Angalieni kitu nilichopata TANESCO

Angalieni kitu nilichopata TANESCO

Ni maumivu ila mezea tu si vizuri kuanika juani TANESCO ni ubatili tu
 
umeme ni bei sana jamani ukiangalia na hili joto la dar lazima uwe na umeme angalau wa feni
 
shamba la bwana kheri. kila mtu anavuna anavyo jisikia.
 
mambo haya hayafai, tanesco wanatakiwa wakokotoe bei mpya ya unit ya umeme ikichukulia na ile bei ambayo wamekukuwa wakitulipisha zaidi ili wapate kuilipa IPTL, bei ya umeme yaweza kuwa hata 100 kwa unit kabla hata gesi ya mtwara haijaanza kutumika. ni uadilifu tu unataikiwa hapa kwa viongozi
 
Nadhani hicho unachotaka kuniambia nilishafanya,TANESCO waliniambia Mpaka nitimize mwaka.

Kiukweli kabisa hapo kinachofanya kazi ni software inayotoza pesa na kwa units. Mambo ya electronics wenyewe wazungu sie kwetu huku tunajikongoja.

Jaribu kubadili tariff kama matumizi yako sio makubwa.
 
Sababu ni ESCROW.......
BUNGE LEO VP KUHUSU ESCROW?
 
ivi kwa sasa unit moja ya umeme ni Tsh ngapi?
 
Gharama zipo juu ingawa inaonekana kuna mwezi hukulipa ndio maana time based imekuwa double( Tsh 6734.4 lazima kila mwezi uilipe zidisha kwa miezi miwili, 13,468.80). Wao wanakomba pesa zetu tunalipa sisi. Tuseme yatosha sasa kwa vitendo.
 
LUKU
Ref BI88BN522
Meter 37135271479
Receipt EVG259343132
Units 7.90kWh
0538 2831 0976 5471 7881
Cost TZS 2,931.20
Timebased TZS 13,468.80
TOTAL TZS 16,400.00
Service charge kwa mujibu wa tariff rate yako. Inaweza kuwa hujanunua muda wa miezi miwili.
 
Itabidi niende tanesco wakanielekeze haya majedwari yao
 

Attachments

  • 1416569860158.jpg
    1416569860158.jpg
    88.6 KB · Views: 240
  • 1416570168473.jpg
    1416570168473.jpg
    56.4 KB · Views: 222
  • 1416570231477.jpg
    1416570231477.jpg
    64.6 KB · Views: 205
hapo kulikuwa kuna deni la time base ya mwezi uliopita ndio maana wameibado
 
Huu ushenzi unaoitwa service charges huwa mie sielewagi kabisa,mbona vocha za simu tukinunua hakuna service charges? Huu wizi lazima tuutokomeze kama sijanunua umeme mwezi huu kwanini mwezi unaokuja wanikate? Hizo service charges tunazolipia hawajarudisha tu gharama zao? Aisee uchaguzi wa mwaka 2015 lazima wagombea uraisi watuondolee huo ushenzi.
 
Huu ushenzi unaoitwa service charges huwa mie sielewagi kabisa,mbona vocha za simu tukinunua hakuna service charges? Huu wizi lazima tuutokomeze kama sijanunua umeme mwezi huu kwanini mwezi unaokuja wanikate? Hizo service charges tunazolipia hawajarudisha tu gharama zao? Aisee uchaguzi wa mwaka 2015 lazima wagombea uraisi watuondolee huo ushenzi.

time will tell...!
 
Kuna kautaratibu unatakiwa wajanja wakuelekeze ili uwwze kuepukana na makato makali ya aina hiyo

Sasa si useme lakini mimi najua timebased ni kama 6000 kila mwezi hiyo haina mjadala,sema tu hiyo 6000 ni kiwango kikubwa sana,sababu katika bei ya unit pia kuna kodi,yaani hawa mafisad unit moja si chini ya TZS 375 na matumizi ya kawaida tena hapo hutumii jiko au microwaves na vikorombwezo vingine matumizi kwa siku ni kama unit 3-4 hapo
umejibana.
 
Back
Top Bottom