Android vs iPhone/iOS

Mimi ntaweka msimamo wa ligi kuhusu vyombo hivi viwili ingawa mpaka sasa mimi mwenyewe nnatumua Android yaani nnamiliki HTC Desire.

Lakini 4S wamekuja na mambo mengi mno na ukiangalia table hii utaona tofauti.

Android
iPhone
Advantage
Battery: Unaweza kuiondoa au kuibadilisha kutokana na kuwepo nyingi tu madukani. Kwahio hakuna tatizo kwenye suala la battery.Huwezi kubadili battery. kwa kifupi huwezi pia kugundua kwamba simu hii ina battery. Chombo hiki kikiharibika itabidi upeleke kwenye workshop au kwa wale wa Ualaya na Marekani upeleke kwa Apple wenyewe na watakutoza gharama za kutengeneza na hasa kama huna guarantee.Android
Apps: Ingawa watu wengi hawatumii Android ina kama 70,000 applications kwa sasa.iPhone wanajidai na applications zisizopungua 230,000 na bado zinaongezeka.iPhone
Jailbreak: Yaani kufungwa na mtandao mmoja. Android OS unaweza kutumia kwa service provider mwingine nje ya Ulaya na US.iPhone hawana hii feature. Kwahio unapoondoka kwenda nje ya Ulaya na US basi uwe umefanya utafiti wa kutosha kwamba utatumia chombo chako nje ya maeneo hayo kwa raha.Android
Notifications: Inaitwa System wide notification (non-modal)na application notifications ( kama vile mail / new tweet / new SMS) ambazo unaweza kufungua chini na kusoma.Kwenye hii 4S inabidi ubonyeze kitufe au Icon ili kifunguke na pia ubonyeze tena ili usome.Android
Internal Memory: Memory yake ya ndani iko limited mno yaani ina kiwango. Haina tatizo kwenye kuhifadhi picha na muzic lakini sio more applications.Itabidi ununue memory kadi ili uongeze memory.Internal memory ni nzuri na inajitosheleza na pia una uwezo wa kuchagua wapi uhifadhi kitu kipi.iPhone
External Memory: External SD card zinaweza kuingizwa ili kuhifadhi photos, media. Lakini baadhi ya SD card zinakuwa rahisi kuwa corrupted na kusababisha kupoteza data / photo / au media.Hakuna external expandable memory. Internal memory ni kubwa na inajitosheleza.iPhone
Dictionary: Google wanasaidia kuweka maktaba kwa kutumia sauti na wanaorodhesha kila msamiati. Hii inasaidia kuelemisha mtumiaji na kujisikia anatumia chombo hiki kwa raha.Simu hii inakitu kinaitwa Artificial Intelligence type dictionary. iPhone inafuata unachoandika. Kwa hio kama unakosea ku-type unachoandika, iPhone itajifunza neno hilo lililokosewa na itafanya reset kusahau neno hilo. Kwa mfano uandike kwa makosa neno ‘habe’ badala ya "have" itafuta neno habe na kukusaidia neno have. Hii process inachukua muda mrefu kulinganisha na Android. Android
Mail App: Kuna Apps tofauti kwa Gmail peke yake na mail zingine. Hakuna otions nyingi kwenye kufanya editing kwenye emails.Kuna application moja tu ya email. iPhone
Aesthetics: Muundo wa simu hii kwa kutumia Google kwa kila kitu kunaifanya simu hii iwe kama vile ni ya 3D kumbe sio kabisa. Kila application – iwe ya bure au inauzwa inaonekana ni nzuri kwa mtizamo. Kwahio muonekano wa kwanza unaweza kuchangia asilimia 90 ya uamuzi wako wa kununua simu hii.iPhone
File Transfer / Sync: Android ina usb cable na unafanya transfer kwenda kwenye laptop au desktop bila shida.Inabidi utumie software ya iTunes sync model – kama vile iPods. Hii inamaanisha kuwa na separate sync folder kwenye laptop na ufanye kwanza transfer ya media content kwenda kwenye folder kabla ya kuanza sync.Android
Hardware Design / Buttons: Menu na Back button zinatofautiana kazi zake na hii inaboa sana.Simu hii ina button moja tu – clear function. Menu na back zote zinaelekezwa na button moja.iPhone
Text Editing: Text editing haijatulia kwani inazingatia ni applicatin gani unatumia.Text editing operations kama vile (cut,copy and paste) zinafanya kazi sawa bila kujali unatumia application gani. iPhone
Charger: Simu ina charger ndogo au Micro USB ambayo inauzwa madukani. Apple charger tu na sio aina zingine kwa hio inabidi ununue charger mbili kwa siku za baadae in-case unapoteza mojawapo.Android
OS Upgrade: Huwezi kufanyia upgrade Operating System.iPhone inasaidia kufanya OS Update. iPhone

Kwahio baada ya uchambuzi huu nnweza kusema kwamba iphone 4S ina alama 8 na Android ina alama 6.

Mwenye mawazo zaidi achangie.
 
Wakuu mnaonyesha ushirikiano mzuri sana (especially mnavyoikubali iPhone). Haya tuendelee.
 
Android ni Bomba sana, especial my Wildfire HTC ina option ya Hotspot yaani ina chuku 3G alafu inasambaza WiFi so unakuwa na wireless yako sAaafi bila shida, kwenye swala la software Android wako vyema sana.
 
Android ni Bomba sana, especial my Wildfire HTC ina option ya Hotspot yaani ina chuku 3G alafu inasambaza WiFi so unakuwa na wireless yako sAaafi bila shida, kwenye swala la software Android wako vyema sana.

mkuu hata IPhone ina MyWi ya kufanya internet tethering, unasambaza wireless connection kwa computer zingine, simu yoyote yenye uwezo na device yoyote inayopokea wireless conn'...bila kusahau kuwa una option tatu za kushare internet connection, either kwa Bluetooth, Cable au Wireless Fidelity yenyewe...

2hn9jxw.jpg
14xm7o4.jpg
 
mkuu hata IPhone ina MyWi ya kufanya internet tethering, unasambaza wireless connection kwa computer zingine, simu yoyote yenye uwezo na device yoyote inayopokea wireless conn'...bila kusahau kuwa una option tatu za kushare internet connection, either kwa Bluetooth, Cable au Wireless Fidelity yenyewe...

2hn9jxw.jpg
14xm7o4.jpg

Ahsante mkuu.
 
Back
Top Bottom