SoC03 Angalizo kuhakikisha ulinzi wa mtoto mtandaoni

Stories of Change - 2023 Competition

Mamshungulii

Senior Member
May 3, 2023
124
66
Ingawa watoto wanatofautiana kimalezi kulingana na maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya eneo husika .Watoto wetu wanakua katika enzi ya kidijitali. Wapo ambao wanatumia vifaa kwa kila kitu, kuanzia kujifunza hadi shughuli za kufurahisha.

Kwa wengi wetu Mtandao, na programu zetu zote zimetufanya tuunganishwe zaidi kuliko hapo awali. Ingawa hii inasaidia, pia inaleta athari nyingi.

Zaidi ya theluthi mbili ya programu za simu zinazoweza kutumiwa na watoto hukusanya na kutuma taarifa zao za kibinafsi kwa sekta ya utangazaji, kulingana na utafiti mkuu mpya ulioshirikiwa na kampuni ya programu ya ulaghai na kufuata sheria za kimtandao.

Watoto wetu wanahitaji kujifunza jinsi ya kuwa salama mtandaoni, ili kujilinda mtandaoni.

Angalizo kwa mtoto
1. Mtoto hapaswi kutumia mitandao bila idhini ya wazazi au walezi.

2. Mtoto anashauriwa kuepuka kuwasiliana na watu asiowafahamu kwenye mitandao.

3. Mtoto anashauriwa kutokuchapisha taarifa binafsi kuhusu yeye binafsi,mzazii,au mlezi kama vile tarehe ya kuzaliwa, anwani ya makazi na nywila.

4. Mtoto anashauriwa kutokuchapisha kitu kingine chochote kuhusu watu wengine bila ridhaa yao.

5. Mtoto anashauriwa kuepuka kutoa au kuchapisha taarifa hatarishi kama vile picha au video za utupu ,vurugu au vitisho.

6. Mtoto anapswa kuelewa mipangilio ya program za mtandaoni na ni muhimu kuisoma mikataba ya faragha kabla ya kutumia program yoyote mitandaoni, vinginevyo inaweza kufanya taarifa za mtoto kuweza kuingiliwa au kuonwa na watu wengine psipo mtoto kujua.

7. Mtoto inamlazimu kuzuia mtu yeyote anayetuma maoni ya kusumbua ,kukutishia ,auu yasiyofaa kuhusu mtoto huyo na inampasa kuripoti kwa mtoa huduma wa program husika au kituo cha polisi cha maeneo ya karibu ambappo mtoto huyo anaishi.

8. Mtoto anapaswa kukumbuka nywila na kutambua kwamba ni siri yake hivyo inambidi kutumia programmu za kujikinga na virusi vya kompyuta na kuhakikisha program hiyo inahuishwa mara kwa mara.

Angalizo kwa wazazi/walezi

1. Wazazi wanashauriwa kuwahamasisha Watoto kutumia mtandao ili uwasaidie kwenye masomo yao kitaaluma zaidi na si vinginevyo .

2. Wazazi wanashauriwa kuzungumza na Watoto juu ya matumizi sahihi na salama ya mtandao ikiwemo mitandao ya kijamii ambayo huruhusu watumiaji wake kushiriki picha ,video ,na majadiliano kati ya marafiki au wageni.

3. Inashauriwa kuwafundisha Watoto namna ya kujifunza kkulinda taarifa binafsi Kwa kawaida siyo salama kuchapisha taarifa binafsi kama vile namba za simu ,anuani,nywila,namba ya kadi ya benki.ikiwa wahalifu wanaweza kuzipata taarifa hizi inaweza kuwarahisishia kuzitumia vibaya dhidi ya mtoto au familia na watu wa karibu.

4. Mtoto anapaswa kuhamasishwa kutoa taarifa kwa mzazi /mlezi au mtu wa karibu pale endappo atakutana na tatizo lolote mtandaoni .Ikiwa mtoto wako anapata tatizo mtandaoni inashauriwa mzazi au mtu wa karibu na mtoto mkubwa kumsaidia mtotokuwasiliana na watu wa mtandao au mamlaka ya mtandao kuepuka kuendelea kukumbana na maudhui yasiyofaa au matukio hatarishi mtandaoni hata kama mtoto ana uwezo wa kufanya kila kitu wa usahihi.

5. Wazazi wanapaswa kujifunza na kuweka udhibiti ikiwa ni Pamoja na kuchuja maudhui yasiyofaa kwa kutumia program maalumu za kompyuta za kuhimili komputa za wazazi kwenye vifaa vyote vinavyotumiwa na mtoto kuingia mtandaoni.

6. Wazazi wanapaswa kuwawekea Watoto mipaka ya mambo ambayo Watoto wanayaweza na yale mambo hawayawezi kuyafanya mtandaoni. Kwa kuweka mashartii kwa Watoto kutasaidia kuwafanya watambue wajibu wao na mipaka yao pindi wawapo mtandaoni .Sio lazima kungoja jambo hatarishi limtokee ndio kumkanya.

7. Wazazi wanashauriwa kujifunza mambo mbalmbali kwa upana kuhusu mtandao hii itasaidia sio tu kuelewa athari zilizopo bali itawezesha kutambua namna nzuri ya kuwasimamia na kkuwaelekeza Watoto.

ENDAPO WATOTO WATATUMIA MITANDAO BILA USIMAMMIZI WA WAZAZI AU WALEZI WANAWEZA KUKUTANA NA CHANGAMOTO ZIFUATAZO:

A. KUKUMBANA NA MAUDHUI YASIYOFAA

Maudhui ya ngono na picha za utupu,matukio ya kkiuhalifuna biashara haramu ,Pamoja na Habari ambazo hazifai kuangalia mtoto zinaweza kumpotosha.

B. KUWAFANYA WATOTO KUWA WATUMWA WA MTANDAO

Fursa mbalimballi zinazokuwepo kupitia mitandao kama vile michezo ya kompyuta,mitandao ya kijamii,katuni na muziki huwavutia sana Watoto ambavyo hupelekea Watoto hawa kuwa watumwa wa mtandao.

C. KUWAFANYA WATOTO KUPAKUA PROGRAMU HATARISHI AU KUWEKA VIRUSI VYA KOMPYUTA

Wakati Watoto wanatumia hivyo vifaa wanaweza kupakua program hizo kupitia tovuti hatarishi ,kubonyeza viunganishi hatarishi au kufungua viambata vya barua pepe vilivyo na virusiiii vinavyoweza kuathiri kompyuta,na hivyo husababisha uharibifu wa taarifa na vifaa vya kielektroniki.

D. KUWAFANYA WATOTO KUWASILLIANA NA WATU AMBAO HAWASTAHIKKI AU WASIOPASWA KAMA WATOTO KUWASILIANA NAO KAMA VILE
a) WANYANYASAJI WA MTANDAONI

Hawa wanyanyasaji hulenga kuwanyanyasa Watoto kisaikolojia na kuwasababishia Watoto kuwa na hofu Pamoja na msongo wa mawazo.

b) MAFATAKI WA MTANDAONI
Hawa huwalaghaii Watoto kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi na kuwafundisha kupelekea mmomonyoko wa maadili kwa Watoto.

c) WAHALIFU WA MTANDAONI
Hawa wakianza kuwasiliana na Watoto huwalaghaii na kuwafanya watoe taarifa aidha za Watoto wenyewe,wazazi au watu wa karibu na Watoto.

Ni muhimu sana kuzingatia malezi ya mtoto kwa wakati wote kuhakikisha unafuatilia kwa ukaribu kuanzia anapokuwa shuleni, nyumbani, barabarani na mahala pote anapokuwa na wenzake au peke yake ili kujua vifaa anavyotumia kujifunza na watu wa karibu wanaohusika kumfundisha.

Ipo haja kutokuwaachia walimu pekee kkuwafundisha nidhamu na maadili Watoto ,ushirikiano mzuri baina ya jamii, wazazi na walimu huleta matokeo mazuri kwa makkuzi yam toto.
 
Watoto wakimaliza mitihani wazazi wajiandae,siku hizi watoto wadogo wanahadaika na simu hivyo kupelekea mimba za utotoni au wizi na uporaji???baada ya darasa la saba wazazi/mzazi/walezi/mlezi umejiaandaaje???
 
Back
Top Bottom