Andengenye na Mahita nani kamfundisha mwenzie? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Andengenye na Mahita nani kamfundisha mwenzie?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kweleakwelea, Dec 25, 2010.

 1. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #1
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,419
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Ninamfahamu kwa karibu kamanda Andengenye RPC wa Arusha. huyu alimaliza masomo pale ya sheria miaka ya kati ya ninety UD na akabahatika kuwa mpambe wa IGP Mahita. IGP Mahita amejulikana kati ya ma IGP waliohusishwa na ukatili mwingi ikiwemo mauaji ya General Imran Kombe na mamia ya wapemba ambao waliozamishwa baharini wakidai haki zao za msingi na wengine kufanywa wakimbizi shimoni kule mombasa. IGP mahita katika kustaafu kukajikuta kunamzawadia Andengenye u RPC wa morogoro, mkoa ambao ni nyumbani kwake bwana mahita. leo hii baada ya Matei kukataa kuwa katili kwa gharama yeyote sisiemu ikaona ni vyema impeleke Andengenye Arusha ili kuisaidia sisiemu kuchakachua na kuweka meya kiharamu.

  wote ni mashahidi wa utendaji wa kamanda andengenye tangia hapo, kiasi kufikia kutaka kumuua mbunge wa Arusha Mh Godbless Lema. Wananchi na wasomi wengi hata sisi ambao tuna vyeo na elimu kuliko hiko ulicho nacho hatujafurahia kitendo hiko hata kidogo. hii inatufanya tufikirie mara mbili kuwa ulikuwa ni master mind behind mauaji ya wapemba kwani bosi wako ambaye kidogo darasa lilimpiga chenga alikuwa anakusikiliza kwa kila kitu. hii inatufanya tuamini kuwa kwenye list ambayo itaenda The HAGUE wewe utaanza, mahita atafuata. wanajf imekaa vipi hii?
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Dec 25, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180

  Ujumbe wako kidogo umetofautiana na Headings, anyway ulichopost kinaeleweka vizuri.

  Ndg yangu hawa jamaa ukiwasoma vizuri, hakuna aliyemfundisha mwenzake, bali inavyoonekana ni watu waliopewa course ya udikteta kama si unyanyaswaji wa wapenda maendeleo, katika chuo kinachomilikiwa na CCM. Mfano wa chuo walichopitia hakina tofauti na vijana waliokuwa wanajulikana kwa jina la Green Guard.

  Mahita anasifa nyingi kumpita Andengenye, kwa mfano suala la Mauaji ya Kombe, Kushiriki kwenye uhalifu ( Indirect Crimes ), ni baadhi tu ya sifa alizonazo. Alikwisha wahi kutajwa na wananchi kwa kuhusishwa na ujambazi akiwa sambamba na aliyekuwa RPC wa Kilimanjaro Mohamed Chiku.

  Andengenye sijamsoma kwenye hizo sifa moja kwa moja, japokuwa ana qualifications za kuchakachua matokeo ( Arusha na Kilombero ), bado tunayo kazi kubwa ya kumstudy.
   
 3. 1

  1954 JF-Expert Member

  #3
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 4,282
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Wewe humfahamu Andengenye. Andengenye alisomea sheria pale mlimani. Wewe ni mwongo. Hakusomea sheria pale mlimani.
   
 4. Jituoriginal

  Jituoriginal JF-Expert Member

  #4
  Dec 25, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Moro,majambazi walikuwa washikaji zake tokea enzi za rpc ngowi ,huku andengenye,akiwa rco .
   
 5. h

  housta Senior Member

  #5
  Dec 25, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  What exactly are you saying??!!
   
 6. m

  mams JF-Expert Member

  #6
  Dec 25, 2010
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Data nilizonazo aliishia form IV na alikuwa muongeaji mzuri wa ngeli na alichukuliwa kuwa mpambe wa Mahita ili amsaidie kukarimani hiyo lugha ya wenzetu. Sasa amefikiaje kuwa na LLB sijui maana siku hizi kuna open University na hizo d'gree za heshima na msishangae akaaitwa Dr. Andengenye
   
 7. k

  kajembe JF-Expert Member

  #7
  Dec 26, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 755
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Data nilizonazo aliishia form IV na alikuwa muongeaji mzuri wa ngeli na alichukuliwa kuwa mpambe wa Mahita ili amsaidie kukarimani hiyo lugha ya wenzetu. Sasa amefikiaje kuwa na LLB sijui maana siku hizi kuna open University na hizo d'gree za heshima na msishangae akaaitwa Dr. Andengenye

  Open University nayo usanii au unamaana gani? sijakuelewa Mkuu ulivyoandika,
   
 8. D

  DENYO JF-Expert Member

  #8
  Dec 26, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  andengenye kamanda wa polisi anayetafuta ukubwa kwa kumpiga lema marungu -mungu amlaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaani
  Asante Yahya Mhoza kwa mada hii nzuri baada ya ile ya katiba wiki iliyopita tuliyoimaliza kwa mtu aitwae Mjuni George wakati sauti ni ile yam zee msekwa.
  Kwanini polisi wanalazimika kutumia nguvu zaidi?
  1. Mimi ni polisi niliacha kazi hiyo kwa sababu katika jeshi hilo kuna viongozi wake wengi wanaamini askari hawana akili na hawawezi kufikiri, lipo kundi kubwa la askari kinyume na sheria na kanuni za jeshi hilo linatumikishwa ndivyo sivyo kwa maslahi binafsi. Wanasema afande ndio mwenye akili na kwamba akisema twanga risasi wanategemea watwange.
  2. Kuna matumizi mabaya ya madaraka ya watawala kutea makamanda wa polisi kwa rekodi ya kupiga mabomu wapinzani na siyo sifa ya utendaji. Kama inavyosemekana mahita alipewa kuwa IGP kwa kuwa alimpiga mabomu mh.mrema sasa andenyenge alikuwa mlinzi wa mahita anamategemeo makubwa kwa kumpiga Lema marungu atapewa cheo zaidi –mimi nadahani amepitwa na wakati.
  3. Tunaelewa na tumefundishwa kwamba polisi anaweza kutumia nguvu pale tu mtuhumiwa anahatarisha maisha yake, au anagoma kutii amri halali mfano jambazi lina silaha itamlazimu polisi kutumia silaha kulidhibiti pamoja na kwamba haruhusiwi kuua. Sasa haingii akilini polisi anamvamia mbunge na virungu ndani ya ukumbi wa madiwani kisa OCD kamuru ili kumfurahisha RPC na Mkurugenzi ambao kwa vyovyote vile wanataka kuwafurahisha wabwana wakubwa na chama tawala.
  4. Jeshi la polisi kwa ujumla imepoteza dira imekuwa kitengo ndani ya ccm na inafanya kazi kwa maslahi ya chama-mfano unawapiga wananchi wanaodai Matokeo kutoka kwa mkurugenzi aliyegoma kutangaza kisa anaogopa wakubwa hawatafurahi, hivi hapa anaevunja sheria ni nani? Mwananchi anaedai haki yake au mkurugenzi anayepora haki???
  5. IGP Mwema amejitahi di kuleta chachu mpya lakini ili aweze kufanikiwa lazima asiwe achidodo asiwe ndumila kuwili asiwe kibaraka, asiwe tawi la ccm, polisi ya sasa inatumia nguvu sana kwa sababu haifuati kanini zake na sheria badala yake inafanya kazi kwa maslahi ya chama tawala, jeshi la polisi lifukuze makamanda kama andenyenge wapo wengi wanaosaka ukubwa juu ya migongo ya watanzania kwa kuwapiga mabomu. Kumpiga mbunge ni sawa na kuwapiga waliomchagua. Mwema awaruhusu polisi hawa waliogeuka watumwa na wajinga –kuwa na fikra na siyo kufanya kila kitu wanachoambiwa na mkubwa wao bila hivyo jeshi la polisi litaendelea kuwa adui wa watanzania. Polisi wanashida sawa na watanzania wengine hawana makazi, hawana Elimu nzuri, hawapati maslahi stahili, kwahiyo ni sehemu ya jamii.
  6. Kitendo cha kumpiga Mbunge Lema kilinifanya nijisikie uchungu kiasi kwamba niliona kumeza bomu na kujilipua wanavyofanya wairaq ni kitu rahisi saana sehemu yenye chuki na maudhi kama hii ya kumpiga virungu mbunge kisa kadai haki, lakini pia sijawai sikia mbunge hata mmoja wa ccm amepigwa marungu hata pale alipovunja sheria mfano Yule mgombea wa maswa aliyempiga mtama OCD je angekuwa LEMA? INGEKUWAJE? SHAME ON RPC , OCD AND DED FOR ARUSHA, SHAME ON POLICE FORCE, SHAME ON ALL THESE INJUSTICE.
   
Loading...