Angalia haya ya fisadi Chenge! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Angalia haya ya fisadi Chenge!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Apr 26, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,918
  Likes Received: 83,432
  Trophy Points: 280
  Chenge awatoa chozi wabunge

  2009-04-25 16:51:37
  Na Emmanuel Lengwa, Dodoma

  Mheshimiwa Andrew Chenge, mbunge wa CCM wa jimbo la Bariadi Magharibi, kidogo awatoe chozi waheshimiwa wenzake pale alipoamua kuweka wazi machungu aliyonayo moyoni kutokana na mikasa ambayo amekuwa akikumbana nayo.

  Amesema mikasa yote hiyo anayoipata ni mitihani ya kidunia ambayo ameamua kumwachia Mwenyeji Mungu ambaye ndiye mweza wa yote.

  Chenge hadi sasa anakabiliwa na kesi ya jinai ya kusababisha vifo vya wasichana wawili baada ya gari lake kuhusika na ajali iliyotokea hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.

  Licha ya hilo la ajali, pia aliwahi kupakaziwa uchawi ambapo alidaiwa kunyunyizia unga kwenye viti ndani ya Bunge.

  Kana kwamba hiyo haitoshi, mheshimiwa huyo pia anadaiwa kujilimbikizia mihela katika akaunti nje ya nchi, sakata lililomfanya apoteze nafasi ya uwaziri.

  Chenge, aliyekuwa Waziri wa Miundo Mbinu, alilazimika kuachia ngazi baada ya kukumbwa na kashfa hiyo.

  Chenge alipata nafasi hiyo ya kuwaeleza wabunge kilicho moyoni, wakati aliposimama Bungeni kutoa maoni ya Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi kuhusiana na muswada wa Bima ambapo kabla ya kuhitimisha, aliwashukuru wabunge na wananchi ambao walimtumia salam za kumpa pole.

  ``Nawashukuru wabunge na wananchi wote walionitumia salam za pole, ninachoweza kusema ni kwamba yote namwachia Mungu,`` akasema Mbunge.

  Mheshimiwa huyo akamalizia kwa kusema kuwa amelazimika kusema hayo kwa vile hiyo ni mara yake ya kwanza kusimama mbele ya Bunge hilo tukufu baada ya kukuktana na mitihani mbalimbali ya kidunia.

  SOURCE: Alasiri
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Bua ha ha ha...

  Na bado!
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Akatubu kanisani anakoabudu na arudishe zile pesa zije kusaidia maendeleo vijijini na Mungu atamsikia kilio chake hapo alipo. Ni mnafiki tu na Mungu hapendi unafiki maana ni dhambi....
   
 4. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  Hakuna cha zaidi na hawezi kuwa na amani kama hatakuwa mkweli
  biblia inasema "ukweli utawaweka huru" cha muhimi ni ku-confess hadharani madhambi yake yote kwa walalahoi, na kama kuna chetu basi akirudishe, hapo hata kama akienda kerezani amani itakuwapo ndani ya moto wake na mabalaa yatamwisha
   
 5. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Huwa najiuliza, kwanini usanii upoo church na sio msikitini? Nisaidieni
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Apr 26, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kweli unahitaji msaada. Mtafute daktari wa akili.
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mimi nadhani baada ya muda si mrefu mafisadi wote wataugua ukichaa kwa sababu hawana amani, sidhani kama hata wanalala usingizi mnono. Kwa mfano Manji, tulishaona ukichaa wake.
   
 8. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #8
  Apr 26, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Cha mtoto cha mtoto.
   
 9. M

  Magezi JF-Expert Member

  #9
  Apr 26, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145


  Ukichaa hautoshi, wafe kabisa tuwazike!! halah!!
   
 10. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #10
  Apr 26, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Siwezi kuelewa ni kitu gani kinaendelea. Hivi watu wote duniani tumwomba Mungu mmoja au kila mtu ana Mungu wake? Kama anajua kuwa kuna watu wengi sana wanaondelea kutaabika kwa kukosa huduma muhimu na wale waliokufa kwa ajili ya ufisadi wake, basi Chenge hana hata chembe ya haki kumtamka Mungu mbele ya kadamnasi! Pia kama anajua kuwa wale wanawake 2 waliokufa kwenye Bajaj walistahili kuishi kama anavyopumua yeye, pia sioni kama angekuwa na nguvu tena bila aibu kulitamka jina la Mungu! Asianze kutuletea usanii hapa. Makosa aliyowatendea Watanzania akiwa mtumishi wa serikali (AG) ni makubwa sana; sawa na kuwanajisi watoto wetu na hastahili huruma ya umma hata kidogo. Hata akiungama hiyo haitamsaidia. Labda arudishe pesa zetu na aende jela ili akifanikiwa kumaliza kifungo chake aje kutuomba msamaha. Vinginevyo aache usanii wa kutafuta huruma. Bado bado hajafanya lolote kuisafisha damu ya Watanzania mikononi mwake. He must pay for his evils!
   
 11. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #11
  Apr 26, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hapa watu naona wana mchezea Mungu na kumsingizia kwamba yeye ndo kawatwisha hayo!

  Yaani we Chenge, Mungu ndo alikufanya uibe pesa ukazifiche ngambo, udharau watu eti ni vijisenti, ufanye ufsika na kusababisha kifo tata cha wadada wawili, Mungu huyu huyu alikuamsha usiku akakupeleka ukawange bungeni? Jamani Mungu huyu Mungu huyu, labda unaye Mungu wako anaye kuaminisha utende hayo uliyo yatenda si Mungu wetu wote tunaye Mwamini the almighty
   
 12. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #12
  Apr 26, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu,

  Hivi hukusoma wajamaa wa njozi? Moja ya theories zao ilikuwa ni hiyo kwamba wananchi wawazomee mabepari na majizi kiasi kwamba wataona aibu na kuacha ujambazi wao. Pamoja na kuzomea kote, mabepari wakachuna tu, wakaendelee kunyonya.

  Dawa ya hawa mafisadi na majambazi wengine wote ni kuwapeleka mahakamani. Hata tuzomee vipi, hizo kelele haziwatishi na wataendelee kutuibia tu. Dawa pekee ni msumeno wa sheria kufanya kazi.
   
 13. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #13
  Apr 26, 2009
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  He was playing on his turf.

  How come he does tell "WAZALENDO" what happened if he is really sincere?

  If he is really sorry and ready to apologize, he should come out and tell all of us that he has mis-managed out tax money and he is going to give it back.

  He should stop playing with citizens.
   
 14. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #14
  Apr 26, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  ..inafaa atafakari zaidi kuhusu nafasi ya Mungu katika maisha yake, labda kama anawaza Mungu yupo kwa ajili yake tu, ninavyojua Mungu yupo fair, lakini Chenge doesn't want to be fair, so?
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  Apr 26, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,625
  Trophy Points: 280
  Siungi mkono ufisadi bali kama binadamu na Chenge ni binadamu, kwenye balaa la ajali namuhurumia kama binadamu mwingine yoyote anapopata matatizo ambayo hayahusiani na ufisadi wake.
   
 16. moza

  moza Member

  #16
  Apr 26, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh,kama c mfuatiliaji, unaweza kumuonea huruma!!!!!!!!but no need of it
   
 17. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #17
  Apr 26, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Chenge had a hand in all the dubious deals that were concluded during Mkapa's ten year rule! IPTL, MEREMETA, DEEP GREEN. MWANANCHI GOLD, KIWIRA GCOAL MINE, etc. all these had Chenge's signature; hence to invoke God's mercy he needs to repent all his sins and emulate Zakayo's courageous decision of returning to the rightful owners all the loot that he stole!!
   
 18. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #18
  Apr 26, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Mzee wa vijisenti bwana!!

  Kaazi kweli kweli!
   
 19. s

  skasuku Senior Member

  #19
  Apr 26, 2009
  Joined: Apr 19, 2008
  Messages: 113
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hapo sasa utaona jinsi gani wabunge wetu walivyo machicha... sasa ya Chenge mimi yanitoe machozi... kweli kabda niwe fisadi mwenzake, then nimoonee huruma.

  Ningependa kuona anapopolewa na viatu, mawe, ... wakati anasema huu ujinga. He deserves everything coming to him.

  Hakuna kuoneana haya sasa, kama anataka kutubu basi aiitishe press conference, aje na list yake ya madhambi (ufisadi wote aliefanya) na kunena anarudisha. You and I know hili halitaweza fanyika. Tuendelee kuungana na wakina Slaa na Mengi kuwapa hawa mafisadi wakati mgumu.....
   
 20. MwanaHabari

  MwanaHabari JF-Expert Member

  #20
  Apr 26, 2009
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kila mtu anamkimbilia mungu sikuhizi, mara lowassa, chenge..sitashangaa kusikia rostam kaokoka pia
   
Loading...