vya kumnadi viweze kugawiwa kwa wananchi wengi hasa wa maeneo ya vijijini.

Shime wana CHADEMA popote mlipo, huu ni wakati wa kuanza kampeni sisi binafsi, individually au ikilazimu kwa makundi, tuhakikishe kila mmoja wetu anasaidia kwa kiasi chake kumnadi mgombea wetu, iwe kuanzia ngazi ya familia, mtaa, kata, na hatimaye jimbo.Huu ni wakati wa kuwaonesha watawala kizazi hiki hakiwezi kuzuiwa kufanya kinachotaka kwa njia zozote haramu ambazo wanadhani wanaweza kuzitumia.

This is a wake up call, let's wake up, so we can shut them all up.
 
inasikitisha sana, magufur nidikteta! wananchi tumpinge na tumpuuze!
 
Back
Top Bottom