Leo asubuhi nilikuwa nasikiliza mwendelezo wa hotuba ya dr h Mwakyembe! yes kausomea udoctor! lkn nimeshindwa kumwelewa kabisa Kasimama mbele ya vyombo vya habari kututajia walinzi! Binafsi siamini kama wale wanahatia kwani hata kama ile kazi wasinge iruhusu kupenya basi huenda maisha yao yangekuwa matatani. Nilichotegemea kutoka kwa mtu mkubwa kama waziri mwakyembe ni kutuambia baada ya kuona muvi nzima kupitia makamera hayo ya JNIA amefanya uchunguzi gani na kubaini wanaosafirisha hiyo mizigo. kwa mtu na akili zake kumvimbisha kichwa MWAKYEMBE kuwa ni Mchapa kazi ni kuwadanganya watanzania ili wamuonapo mkuu wa kaya akigawa uwaziri kumfikiria huyu mtu. Sikubali utaratibu alooutumia MWAKYEMBE kwani hakutueleza ni jinsi gani amepambana na mizizi ya tatizo na siyo ujinga wa kuwapumbaza watanzania. kumfukuza mlinzi na wauza madawa ya kulevya wapi na wapi? hao ni dagaa tu mapapa yapo yanafikiria ni jinsi gani yawatumie hao vijana kupanu miradi yao. Miradi ya wakubwa tunajua ukilima bangi unatafutwa kwa udi ila wenye vidonge vya unga hadi wakamatwe out. nilichojifunza kwa taarifa ya Dr ni kuwa kitendo cha wauza unga kukamatwa sauz Africa kimetia doa TANZANIA hivyo waziri kaona kujiosha ni kuwatimulia mbali walinzi. huenda hata hawajahojiwa ili wasimwage siri za mtandao wa unga. Inauma sana
Nianze na neno la mwisho inauma sana, jee kilichokuuma ni nini? Kwamba vidagaa wamekamatwa na mapapa bado siyo au kitu gani kunakuuma?
Mimi nilitegemea kwamba pamoja na kuanza na vidagaa hiyo ndio safari ya kuelekea kwenye bahari kuu kuwapata mapapa.
Dr. Harisson kaonyesha ujasiri wa hali ya juu na hatuna budi kumshukuru japo kwa kuanza na vidagaa. Hao vidagaa sasa ndio watatoboa siri wametokea bahari kuu ya wapi ili mapapa wakavuliwe kwa nyavu za chuma. Hii kazi ni nzito msikurupuke tu kulaumu laumu ovyo. Huyu kiongozi kajitosa uhai wake ww unasema eti vidagaa, sawa lakini hata papa huanza kma kidagaa.
Hivi ww ukiwa umesimama kwa mbali ukaona mti wa mbuyu utaanza kuona mizizi au matawi na majani yake? na kabla hujauchimba mbuyu nadhani kwanza utakata kata matawi na kisha kuanza kuung'oa mizizi.
Hata mwembe uliokatikati ya mijengo unapotaka kuukata lazima uanze na matawi ili yasije angukia nyumba na kuibomoa, kisha utaendelea na kufukua mizizi yake wakati matawi hatarishi umeyakata.
Kuanza na vidagaa ni sawa tu maana hao mapapa wakikosa vidagaa wa kuwatuma wao wenyewe hawawezi ingia mtaani watabaki na unga wao mpaka uoze.
Tena mie napenda hao vidagaa watiwe adabu mpaka washike adabu yao na iwe fundisho kwa wengine wenye mawazo km hayo.
Ngd yangu, safari yoyote huanza kwa hatua ya kwanza na kesha zinafuata nyingine hadi kufika mwisho wa safari.
Km una hisi kuna ndg yako ameguswa na mafekeo ya Dr basi katoe ushirikiano kwa Dr. ili kusaidia safari hii iendelee na sio kulaumu.
Nawasilisha