Kuna SPORTS na ENTERTAINMENT
So mieleka inayozungumziwa hapa ni ENTERTAINMENT na sio SPORTS
Ipo mieleka ya SPORTS ambayo washindani hawapigani bali kuangushana chini tu
Wenzetu USA kodi zinakatwa kulingana na makundi mbalimbali, sasa hili swala liliwahi kuleta mzozo kama hii mieleka ikatwe kodi kwenye category ipo SPORTS au ENTERTEINMENT
Baada ya majadiliano ikabainika hii ni ENTERTAINMENT na si SPORTS
So tujiulize nini tofauti ya SPORTS na ENTERTAINMENT?
Kila kinachofanyika kwenye ulingo wa mieleka kimepangwa kwa uangalifu mkubwa wa kitaalamu
Ingawa kuna wakati wanaumia au kuvujika ulingoni na hii ni kutokana na makosa ya timing nk
Tunaposema FAKE hatumaanishi hawa rukiani wala kuangushana, la hasha bali yale kwa lugha rahisi ni mapambano ya maigizo, unatakiwa kuwa na mazoezi na mafunzo maalumu ya muda mrefu na body yako iwe imara na kubwa ili kufuzu kucheza maigizo yale kwa ufanisi na kuwa safe, maana ina involve kusukumana kubebana kuangushana kurukiana nk vitu vinavyotaka umakini wa hali ya juu kupunguza risk ya kuumizana
Kwahiyo wanachokifanya pale ulingoni ni kweli lakini kimepangwa kwa kufanyiwa mazoezi kuleta burudani, aina ya viti,fimbo,minyororo wanavyopigana navyo na vitu vingine ikiwemo wanapoangukia iweni mezani au wapi,sehemu wanazotakiwa kupiga, vyote vimepangwa na kuwekwa vitu ambavyo havitaleta madhara kama tunavyodhania waangaliaji,
Kuhusu watu kujaa kwenye maonyesho hakuna tofauti na kuangalia maigizo,opera au hata sinema
Na uzuri wa hii ni kwamba kuna watu bado wanaamini wanachokiona pale ni sawa na wanvyoona pambano la Tyson na Bruno
Pamoja na hayo yote lakini uzuri mwingine ni kwamba kila mchezaji anambwembwe zake binafsi na anachagua njia yake ya uvaaji,upigaji wake wa ushindi unique(napenda wa Ray mysterio)anavyoingia ulingoni nk Hii inaongeza utamu wa kuangalia maigizo haya ya mieleka