Mi sijaona Symbian alichomzidi Android.
mkuu symbian imekufa kwa mambo mawili
1. resolution ya screen haizidi 360p wakati os nyengine zishafika 720p na 1080p
2. haiwez tumia core zaidi ya moja kwenye processor na kufanya games za hd kuwa slow
apart ya hivo vitu viwili symbian inampita android kila eneo nikiwa kama power user wa os zote mbili ngoja nikutajie maeneo ambayo nayamiss hadi leo nilipoanza kutumia android.
access point
kwenye android na os nyengine unatumia access point moja tu wakati wa kubrowse internet, ina maana nikieka proxy za opera ina affect hadi nikitumia playstore. hii inamaanisha siwez tumia proxy kwa app 2 kwa wakati mmoja. symbian yeye anaruhusu access point zaidi ya moja ina maana setting hii ya internet naipoint opera, hii naipoint ucweb, hii naipoint ovi store. hii inakua rahisi na inakupa flexibility
http tuneling
mpaka leo hakuna http tuneling ya maana android, inamfanya hata paje asiweze tumia guru yake kwenye android wakati symbian zipo za kumwaga kama vile lothar's edge, cruxifire, jamieproxy na nyenginezo.
python application
kwenye symbian unainstall python kwenye simu halafu kuna app za python unazieka hizi apps zilikuwa very powerful mfano mzuri ni image designer hii ni clone ya adobe photoshop lakini ina kb600 tu, nimetafuta android market nzima sjapata image editor nzuri kama hii unaweza ona screenshot hapo chini
mfano mwengine ni bbcode editor, its shame android sjapata app ya kuedit bb code, hivi vitu vyote munavyofundishana watumiaji wa simu mimi kwa symbian nilikua nafanya automatic kutumia symbol paster kwenye symbian, zipo apps nyingi siwezi kuzitaja zote hapa.
wepesi wa os
japo symbian ni powerful ila ukitajiwa hardware zake utacheka n73 ina processor 300mhz na ram 64mb tu lakini inapiga mzigo, n8 inasifika sana na camera yake ila ina 600mhz na ram 256mb hii inaonesha jinsi os ilivyokuwa optimized. japo imekufa ila tutaikumbuka symbian belle9 ilivyokuwa smooth.
multitasking
symbian alikua king wa multitasking unaweza acha app open hata mwezi mzima ila ukija kuiangalia ipo vile vile, japo android anajitahidi lakini still hajafkia multitasking ya symbian. multitasking ya android ukifungua app nyingi kidogo tu basi zile za kwanza zinajistop. ukitaka kujua symbian ni noma angalia video hapo chini jamaa kafungua application 48 kwa mpigo na kitu kipo smoooth
Nokia 808 multitasking 48 apps - YouTube
file manager
file manager ya kwenye symbian ilikua ni ya kawaida kama android lakini 3rd party zake zilikua ni noma kwa kutumia file manager kama xplore ulikua unachange system files hadi os yenyewe wakati android kufanya hivyo hadi ueke custom rom(ina maana changes zinafanywa nje then ndo unaeka rom kwa symbian unafanya mule mule)
limitation
kwa os nyengine ios na wp inaonekana android ipo open ila ukiilinganisha na symbian android ipo closed sana na hizi ni sababu
1. symbian unainstall moja kwa moja apps kwenye memory card android mpaka uzimove nyengine zinakataa hadi uroot
2. android inakuja na apps pre installed kama google ecosystem nzima zinataka internet na acount oem kama samsung wanaeka zao so unakuta phone memory karibia 2gb inachukuliwa yote mambo haya hatuna symbian
mambo yapo mengi mengine hata hayaji kichwani kwa kuhitimisha tu symbian ndio hivo imekufa inabidi tuukubali ukweli na hakuna os nyengine ya simu inayofanana nayo kama android, lets hope jolla atatuletea kitu kizuri fans wa nokia