Angalia soma chukua hatua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Angalia soma chukua hatua

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by tembaisdor, Oct 30, 2012.

 1. tembaisdor

  tembaisdor Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Nilipoingia katika mahusiano naye nilimuamini, nikampa kila kitu nilichoweza. Nakumbuka enzi zile nyumbani tulikuwa tuna ng’ombe, niliiba maziwa kila siku na kumpelekea kwao. Akanenepa!! Penzi letu likawa huru alipoanza maisha yake mwenyewe. Sikuwa najua lolote kuhusu mapenzi. Alinifundisha. Nikaegemeza maisha yangu yote kwake. Akanifanya nikawa mtumwa wa ngono kila nikienda chumbani kwake. Kama haikutosha sasa akaanza kunifundisha kunywa pombe. Niliamini kuwa ndiye mume wangu mtarajiwa, kwa nini nikatae? Nilimkubalia kila kitu. Alinilazimisha ngono hata nilipokuwa katika siku zangu. Kweli nilikuwa msomi na niliyajua madhara ya kufanya hivyo lakini sikutaka kumuudhi huyo niliyeamini kuwa ni mume wangu. Nilipenda tututmie kinga lakini aliipinga sana. Nikapata mimba ya kwanza!! Hakuwa na pesa lakini alinilazimisha niitoe. Nikaiba pesa nyumbani nikafanya alivyotaka. Kwa mara ya kwanza nikatyoa mimba. Haikuniuma sana!! Niliamini kuwa ni yeye atakuja kunioa na atanifichia aibu hii. Nilitegemea sasa tutaanza kutumia kinga. Lakini hapana haikuwa hivyo. Aliendelea kunilaghai. Tayari aliujua udhaifu wangu. Alinishika hapa na pale. Nikishtuka tayari amefanya anavyojua. Pombe kidogo na nyingine kidogo. Nikazoea lakini nikawa nawahi kulewa. Akautumia udhaifu huu kunifanyia jambo baya lililonifanya niandike haya kwako. Akaniingilia kinyume na maumbile. Alinilawiti!! Nilishindwa kumshtaki popote. Nikavumilia kwa kuwa alikuwa mume wangu mtarajiwa. Mume asiyejulikana hata kwa wazazi. Mchezo ule ukaendelea. Akajitetea eti hataki nipate mimba tena, hivyo hiyo ni mbinu mbadala. Najuta kumuamini!! Lakini huyo alikuwa mume wangu. Miaka ikapita, ule urembo wangu niliozoea kuuona katika kioo ukatoweka, simu za mara kwa mara kutoka kwake zikatoweka, akawa mkali sana kwangu. Hakutaka niende kwake. Wakati huo nilikuwa nasoma chuo. Pesa ya mkopo ikitoka ananitafuta na tunakuwa marafiki tena. Anasema ananipenda na atanioa. Ananilewesha na kunitumia kinyume na maumbile. Pesa ikiisha na mapenzi yanaisha nabaki mwenyewe katika msoto. Sasa akaanza kubadilisha wasichana waziwazi. Ningesema nini mimi? Ninajua alishindwa kusema neno moja tu. Tuachane!! Nilijua tayari ameniacha!!! Afya yangu ikadolola sana, nikalazimika kwenda kupima hospitali. Sikuwa na virusi. Nikapewa ushauri nikautumia. Siku zikasonga nikampata mwanaume mwingine. Huyu alikuwa ananijali sana. Nikaanza kumsahau yule aliyenitenda. Nilipomaliza chuo akajitambulisha nyumbani na alitaka kunioa. Akanio kweli. Maisha yakaanza. Mwaka wa kwanza, mwaka wa pili na hadi wa tatu. Sikuwa nabeba mimba. Mume wangu alikuwa mvumilivu sana, hakuwa hi kunilaumu. Lakini niliumizwa na mawifi. Nikaamua kwenda hospitali. Nikaambiwa kizazi change kiliharibiwa kwa kutoa mimba mara kwa mara. Pia mapenzi ya kinyume na maumbile yamenivuruga kabisa. Nililia sana huku nikimkumbuka yule aliyeuleta uchungu huu kwangu. Dunia haikuwa mahali pangu sahihi. Nimekuandikia barua hii mdogo wangu. Uisome mwenyewe!! Lakini uwasimulie wengi baada ya kifo changu. Uwasimulie bila kuchoka wasichana wa kileo wanaodanganyika na kufanya mambo magumu kuwaridhisha wapenzi wao. Waambie watakufa kwa mateso kama mimi. Wasipokusikiliza usijisikie vibaya maana hata mimi nilikuwa siwasikilizi watu waliponambia lolote kuhusu yule mume mdanganyifu. Sitajiua lakini nitakufa kabla ya wakati!!! Nimekuandikia wewe kwa kuwa u mwandishi. Japo kwa sasa u mtoto mdogo najua utaipata nafasi siku moja ya kuwafikishia wasichana hawa. Usilie kwa sababu nitakufa. Lia kwasababu mwanaume mwenzako AMENITENDA HIVI!!! TAFADHARI TAFAKARI
   
 2. No admission

  No admission JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 26, 2011
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakika yasikitisha ila sikio la kufa halisikii dawa
   
 3. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Duh mwili umenisisimka wakat nasoma hii sred thanx God its just a story....
   
 4. Lateni

  Lateni JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 11, 2012
  Messages: 685
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Jamani kuna mambo magumu kwenye maisha, hua naumia sana nikikumbuka mistakes ambazo nilishazifanya huko nyuma, lakini pindi ninaposikia kua kuna watu wengine wenye mambo makubwa kuliko hata ya kwangu, najikuta napata moyo wa kuendelea kuishi.
   
 5. Majigo

  Majigo JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 5,418
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  umenena!!
   
 6. Lateni

  Lateni JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 11, 2012
  Messages: 685
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Unajua mara nyingi ukipatwa na matatizo, unayaona kama ni makubwa sana, na ni wewe tu unayapitia, lakini ukipata kusikia ya watu wengine utajifunza kitu, na pengine ukapata faraja. Ukweli unao uma ni kwamba , kuna mistakes mtu huzifanya , badae akaja akajuta na kutamani muda ungerudi nyuma ili arekebishe baadhi ya vitu, lakini life haiwezi kukupa tena chance hio.
   
 7. J

  Juma. W Senior Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 131
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Maisha ni matukio. Kukata tamaa ni dhambi kubwa. "Change all problems into challenges and move ahead".
   
 8. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  This is how most of our girls alike,look to those so called Bongo movies stars!
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Hakika inatikisisha kweli,vipi shigongo umempelekea copy?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. L

  Luluka JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mbona umecopy na kupaste bila kuaknowledge source!??hii aliandika George Iron mwandishi wa vitabu..mtendee haki please!!
   
 11. T

  Tetra JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 1,523
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mapito Mazito
   
 12. kazikubwa

  kazikubwa JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mzee umenena, umbea ukiisha nchini jamaa atalala njaa.
   
 13. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Duh!Bora ni story tu na ibaki kuwa hivyo!Inasikitisha sana aisee!
   
 14. KIKUNGU

  KIKUNGU JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 853
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Vapanga mdugu wane ITEGAMATWI?Hii yaweza kuwa story based in true story,nimeishi na naendelea kuishi nimeyaona zaidi ya haya.Can you imagine mtu kama huyu halafu anakuja kupata HIV then full blown AIDS,tena ile ya miaka 80's/90's ambayo mgonjwa aliyekua na kilo 100 anayekuja kuzikwa hata kwenye mfuko wa rambo anafit?Believe me,nimeona wadada/wakaka yakiwakuta hayo.Tujiombee na tuwaombee na wengine yasije tukuta/wakuta
   
 15. SWEEPER

  SWEEPER JF-Expert Member

  #15
  Oct 30, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  inatokea zaidi ya hii story in real life situation.... Men' s character vs Women character in action
   
 16. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,631
  Likes Received: 2,055
  Trophy Points: 280
  Na hii ndio inawafanya watu wasichukue maamuzi magumu pindi wanapopata matatizo kwa kuwa tatizo ambalo mtu analiona kubwa akienda kwa mwingine anamkuta ana tatizo kubwa zaidi yake. Ukifanya uchunguzi usio rasmi utagundua kwamba wengi wanaojiua kutokana na matatizo mbalimbali huwa ni watu ambao matatizo yao walikuwa wanayatatua wenyewe bila kushirikisha watu na mwisho wa siku yanawashinda na kuchukua maamuzi magumu but kama wange-share problems na other people huenda wangeahirisha kwa kuwa matatizo yao wengine yangeonekana ni madogo
   
 17. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #17
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  duh, nafasi ya mpenzi wa kwanza ni kubwa sana kwenye lifestyle ya mapenzi hasa kama ulianza kwenye umri mdogo.
   
 18. KIKUNGU

  KIKUNGU JF-Expert Member

  #18
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 853
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Jodoki Kalimilo,umesema kweli kabisa hasa sisi waafrika hatuna utamaduni wa kuomba ushauri nasaha pindi tunapopata matatizo na haswa kama huko close na ndugu zako au marafiki.
   
 19. KIKUNGU

  KIKUNGU JF-Expert Member

  #19
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 853
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  You are absolutely right,Kongosho
   
 20. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #20
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Nimeisoma na hadi sasa macho yangu yanawasha kwa kulengwalengwa na machozi. Naumia kwababu ya maumivu ya huyu dadaetu lakini pia naumia kwasababu naendelea kuwaona wadogo zetu wakidanganyana katika jina la "kupendana". Its not only touching but also paining!!!!
   
Loading...