View attachment 427650
Katika hili nampa Rais wetu safi sana. Mitandao ya jamii imejaa sifa kemukemu kuhusu rais Magufuli akiongea na wandishi wa habari punde tu baada ya Rais Uhuru kumaliza hotuba yake ambayo yeye aliongea taratibu.
Rais wetu alipoaanza kuongea alianza taratibu na saut ya kawaida. Lakini alipofikia kugusia kidogo mafanikio ya watanzania katika kupambana na ufisadi.
Rais aligeuka kuwa kama MHUBIRI huku akiinua mikono hewani kusisitiza pointi zake kwa HEKIMA huku AKIPIMA kila neno na kusisitiza point zake na kuinua sauti yake kidogo kama vile anahubiri.
Katika kusisitiza Magu alichapa KIZUNGU kikali akitoa mfano wa somo la Chemistry nakusema Uhuru{ Kenya} na Magufuli {Tanzania} ni kama catalyst katika kuleta mageuzi kati ya hizi nchi mbili!
Hongera kwa kuondoa HOFU ambayo ndugu zetu walikuwa nayo.
Nakuendeleza uhusiano mwema kati ya nchi hizi mbili ambazo wakenya waliguswa sana uliposema Huwa mnaongea na Kenyatta mara kwa mara kwa njia ya simu na pia kuwa WAKENYA ni wa kwanza katika afrika kuwa WAWEKEZAJI wakuu wakiwa na makampuni 500 na kitu na yameajiri zaidi ya watu 56, 000 nchini Tanzania hivyo kuondoa FITINA na uchonganshi!
Hongera!