Angalia haya ya fisadi Chenge!

Ukichaa hautoshi, wafe kabisa tuwazike!! halah!!

Mmmmh! naogopa hapo.

Hata kama tunamchukia mtu kwa kosa lake la kutuibia pesa zetu ambazo zingelitosha kuondoa baadhi ya matatizo yanayotuzunguka, sidhani kama tunatakiwa kufikia sehemu ya "Kumuombea mtu kifo" .......... maana kumuombea mtu kifo ni dhambi kubwa kuliko hata dhambi aliyeifanya huyo muhusika.

tuombe sheria ifuatwe na tuwe sababishao la sheria kufuatwa.
 
Mh,kama c mfuatiliaji, unaweza kumuonea huruma!!!!!!!!but no need of it

sure! jizi rafi namna hii lisilo kuwa na chembe ya huruma, linaiba kwenda kuficha nje? huruma ya nini?, hayo ni machozi ya watanzania wanao lalia mlo mmoja, na bado!
 
Kuomba msamaha si vibaya, unapotenda kosa na kwa uungwana ukatambua kuwa umetenda kosa basi kuomba msamaha ni jambo jema. Kikubwa kwa muheshimiwa hapa ni kuwajibika kwa msamaha alioomba, kuwajibika hapa kunamaanisha kuwa atubu kikamilifu kwa wale wote aliodhurlumu na kuondoa uhai wao.

Pia awaeleze watanzania ni kina nani aliokuwa anashirikiana nao katika kukwapua vijisenti na labda kama ataona inafaa atuambie kabla hatujamuuliza ni visenti vingapi anavyovimiliki ukiacha vile vilivyobambwa na SFO

nampongeza na akidhamilia basi wote watamwelewa na kama wote watakubali msamaha wake nina hakika Mungu atamsikia


Dhambi mbaya ni kukataa kutubu kwa kosa ulilotenda
 
Chenge had a hand in all the dubious deals that were concluded during Mkapa's ten year rule! IPTL, MEREMETA, DEEP GREEN. MWANANCHI GOLD, KIWIRA GCOAL MINE, etc. all these had Chenge's signature; hence to invoke God's mercy he needs to repent all his sins and emulate Zakayo's courageous decision of returning to the rightful owners all the loot that he stole!!

Ni rahisi Ngamia kupenya ktk tundu la sindano kuliko tajiri kuurithi uzima wa milele.
 
Ukichaa hautoshi, wafe kabisa tuwazike!! halah!!

Ya nini kuwaombea wafe?
Mimi nadhani ni vema wabaki tena na akili yao timamu ili watakapopata hiyo mitihani au majaribu ya kidunia basi waisome vizuri.
MWISHO WA UBAYA SI NI AIBU?
 
Ubeb'e chenge Ingwe, !

Mnafiki mkubwa wewe, unatafuta huruma ya wabunge wakati wewe ni mwizi mkubwa, kama unataka upate amani maishani mwako, katubu kwa kumaanisha, kisha urudishe pesa zote ulizoiba na zile zitokanazo na mtaji wa wizi, vinginevyo tutakufuata kila uendako mpaka pale utakapoingia kaburini. MWIZI MKUBWA WEE
 
Ya nini kuwaombea wafe?
Mimi nadhani ni vema wabaki tena na akili yao timamu ili watakapopata hiyo mitihani au majaribu ya kidunia basi waisome vizuri.
MWISHO WA UBAYA SI NI AIBU?

WoS,

Kibinadamu hutakiwi kumwombe amwenzio mabaya. Lakini kama ukiangalia nchi kama China, unadhani walikosea kutoa hukumu ya kifo kwa watu wa aina ya Chenge? Nadhani kama tunataka kukomesha wizi wa kipuuzi unaosababisha maisha ya watu kupotea bila sababu, adhabu ya kifo tena mbele ya wale walioteseka inaweza kusaidia. Kama wangekuwa wanasoma hiyo mitihani vizuri basi mafisadi na mapapa wasingekuwa wanapanga mipango ya kuwafanyizia raia wema. Kuna umuhimu wa kutomwangalia nyani usoni kama kweli tunataka kumaliza hili tatizo la ufisadi na upapa. Mbona vibaka wanapigwa viberiti au wao roho zao ni bei poa kuliko za mafisadi! Hii ni vita, wakituwahi wanatumaliza kama wanavyofanya sasa hivi. Je, tukiwawahi tuwape kikombe cha kahawa?
 
Back
Top Bottom