Angalizo kwa viongozi wanao endesha magari !!!

GeniusBrain

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
4,315
306
Wakati tupo bado tuna majonzi yakuondokewa na mpiganaji mwenzetu Ndg. Regia Mtema kutokana na ajali ya gari na mazingira mazima ya chanzo cha ajali yake. Ilivyo na inavyo julikana ni kuwa viongozi km wabunge, mawaziri nk hupewa pesa yakuwalipa madereva wao kutoka mamlaka zinazohusika.

Kwa maana hiyo , basi tunawaomba waajiri madereva ambao ni qualified kwa kazi hiyo kuliko wao kujipa jukumu la kuendesha magari hayo hasa hasa kwenye safari ndefu. Hii kwanza itaongeza ajira na vile vile itapunguza ajali kwani wao sio professional drivers, wawaajiri watu wenye professional hiyo waifanye kazi hiyo.
 
Hili nalo neno la msingi.AMINI USIAMINI DEREVA PROFESSIONAL ana UWEZO MKUBWA WA KUOKOA AJALI.BINAFSI NISHANUSULIKA KUPATA AJALI mbaya MARA 2.ZAIDI YA MUNGU KUTOTAKA DEREVA WANGU ALIKUWA NA MAAMUZI YA BUSARA MPAKA RAHA.HAKUWA ANAPANIKI Hata kidogo....nina amini mikasa aliyokuwa anapata huyu dereva wangu ingekuwa hana uzoefu na kazi yake tungekuwa tushaanguka....Barabarani unapokuwa unasafiri safari ndefu kuna mauza uza kuliko maelezo.... J
 
Nadhani suala la umakini zaidi katika utoaji wa leseni za udereva ni muhimu sana.
 
Back
Top Bottom