Anayemsifu MWAKYEMBE Atakuwa hamnazo!

Anayemsifu MWAKYEMBE Atakuwa hamnazo!

Status
Not open for further replies.
hapa mimi naona CCM inaogopa kuyumba kwa chama, kwani hao mabandidu(wauza unga ) , principle kubwa uwe mfadhili wa chama, na mfurukutwa wa chama basi wewe utauza unga mpaka basi!!!, na vigogo wa serikali utawapa maelekezo .sijasikia watu wa upinzani hata mmoja hasa viongozi wanapendwa na hawa watu wa madawa ya kulevya , ni kwamba matajiri wa hela chafu wanachukia chadema kuliko maelezo. na hili la CCM wasipoliangalia litawagharimu sana ukiwa mfadhili mzuri wa CCM basi karibu kila kitu unapitia kwa mwenyekiti wa mkoa unakuta mambo yako yanaenda vizuri kama tenda n.k, basi na wauza unga wanapita humo humo, na maunga yao . yaani mwenyekiti wa ccm mkoa anakauli kushinda hata mkuu wa mkoa hili nalo janga , halafu wana njaa kweli kweli kwa nini wauza unga wasione nchi yao wanaishika wao imekuwa COLOMBIA!!!!!. yaani kumbe mwalimu aliona mbali sana ,huyu mtu mmoja tu anawazungusha akili si wamtaje tu na kamtandao kake sisi tunajeshi , vita vya haya madawa tuvianzishe na tuvimalize. yaani mpaka namkumbuka mrema kwa utendaji wake , naona wangepewa siku 7 tu , na ikibidi huko hong kong wafanye mpango kuwahoji washitakiwa na waliofungwa huko watusaidie jamani hili. tukifanya uzembe halitaisha na harakati za mwakyembe hazitaonekana .
 
Kitendo cha Dk Mwakyembe kuwataja watu walio fanikisha usafirishaji wa madawa ya lkulevya ni hbari nzito inayoendelea sasa!
Kwa mara nyingine nimeshtushwa na namna tunavyowapima viognozi wetu na utendaji wao .
Kwa mtu wa aina ya Mwakyembe anajua kuwa alichofanya ni propaganda tu ya kuuza jina! Kinachoendelea nchini ....kushamiri kwa biashara hii ni matokeo ya ombwe kubwa la uognozi lilotamalaki kuanzaia utawala wa JK [NASISITIZA ....KUTAMALAKI] Tumefika hapa kutokana na kuanguka kwa tasisi zetu na ubnafsi uliopinukia ulizalishwa na uongozi lege2 !
Kama isingekuwa unafiki wa Mwakyemmbe wa kutoa taarifa nusu ya Richmond leo tusingekuwa na Ombwe hili la uongozi!
Tanzania haihitaji viongozi imara bali tasisi imara za uongozi!
Kama Rais anaorodha ya wauza unga hizi sifa tunazompa Mwakyembe kuwakamata makoplo ni zanini@
Dhambi ya unafiki aliyotenda Mwakyembe na wenzake haitamwacha
Madaw ya kulevya ni biashara haramu duniani kote lakini hushamirizaid pale penye uongozi dhaifu !
Vita yetu iwe kwenye uonozi dhaifu .Tulipo sasa tuna upungufu wa kinga haya mengine ....umaskini ,rushwa ,tamaa ,madawa ya kulevya ni magonjwa nyemelezi tu
MUNGU IBARIKI TZ ILI WATU WAONE NURU YA KUIKOMBOA NCHI HII!
 
Safi ndugu, hiyo ni critical analysis.
Watanzania ni wasahaulifu sana na haya maigizo ya CCM na serikali yake eti bado yanatupumbaza. Kwa nini Mwakyembe? Kwa nini leo wakati biashara imekuwapo toka JK anaingia Magogoni? Kwa nini kutumia media lobby badala ya taasisi husika kama Polisi, TISS na Mahakama?

Naunga mkono hoja yako kuwa tunahitaji taasisi imara za uongozi na sio kiongozi imara.....CHADEMA ticks this box nicely.
 
Well said mkuu. Nakuunga mkono 100%. Ni sawa na mgonjwa wa tyfod akawa anameza diclofenak kutulza maumivu tu, kisha gonjwa lipo palepale. CCM ndo wauzaji wakubwa wa sembe
 
wanafiki ni nyie ambao kila kukicha mmekuwa mkijaribu kupindisha ukweli juu ya harakati za mwakyembe ktk kupambana na wauza sembe.at least yeye ameonyesha njia nami namuunga mkono
 
Zanzibar wamefanya mabadiliko baraza la Mawaziri ni wakati wa Tz Bara Mh Rais tunakuomba ukifanya mabadiliko mh James Lembeli usimsahau kwenye baraza la mawaziri ikibidi awe Waziri wa uchukuzi kisha Mwakyembe awe Waziri wa mambo ya Ndani Magufuri awe waziri wa Utawala Bora hakika ndani ya mda mfupi Nidhamu na maadili yatarejea kwa kasi sana
 
Kama hukuuelwa ujumbe uliokuwemo ndani ya Richmond report pole, sisi tumesha toka huko, usiturudishe, ajenda iliyopo mezani wauza 'unga'.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom