Anayesimamia Idara ya Habari CHADEMA anakihujumu chama

Kama hilo tu limewashinda,kuongoza watu na ile Idara ya Msigwa ndo wataiweza?

Hiyo idara ya mawasiliano ifumuliwe iundwe na watu wenye uwezo huo...

Hivi Kama taarifa tu Wana boronga hivyo, je kukusanya taarifa za matokeo ya uchaguzi wataweza?
Je wanaweza kufanya propaganda kipindi Hiki Cha kampeni?...
 
Hii ni makala ya hasira, nina hasira kiasi kwamba nitabandika makala tatu tofauti leo.

Watu wengi wameshalalamika ni kwanini CHADEMA wanashindwa kurusha matangazo yao Live, sitaliongelea hilo.

Leo mi naongelea kitu kingine. Naongelea jinsi mnavyowakilisha habari zenu kama ilivyoandikwa hapo chini:

Mnaweka video za sekunde chache YouTube, YouTube siyo TikTok, Facebook au Instagram. Wanaoenda YouTube wako tayari kuangalia video za zaidi ya dakika 20. Hizo za sekunde chache ni za kuweka Facebook ili ziwasukume watu kwenu. Facebook inajua nani anataka kuangalia nini na ujumbe utasambaa sana.

Mpaka sasa hamtangazi kwa watu ni jinsi gani watapata habari. Niliandika kwamba CCM wameshaamua kutoa mtandao kafara. Kwenye Vita ya Uchaguzi CCM wameshachagua nini wanatoa kafara.

Mko kwenye vita ya habari na CCM wameshawashinda. Sasa badala ya kutumia majukwaa yenu ya kampeni na kuwaelemisha watu watapataje habari zenu mko kimya.

Watanzania wanaogopa kutuma message WhatsApp. Mnamdanganya Lissu kwamba whatsApp inatosha. Lissu amesema kuwa watu wanaoenda kwenye mikutano ni kupitia kuambiana kwenye whatsApp. Hivi mna akili timamu kweli? Mnajua ni watu wangapi wako Tanzania? Kama mnategemea WhatsApp mnawaacha watu wengi pembeni. Pia kuna vyanzo vingine vingi vya habari mnavisahau.

Hamjitayarishi kurusha matangazo Live: Mara yakirushwa yanakatwa, mara video zinaganda. Inatia aibu kiasi kwamba kwenye mkutano wenu wa Arusha aliyerusha matangazo yenu live alikuwa mtazamaji na simu yake ya mkononi ambayo alikuwa ameiweka potrait mode (amesimamisha) badala ya landscape mode(iliyotengenzezwa ili video ijae kwenye screen)

Mnakata mahali muhimu kwenye matangazo kama TBC. Hata ikiwa live, nashangaa inakata kwa style ileile ya TBC, Lissu akianza kutoa cheche inakata. Inabidi mtu u search upya na unakutana na link nyingine.

Hawatengenezi media contents: Embu angalieni nini ACT wanafanya, jinsi wanavyotengeneza material for media kampeni. Jinsi walivyoiwakilisha ilani yao, jinsi wanavyotoa matangazo madogo marahisi kuyaelewa ambayo unaweza sambaza kwenye whatsapp na yana ujumbe wote. Hivi vitu ni bei rahisi kuna wahindi wanapatikana online watakutengezea kwa dolla sita (12,000Tsh).

Mimi sidhani anayeongoza kitengo cha habari hajui kazi yake. Anatumia ujanja kwamba viongozi wa CHADEMA siyo wanahabari na hata kama ni wanahabari hawako exposed na effective way of communication. Naogopa kusema hili lakini naanza kuamini huyo mtu ana kazi maalumu ya kitengo. CCM vita yake kuu ni kunyima ujumbe usifike. Kwa sababu anayependa kusifiwa hapendi kudhalilishwa.

Anayeongoza kutoa habari CHADEMA apewe onyo na asipojirekebisha akae pembeni.

Akhsante.

Niongezee: Hamko consistency na wapi tupate habari. Mara leo BAVICHA Facebook page, kesho CHADEMA TV, keshokutwa Jamvi Online aghhhhhh

Update:
Makala ya pili ya hasira zangu hii hapa;
Chadema, Mlituahidi Kampeni Nyumba kwa Nyumba lakini mnaruka wilaya na vijiji kwenye misafara yenu
Ngoja nikale kabla sijanuniwa na mimi nikirudi nitaandika ya tatu!!

Kitengo cha habari kinahitaji kuhusisha vijana aggressive haswa wenye weledi wa kutosha kwenye IT.

Kampeni nyumba kwa nyumba si za kubeza.
 
Kitengo cha habari kinahitaji kuhusisha vijana aggressive haswa wenye weledi wa kutosha kwenye IT.

Kampeni nyumba kwa nyumba si za kubeza.

Hiyo nyumba kwa nyumba inafaa kwa baadhi ya maeneo lkn kwa chuki iliyopo inaweza kuleta fujo pale mpiga kampeni anapofika eneo la wapinzani...
 
Niongezee: Hamko consistency na wapi tupate habari. Mara leo BAVICHA Facebook page, kesho CHADEMA TV, keshokutwa Jamvi Online aghhhhhh
Chadema kwenye media walishajivuruga pale walipowafukuza hadharani TBC
Watu wa media Wana nongwa sana,hata Kama hawaoneshi hasira hadharani lakini kwenye news room wanawaongelea,leo TBC kesho ni sisi
Tumieni tu hizo twitter zenu kwenda ikulu
 
Ya kufukuzwa TBC imewapunguzia chadema sehemu ya kutoa taarifa. Ukweli unabaki TBC walichakachua mno taarifa za chadema na hawawatendei haki. Hivyo sidhani kama TBC wanastahili huruma.

Sent from my SM-G935W8 using JamiiForums mobile app
 
Hiyo nyumba kwa nyumba inafaa kwa baadhi ya maeneo lkn kwa chuki iliyopo inaweza kuleta fujo pale mpiga kampeni anapofika eneo la wapinzani...

Nyumba kwa nyumba ni kuhamasisha watu wa kunakoitwa grassroots kusambaza upendo ndani ya maeneo yao.

Mimi mtaani kwetu na wewe kwenu. Ndani ya watu tunaowajua. Tusibweteke watu wakapige kura.

Kuna watu wengi wenye haki ya kupiga kura huwa hawaendi kupiga kura.
 
Ya kufukuzwa TBC imewapunguzia chadema sehemu ya kutoa taarifa. Ukweli unabaki TBC walichakachua mno taarifa za chadema na hawawatendei haki. Hivyo sidhani kama TBC wanastahili huruma.

Sent from my SM-G935W8 using JamiiForums mobile app

TBC hawakuwa na nia ya kutangaza habari za CDM. Hao ni sawa na kutegemea lb7 aseme jema lolote la CDM.
 
Chadema mbona inavijana wengi wasomi wa IT +Wenye taaluma ya habari kwa nini wasiwatumie?
 
Tumaini makene Ni CCM yule ashakula pesa za CCM

Athibitiwe hata Kama hawana uwezo wanipe Mimi kazi nitawaweka live YouTube, Instagram, Facebook na Twitter

Muda wote wa kampeni mpaka wanamaliza.

Huu unaofanyika Sasa Ni utoto toka asubuhi saa 11 ndio watu wanaleta picha huu Ni zaidi ya utoto.
ukata
 
Shida kubwa ni kuwa ccm imewashambulia kwa kiwango kikubwa hata kufikia hatua ya baadhi yao kuwa ktk hatari ya kukosa mkate wao wa kila siku. Hivyo chama kimesambaratika wamebaki wachache wasioweza ku cover kila eneo. Mbaya zaidi media zote zimebanwa haswa ambazo zingesaidia.

Imefikia wakati kila mmoja wetu anaficha utambulisho au mapenzi yake kwa upinzani ili kupata angalau riziki ila box la kura litaamua kudadek. mwaka huu nilikuwa nisipige kura ila nitapiga wacha waibe ila kura tangu itaniwakilisha katika roho kuwa nilikataa udhalimu na kuchagua haki. Amen.
Ameen
 
Tumaini makene Ni CCM yule ashakula pesa za CCM

Athibitiwe hata Kama hawana uwezo wanipe Mimi kazi nitawaweka live YouTube, Instagram, Facebook na Twitter

Muda wote wa kampeni mpaka wanamaliza.

Huu unaofanyika Sasa Ni utoto toka asubuhi saa 11 ndio watu wanaleta picha huu Ni zaidi ya utoto.
Hawa jamaa nimewashangaa sana. Hiyo idara ya habari ba maelezo wana uwezo mdogo sana kwenye hicho kitengo. Au wana lao moyoni.
 
Ht hizo live stream zikiwepo bado naona mapungufu ktk kampeni zao...

Khs maendeleo ya miundo mbinu wakosoe kwa hoja wao watafanya nn... sio kulalamika tu kwa Mambo yaliyopita..
Kampeni ziko Murua. Lazima uwambie wananchi kwanini wewe unakuja.....so lazima uoneshe uongo na udhalimu wa CCM.

Wananchi wamedanganywa sana kwa miaka 5. Lissu anachofanya ndio sahihi kabisa. Kuufuta uongo uliokuwa umeenezwa na CCM.
 
Back
Top Bottom