Binafsi ningeshukuru sana akatiwa moyo/msukumo, badala ya kupewa tahadhari ya uoga.
Kama kweli Emanuel Nchimbi anajisikia tofauti na kundi alilomo, namshauri asiogope; awe mkweli wa nafsi yake tu na aseme anachojisikia kusema.
Siyo lazima aseme kwa kushutumu; lakini akisema kwa namna nafsi yake inavyomtuma, waTanzania watamwelewa, na wataungana naye.
Katika hali ya sasa, hawa waovu hawana wigo mkubwa wa kufanya maovu tena kama walivyokuwa wakifanya huko nyuma.
Umesikia hivi karibuni mtu aliyetekwa, baada ya Oktoba?
Umemsikia lini mara ya mwisho Jumanne Mulilo akitishia kuua watu mitaani baada ya oktoba?
Emmanuel Nchimbi aseme anachojisikia kusema. WaTanzania watamsikiliza.
Vinginevyo, hatakuwa na tofauti yoyote na hao waovu anaowasaidia kubaki madarakani kwa mabavu.
Akiendelea kukaa kimya, au kutoa vimaneno rejareja visivyokuwa na maana yoyote, yeye atakuwa ni kiungo muhimu wa kuendeleza uovu.