Andy Cole na ubabe wa Ferguson

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
820
2,070
.
Leo kazaliwa Legend wa United Andy Cole, una ambiwa uhamisho wake kuja United kutoka Newcastle ulisababisha bifu zito kati ya Alex Ferguson na kocha wa Newcastle Kevin Keagan

Ni stori ndefu lakini inaburudisha

Mwaka 1995 Andy Cole akiwa katoka kuifungia Newcastle goli 43 msimu wa nyuma yake mara ghafla form yake
ikayumba, Keagan akajaribu kuwa nae karibu kujua shida ni nini lakini Cole hakuonesha ushirikiano wowote.

Kiungo wa Newcastle Lee Clark alikua ni jirani na rafiki wa karibu wa Cole, mara nyingi walikua wanapitiana muda kwenda mazoezini siku moja January, 1995 Clark alimpitia Cole nyumbani kwake ili waende mazoezini lakini Clark alipofika kwa Cole alibisha hodi bila mafanikio yoyote, alipopiga simu yake iliita bila kupokelewa, Clark akaamua kuondoka, wakati yuponjiani Cole akampigia simu akamwambia kuwa yupo jijini Manchester kuna ishu moja ya siri anaifanya.

Keagan akiwa viwanja vya mazoezi akapata taarifa kutoka kwa mashushu wake kwamba agent wa Cole na Cole mwenyewe wameonekana na Ferguson huko jijini Manchester.

Keagan baada ya kupata taarifa zile akaenda moja kwa moja kwa mkurugenzi wa timu akamuuliza Kama kuna ofa yoyote imekuja kwa ajili ya Cole akaambiwa hakuna, Keagan akasema basi ikija ipokelewa tu.

Uamuzi Keagan kumuuza Cole ulizua utata na mgongano Kati yake na bodi ya Newcastle, pia uamuzi huo ulizua jazba kwa mashabiki wa Newcastle, Clark ansema wachezji walipo sikia taarifa hizo morali ilishuka sana.

Keagan alichukizwa sana na kitendo cha Cole kutafuta timu nyingine bila kumpa taarifa na kikubwa zaidi Ali
chukizwa na njia Ferguson aliyo tumia kufanya mazungumzo na Cole.

Keagan aliwaza ni jinsi gani na yeye ata mkwaza Ferguson ndipo akagundua kwenye academy ya United kuna winga machachari wa miaka 19 aitwaye Keith Gillespie, kinda huyu Ferguson alimuhusudu kupita maelezo.

January 7, 1995 United walipeleka ofa rasmi ya £6m, baada ya ofa kufika Keagan akaiambia bodi wafanye
wafanyavo lakini ofa hiyo imjumuishe, Keith Gillespie.

Baadae Newcastle wakawapa majibu United kwamba wako tayari kumuuza Cole kwa £6m + Gillespie, baada ya Ferguson kusikia taarifa hizo alimjia juu Keagan kwamba anafanya ukorofi.

Baadae United wakapeleka ofa mpya ya £12m lakini keagan aliwaambia mabosi zake wakubali £12m au £1m
hiyo ni juu yao lakini yeye anachotaka Gillespie awepo kwenye dili.

January 9, 1995 Ferguson alimjumuisha Gillespie kwenye kiosi kilicho kua kinaenda kucheza ugenini kwenye kombe la ligi dhidi ya Sheffield United.

Gillespie ansema siku hiyo alikua na furaha Sana maana alikua anazani siku hiyo angecheza lakini dakika chache kabla ya mechi kuanza Ferguson alimuita, pembeni na kumueleza kila kitu kwamba anatikiwa kuwa sehemu ya dili la Cole.

Gillespie anasema kwenye mechi ile united, ilishinda 2-0 lakini hakumbuki chochote kilichotokea maana muda wote wa mechi, yeye alikua akiwaza hatma ya soka lake.

Baada ya mechi Ferguson alimchukua, Gillespie na kwenda nae Sheffield hotel ambapo Keagan na viongozi wa Newcastle walikuepo, Gillespie anasema kwa sababu hakua na agent basi Ferguson aliamua kusimama Kama
agent wake, licha ya kwamba Gillespie alikua analipwa £250 pale United lakini Ferguson aliwaambia kina Keagan kwamba Gillespie alikua analipwa £600 na Kama wanataka awepo kwenye dili la Cole basi wamlipe £1,200, Gillespie alifurahia Sana jinsi Ferguson alivyo pambana kwa niaba yake.

Baada ya makubaliano kufikiwa dili lika kamilika, Januray 10, 1995 Andy Cole na miaka yake 24 akatua United.
Baada ya Ferguson kuona mashabiki wa Newcastle wamemkalia kooni Keagan kwa kuuza silaha kwa adui basi wakati akimtambulisha Cole akasema "kiukweli mpaka sasa sielewi kwa nini Keagan kakubali kunipa mchezaji mzuri kama huyu "

Mwisho wa msimu United alimaliza wa Kwanza Newcastle wa pili.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom