Andrew Chenge; Serikali isitishe kuajiri watumishi ili kupunguza matumizi

O

Onguluo

JF-Expert Member
406
225
Chenge ndiye m/kiti wa kamati ya bajeti Bungeni. Leo ametoa pendekezo kuwa serikali isitishe kuajiri watumishi ili kupunguza matumizi ya serikali. Kimsingi nimeona ni kupotosha umma na kuonesha dhihaka kwa watz, wao wenyewe ndo wamebeba pesa zetu kwenye viroba na kupeleka Uswiss, kibaya zaidi amezidi kuhamasisha serkal kutoza kodi ya laini ya simu kwa sababu kamati yake ilibuni mbinu hiyo ya kuongeza kipato.
Jamani hv jamaa ana nn mbona anadharau sana wananchi? Simpendi km kapuya.
 
Abdulhalim

Abdulhalim

JF-Expert Member
16,618
1,500
This guy is out of touch. Hata angekua anaenda kijijini au jimboni kwake angeona walau jinsi halmashauri yake ilivyo understaffed palepale wilayani, achilia mbali sekta nyingine kama walimu, wauguzi na madaktari, etc. Pia anasahau kua kila mwaka watu wanastaafu. Chama cha majanga kweli ni majanga. Hakuna dira yeyote za kiuchumi bali majanga tu/
 
T

tusichoke

JF-Expert Member
1,314
1,195
Aliyeshiba hamjali mwenye njaa,wao hata kodi hawalipi kwenye posho ambazo ni kubwa kuliko mshahara wa mwezi kima cha chini
 
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
49,453
2,000
Huyu jamaaa ni janga. Sijui kwa ni i hadi sasa hivi yupo serikalini. Anatakiwa aanze kujiuzulubyeye kwanza
 
mwa 4

mwa 4

JF-Expert Member
3,392
1,250
sijui kwa nini watu hupenda kupotosha ukweli nimemsikiliza chenge hajasema hivyo rejea hansard za bunge mkuu.
 
Chibolo

Chibolo

JF-Expert Member
3,969
2,000
kweli ccm ni chama chakavu jamani serikali itakosaje kuajiri wkt kuna wastaafu,wanaokufa,wanaocha.n.k
 
Ng'wanangwa

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
10,823
2,000
watu wanalia ajira, afu mtu anashauri serikali isiajiri!

kweli ccm inatakiwa itoweke kwenye ramani za utawala wa nchi hii na mapema.
 
meningitis

meningitis

JF-Expert Member
8,119
2,000
mwanakharashi na muuaji mkubwa huyu
 
T

This_2013

Member
23
20
Huyu mh anafikiria nini hadi kusema kuwa serikali isitishe kuajiri watumishi!
Napata wasiwasi mkubwa na utendaji wa hawa watu kwani inaonyesha hawaijui hali halisi ya watz hasa maeneo ya vijijini.Kijana anasoma kwa taabu ili angalau apate ajira tena hata ikiwa mshahara ni kidogo mithili ya posho zao ili aisaidie familia yake!Leo unasema watu wasiajiriwe!!!!!
Pia watu wanakufa,wanastaafu sasa hizi changamoto unaziepuka namna gani?MABADILIKO YANATAKIWA!!!!!
 
mwa 4

mwa 4

JF-Expert Member
3,392
1,250
Alichosema zipo ajira ambazo haziko kwenye utaratibu mzuri ambazo pia husababisha kuwepo kwa malipo hewa ni vema ajira za namna hii zikomeshwe kama siyo kusitishwa kabisa mada yako inapotosha.
 
C

CHIGANGA

JF-Expert Member
610
0
Umepotosha ukweli,alitolewa ufafanuzi kwamba,kama matumizi yanaongezeka sababu ya kuajiri,basi serikali iainishe maeneo ya kipaumbele katika kuajiri,au namna nyingine ili kupunguza matumizi,sii sahihi kunukuu kipande cha taarifa na kukijengea hoja.
 
mwa 4

mwa 4

JF-Expert Member
3,392
1,250
watu wanalia ajira, afu mtu anashauri serikali isiajiri!

kweli ccm inatakiwa itoweke kwenye ramani za utawala wa nchi hii na mapema.
we muongo umedandia pasipo kujua undani wa kile alichomaanisha chenge.
 
I

ilisha juniour

JF-Expert Member
689
225
Chenge ndiye m/kiti wa kamati ya bajeti Bungeni. Leo ametoa pendekezo kuwa serikali isitishe kuajiri watumishi ili kupunguza matumizi ya serikali. Kimsingi nimeona ni kupotosha umma na kuonesha dhihaka kwa watz, wao wenyewe ndo wamebeba pesa zetu kwenye viroba na kupeleka Uswiss, kibaya zaidi amezidi kuhamasisha serkal kutoza kodi ya laini ya simu kwa sababu kamati yake ilibuni mbinu hiyo ya kuongeza kipato.
Jamani hv jamaa ana nn mbona anadharau sana wananchi? Simpendi km kapuya.
aliyeshiba hamjui mwenye njaa;->
 
P

Percival

JF-Expert Member
2,655
2,000
Utakula ulicho nacho. Serikali ikikikaa kuajiri watu wasiozalisha si itapidi uwatoze kodi wengine ili kuwalipa mshahara !! . Ajira haitokani na serikali pekee bali sekta kama kilimo, biashara ndogo ndogo, makampuni, miradi ya serikali inayo jiendesha kifedha n.k
 
The Boss

The Boss

JF-Expert Member
38,951
2,000
Huyu anastahili kunyongwa hadharani....
 
Matango

Matango

JF-Expert Member
515
195
KUMBUKA KUNA SEHEMU ALISEMA NI MAWAZO YAKE. KISHA TAZAMA HII " MAJOGOO YA SHAMBA BAADA KUPIGANA SANA NA KUCHOKA YANATAZAMANA, TUSIWE KAMA MAJOGOO", Chenge. (mwisho wa kunukuu.
kweli ccm ni chama chakavu jamani serikali itakosaje kuajiri wkt kuna wastaafu,wanaokufa,wanaocha.n.k
 
Young Tanzanian

Young Tanzanian

JF-Expert Member
1,737
0
sijui kwa nini watu hupenda kupotosha ukweli nimemsikiliza chenge hajasema hivyo rejea hansard za bunge mkuu.
Ufpa kwa kubadili maneno si unawajua tena uktaja matumizi ya ruzuku mwkt anavyonunulia majumba ya kfahari wanakmbia
 
LESIRIAMU

LESIRIAMU

JF-Expert Member
5,365
2,000
Chenge ndiye m/kiti wa kamati ya bajeti Bungeni. Leo ametoa pendekezo kuwa serikali isitishe kuajiri watumishi ili kupunguza matumizi ya serikali. Kimsingi nimeona ni kupotosha umma na kuonesha dhihaka kwa watz, wao wenyewe ndo wamebeba pesa zetu kwenye viroba na kupeleka Uswiss, kibaya zaidi amezidi kuhamasisha serkal kutoza kodi ya laini ya simu kwa sababu kamati yake ilibuni mbinu hiyo ya kuongeza kipato.
Jamani hv jamaa ana nn mbona anadharau sana wananchi? Simpendi km kapuya.
Lakini ni sahih yeye kulipwa 420,000 kwa siku kama allowance hao ndo wawakilishi wa Ccm bungeni
 
mukandarasi

mukandarasi

JF-Expert Member
925
250
Kwa akili za kawaida huwezi kumpa cheo/wadhifa mtu mwenye tuhuma lukuki ndani jamii! Lakini kwasababu wenzetu ndani ya chama wanaamini UMOJA WAO NDIYO USHINDI WAO,bila kujali huyu ni GAMBA au FISADI!Ndiyo maana "mwenzao"(siyo sisi kina kabwela) anaweza tamka lolote tena kwa kejeli hasa.Lakini itapita kama hajasikika.Sisi tutakuwa na matarajio,matumaini na mategemeo ya ajira kustawishwa zaidi kwa vijana,Kama tulivyo somewa ILANI YA CHAMA kumbe kwa mujibu wa mkuu huyo mawazo yetu si sahihi.Sasa ndugu zangu ifike wakati tujitambue kuwa sisi wapiga kura ndiyo tuna matatizo kwa kupeleka watu kadhaa kama Mkuu huyo ndani ya Mjengo!
 
O

Onguluo

JF-Expert Member
406
225
Umepotosha ukweli,alitolewa ufafanuzi kwamba,kama matumizi yanaongezeka sababu ya kuajiri,basi serikali iainishe maeneo ya kipaumbele katika kuajiri,au namna nyingine ili kupunguza matumizi,sii sahihi kunukuu kipande cha taarifa na kukijengea hoja.
Umemsikia vizuri tatizo hujaelewa alichomaanisha. Hv mpaka leo hujui vipaumbele vya ajira serikalini au vipaumbele gani unataka? Kama hujui sema uambiwe ucjifanye unajua kila kitu!
Je,kodi ya laini ya simu unasemaje? CCm imechakaa hadi kwenye Injini.
 
Forum statistics

Threads
1,424,523

Messages
35,065,902

Members
538,009
Top Bottom