TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,742
Ni watu wawili tu ndiyo wanaowatesa CHADEMA, ni NGEDERE na rais Dr. Magufuli.
NGEDERE alichokuwa anataka ni kusafishwa na aliyemmwagia matope, amefaulu lakini CHADEMA hawatakaa wawe wasafi tena.
Rais Dr. John Pombe Magufuli amekonga nyoyo za Watanzania. hakuna anayehangaika na kusikia CHADEMA wanafanya nini kwa sababu wanafuga NGEDERE aliyekula mahindi yao kwa kipindi chake chote alipokuwa mashambani mwao.
Vipi sasa Chadema wanavyotapatapa kujinasua kutoka kule walikotumbukia?
Ni kwa kuwaaminisha Watanzania mambo mawili:
Kila kukicha utasikia mara "mawaziri wa Magufuli Majipu", mara "MAWAZIRI WA MAGUFULI WANAOSUBIRI KUTUMBULIWA" Ukiangalia kwa undani utagundua mawaziri wanaotajwa ni wale waliosimama kidete kuhakikisha NGEDERE anaondoka Shambani, waliosimma kidete kuhakikisha watu hawawi madalali wa vitalu vya gesi, waliopigania chama kuhakikisha kinapata mgombea safi na kuhakikisha CCM inashinga katika uchaguzi mkuu uliomalizika mwaka jana n.k.
Chadema kama Chama kinatakiwa kifanye kazi zake kama taasisi na siyo kuongozwa na NGEDERE kupambana na mtu mmoja mmoja ambao kwa namna moja au nyingine anaonekana kuwa na uhasama naye NGEDERE au mtu yeyote atakayewapa pesa.

- Kwamba NGEDERE hakulihujuhumu taifa hili(siyo fisadi). Hilo wamelitekeleza kuanzia wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka jana pale walipomtuma mtu aliyemwandika NGEDERE zaidi ya mara 70 kwenye gazeti lake kuwa "HUYU NGEDERE NI HATARI" kwenda Kyela kumwangusha Mwakyembe kwenye Uchaguzi wa Ubunge katika jimbo hilo. Ikumbukwe kwamba Mwakyembe ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati iliyomng'oa NGEDERE. Namna nyingine ya kumsafisha Ngedere ni kukosoa Operesheni tumbua majipu, eti utumbuaji unawaonea wanaotumbuliwa. Hii yote ni kutaka kutuaminisha kwamba inawezekana na NGEDERE alionewa. wao walikurupuka kumvua nguo bila kujiridhsha? NI VIGUMU SANA MTU YEYOTE ANAYEKULA SAHANI MOJA NA NGEDERE KUPONGEZA UTUMBUAJI MAJIPU, LABDA ARUDI YESU LEO. Hili la kumsafisha NGEDERE linafanyika katika nyumba za ibada, kwenye Majukwaa ya kisiasa n.k. ni hatari sana.
- Kwmaba serikali ya Magufuli nayo siyo safi