Angalizo hukumu jimbo la segerea.

Angalizo hukumu jimbo la segerea.

Chillipo

Member
Joined
Mar 27, 2012
Posts
37
Reaction score
6
Katika hatua nyingine, Shahidi wa 14 wa upande wa wadaiwa katika kesi ya Uchaguzi Jimbo la Segerea, Samuel Bubegwa amekiri mahakamani kuwa matokeo yaliyompa ushindi Mbunge wa jimbo hilo, Dk Makongoro Mahanga wa CCM, yalitangazwa bila kura zenye migogoro kutatuliwa.

Bubegwa ambaye ni Mkuu wa Idara ya Usafishaji wa Manispaa ya Ilala na ambaye pia alikuwa Msimamizi Msaidizi Ngazi ya Jimbo hilo (ARO), alisema hayo jana alipohojiwa na na Wakili wa upande wa madai, Peter Kibatala.

Kesi hiyo namba 98 ya 2011 inasikilizwa na Jaji Profesa Ibrahim Juma na ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea nafasi hiyo kupitia Chadema, Fred akipinga matokeo yaliyompa ushindi Dk Mahanga, akidai kuwa sheria na taribu za uchaguzi zilikiukwa.

Dk Mahanga anatetewa na Mawakili Jerome Msemwa na Aliko Mwanamanenge na washtakiwa wengine, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala wakitetewa na Mawakili wa Serikali , David Kakwaya na Seith Mkemwa.

Akiongozwa na Wakili Mkemwa, shahidi huyo alidai kuwa walipokea fomu za matokeo ya ubunge kutoka katika vituo vyote 749 na kwamba baada ya kufanya uhakiki, hawakuona kura zenye migogoro.

Alidai kuwa baada ya uhakiki walianza kujumlisha matokeo kwa kusoma matokeo ya kila kituo kwa kila mgombea kuanzia saa nne usiku na kumaliza saa nane.

"Baada ya kumaliza kujumlisha tulimwita msimamizi (wa uchaguzi wa jimbo) ambaye alifika na kusaini fomu za matokeo na kisha akaenda kutangaza matokeo," alidai shahidi huyo.

Alisema wakati wote wa mchakato huo tangu kuanza majumuisho hadi kutangazwa matokeo, Mpendazoe hakuwepo wala wakala wake na badala yake walikuwapo mawakala wawili tu wa CCM na CUF pamoja na Dk Mahanga.

Akihojiwa na Wakili Kibatala ambaye alimuonyesha baadhi ya Fomu namba 21B za matokeo ya kura za ubunge kutoka vituoni alikiri kuwepo kwa kura zenye migogoro na kudai kuwa hajui kura hizo zilikopotelea na kukiri kuwa majumuisho ya kura ambazo Dk Makongoro alitangazwa mshindi, yalifanyika bila kura zenye migogoro kutatuliwa.

Lakini wakati akihojiwa na Mawakili Mwamanenge na Kakwaya, shahidi huyo alidai kuwa hakukuwa na kura zenye migogoro kwa kuwa hawakukabidhiwa kutoka vituoni na kwamba kiutaratibu, kura hizo hujazwa kwenye fomu maalumu na kufungwa kwenye bahasha.
Source: Mwananchi newspaper
 
Mabilioni ya wavuja jasho yanazidi kutafunwa kwa kutumia chaguzi ndogo ndogo ama kweli siasa ni hatari.
 
Source Mwananchi news paper

Na hii je imekaaje, kwani mahakama hutowa haki?
 
HILI LI NCHI PUMBAVU SANA!
Misaada yote itaishia chaguzi ndogo!
Anyway,CHADEMA Tunaongeza majimbo,though at cost of our economy!
 
Hapa Mahanga hachomoki, sema kwakuwa mahakama ziko chini ya Magamba, lolote linaweza kutokea, imani yangu ni kwa jaji Professor.
 
Mahanga alishajua tangu mwanzo hii kesi hawezi kushinda, ndio maana siku hizi amekuwa mpole kupita kiasi. hata bungeni haendi mara kwa mara...
 
Mabilioni ya wavuja jasho yanazidi kutafunwa kwa kutumia chaguzi ndogo ndogo ama kweli siasa ni hatari.

Inaboa sana kwa kweli. Hivi kwa nini tusibadili katiba na kumpa ubunge yule eliyekuwa anafuatia kwa wingi wa kura mara ubunge wa mtu unapotenguliwa? Cant we go one step further? Gharama za marudio ya uchaguzi ni kubwa
 
Mxiiiii Arusham tuna retain na hili la sega dance (segerea) tunalichukua. CCM nani anawapenda wezi nyieee
 
Usije ukashangaa kesi hii yenye ushahidi wa wazi kabisa, hakimu akatupilia mbali madai ya Mpendazoe, hapo ndo utajua Tanzania ni zaidi ya uijuavyo, let wait and see what gonna happen, stay tuned
 
Kama kweli Arusha haki imetolewa, na huko segerea wafanye hivyo haraka sana.
 
Sisiemu wamekasirika Arumeru kwenda CDM,hila hili la Arusha mjini imekula kwao CDM watalamba zaidi ya 90%! Tunasubiri Fred Mpendazoe alambe Segerea! Sisiemu inaweweseka!
 
hivi uchaguzi wa rais kwa nini hatukushitaki kaiba kura ili urudiwe?
 
Back
Top Bottom