Anga za mbali.

lopinavir

Senior Member
Jul 11, 2015
186
121
Kumekuwa na nchi tofauti hasa zenye uchumi mkubwa kwenda anga za mbali na nyingine kuwa na vituo huko angani kama ilivyo Marekani(NASA).
-Mara kwa Mara tumekuwa tukipewa taarifa za mafanikio tu,kama chombo cha nchi fulani kimefanikiwa kufika anga za mbali kama ilivyo Apolo na vinginevyo.

Ni changamoto zipi haswa wanakutana nazo huko angani?endapo chombo kitaharibika na ndani kina watu au endapo kiyagongana na miamba iliyopo huko angani na kuharibika kabisa?
-Na ikiwa kimepotea njia na pia kimepoteza mawasiliano nini hufanyika?
-Huko angani huwa kuna mipaka pia ya kila nchi zinazoenda huko?
-Ile Center ya NASA ni kila nchi inaruhusiwa kushusha chombo chake pale au ni lazima kila nchi inayopeleka chombo chake itengeneze sehemu ya kufikia chombo chake?
-Deep space ni nini?

Wajuzi wa haya mambo naomba mnielimishe...
 
Bila shaka ulipoandika NASA umekusudia ISS. Maswali yako ni mazuri, bila shaka wataalamu wa mambo haya watakujibu. Nikipata muda nitakupa dondoo kwa kile kidogo ninachojua.
 
Bila shaka ulipoandika NASA umekusudia ISS. Maswali yako ni mazuri, bila shaka wataalamu wa mambo haya watakujibu. Nikipata muda nitakupa dondoo kwa kile kidogo ninachojua.
NASA na ISISwanahuianaje?
 
Hahaaaa! Mkuu [HASHTAG]#SDG[/HASHTAG], siyo ISIS ni ISS. ISS=International Space Station....
 
Yeah,Nani alikijenga hiki kituo na ni nani haswa anaeruhusiwa kutua hapa kwenye hiyo station?
Ilikua ni project ya mataifa kadhaa kipindi ncho rais wa marekan mnyama ronald reagan alitoa wazo la kuwa na satellite huko angani bunge likakubali.
-Mataifa kadhaa kama japan, german, russia, marekan wenyewe n.k wakafanya hiyo proect.
-Mnamo 1998 walirusha vyombo vya hiyo satellite kwa rocket na mpango ukakamilika.
-Inaitwa iternational space station (ISS).
-Huko wachunguzu wapo huko na maisha yanaendelea kama kawa, Tafit mbali mbali zinafanyika.
 
Ahsante kwa maelezo mazuri....!!Ambao hawakuwepo kwenye huo mpango wakati ISS inaanzishwa kama China na India wao wakipeleka vyombo vyao huko wanawalipa hao walioanzisha au wanapeleka kwa utaratibu upi?

-Nisaidie pia kujua Deep space ni nini hasa?
 
Mkuu kutengeneza hizo satellite sio kitu kidogo, ni gharama sana.
-Ugumu upo kwenye kuweka hiyo satellite kwenye space, hapo lazima roket ihusike kupandisha hivyo vyombo na kuunga mitambo hiyo.

-Washirika walifanya hiyo project ndo wanahakimiliki ya satellite husika.

-Hiyo deep space ni anga za mbali. Baadhi ya vyombo vimetumwa huko kuchunguza na huleta majibu baada ya miaka kadhaa maana ni mbali mno.
 
Back
Top Bottom