Anayependa kuwa mshirika wetu katika biashara kwenye kampuni

Anayependa kuwa mshirika wetu katika biashara kwenye kampuni

samida

Member
Joined
Jan 6, 2011
Posts
35
Reaction score
0
Naandika post hii kutoa fursa kwa Mtu binafsi yeyote ambaye anapenda kuwa mshirika wetu katika biashara (business partner) katika kampuni yetu. Tunahitaji angalau mtu mmoja kila mkoa isipokuwa mikoa ya Dodoma, Arusha na tayari tumeishapata business partners huko.

Yeyote ambaye anaweza kuwekeza angalau kiwango cha chini shilingi milioni kumi (10,000,000/=) naomba anitumie private message ili nimtumie deatails za kampuni ikiwa ni pamoja na compasation plan, web link ili aone biashara yetu na mfumo wetu ili kama ataridhia tuanze biashara mapema sana wiki hili. Nashauri unitumie namba zako za simu ili nikupigie tuongee kwa maelekezo zaidi. Itakuwa vizuri ukieleza mahali au mkoa ulipo.
Asanteni.
 
yale yalee
Weka humu then iwe public if is a serious deal.Ili watu waichallenge.
Kumuita mtu in privacy ni sawa na kumbania hukohuko bila kupata msaada wa experts wahumu.
Weka wazi ili watu wa challenge.
Maana nashangaa Pesa milioni kumi umetaja mbimbio hayo mengine private duhh
I smell.......
 
Mkuu kwa stail hii ya Uandishi hakika huwezi pata mtu, Mkuu kutafuta busness partnersni ishu moja ngumu kabisa, ni sawa na kutafuta mke wa kuoa, Mtu kutoa 10 milioni si ishundogo hata kidogo anatakiwa kujiridhisha 100% kuwepo na sapoting docoments.

Sio ishu tu ya kuandika ni lazima ushushe detailz za kampuni,
- Ni nani mmiliki wa kampuni kwa sasa? hapa ni pamoja na CV zao
- Kampuni imesajiriwa? Kama ni ndio it means lazima muandae docoment ya kuongeza share holder
- Biashara mnayo fanya au mnayo taka kuifanya,
- Market Research ya hiyo biashara na Market research iwe imefanywa na kampuni yenye watalaamu katika maswala ya utafiti,
-Ishu za mtaji
-Faida
-Risk

SO MKUU KUTAFUTA PARTNERS SI ISHU NDOGO, MAKE NI HATARI SANA KWAKO NA KWA UNAYE MTAFUTA, KWA SABABU UNWEZA PATA MTU ASIE MWEMA AU WEWE USIWE MWEMA,

That is why partners wanatakiwa muwe mnajuana muda mrefu, na mnajuana hadi tabia,na kila kitu


NA MWISHO HAYA MAMBO SIO SIRI KWA SABABU UKITEMBELEA WEBSITE ZA TAASISI KIBAO HAYA MAMBO YAKO OPEN KABISA, Ingia Bid Network utakuta watu wanatafuta partners au capital kwa uwazi kabisa
 
Nikweli mkuu hapo umemaliza kabisa
Kwa ufupi 10 millions hakuna mtanzania anaeweza ku risk namna hiyo maana we angalia hapa kuna mtu anataka ku invest kwenye laki tatu tu hapa anapata ushauri na kufanikiwa kuingiza kiasi hicho ndani ya muda mfupi.
Sasa iweje hiyo milioni kumi.
 
Back
Top Bottom