Angalizo kwa wadau wa usafirishaji

Angalizo kwa wadau wa usafirishaji

george tiru

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2018
Posts
200
Reaction score
147
Naomba kutoa angalizo kwa wadau wa usafirishaji hasa trucks. Kuna mzigo wa WFP unapakiwa Bandari ya Dar kwenda DRC na Bunia.

Huyu main contractor aliyepewa kazi ya kusafirisha huo mzigo ni matatizo matupu, si mlipaji kabisa si advance wala balance. Ukipakia gari ujue itakaa si chini ya wiki 3 hapa kabla hujaondoka. Hiyo balance ndo sahau.

Sasa basi kama utapeleka gari yako basi its your own risk, na tunaomba WFP mbadilishe utaratibu la sivyo hatutatoa magari yetu kupakia huo mzigo.

Wenye masikio na wasikie.
 
Asante kwa taarifa mkuu
Naomba tupaze sauti kwa wadau wote, hivi ninavoandika kuna gari za jamaa angu ziko bukoba wiki ya 3 anasubiri advance, sasa hyo ni kazi kweli?na yeye hakujua kama itakua hivi, kaweka mafuta yake kasukuma gari,sasa ni kilio.
 
Asante. Na office zao ziko wapi? Maana kuna mmoja yupo ushirika na yeye ana same project.
 
Naomba tupaze sauti kwa wadau wote, hivi ninavoandika kuna gari za jamaa angu ziko bukoba wiki ya 3 anasubiri advance, sasa hyo ni kazi kweli?na yeye hakujua kama itakua hivi, kaweka mafuta yake kasukuma gari,sasa ni kilio.
Huyu jamaa yako alikuwa anaenda kupitia bukavu mkuu? Kama mwenye gari hajalipwa dereva si atakuwa anakufa njaa? Inasikitisha sana
 
Mkuu budget movers siyo main contractor...
Kampuni yetu pia ya makundi transport tuna huo mzigo na siyo kuwa ndo main contractor.
WFP wana kitu wanaita counter offer so wote tuliojaza RFQ tumepewa na tatizo la budget movers ni la kampuni yao kaka.
 
majungu gani tena , hapa sio fb au instagram, tunaambiana ukweli tu, km huwezi kazi tutakwambia tu, hatutaki usumbufu.
 
Mian contractor ni Budget Movers, kuna jamaa anaitwa Emmanuel na James
Acha kuchafua watu na kampuni zao tafadhali, nakushauri ungeweka hapa mkataba mlioingia na hiyo kampuni lingekuwa jambo zuri katika kujenga hoja yako.

Pili unapotoa taarifa hizi tambua watu wametumia miaka mingi kujenga brand katika biashara zao, sasa wewe unatoa habari ambayo huna hata nakala za ushahidi wowote ule, lengo lako ni kumharibia au ni nini?

Kama una mkataba naye nenda ofisi ya WFP ukatoe malalamiko yako na si hapa.
 
Back
Top Bottom