Anayejua posho na mishahara ya Wabunge atuwekee

rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
16,364
22,519
ANAYEJUA POSHO NA MISHAHARA YA WABUNGE ATUWEKEE

Kuna kipindi wabunge wakiongozwa na Tundu Lissu na Zitto Kabwe walidai rais atangaze kima cha mshahara anachopata.habari yao ilipewa uzito mkubwa mpaka pale rais alipotamka mshahara wake.Baada ya rais kutamka kiwango anachopata walitaka kujua posho anazopata pia walitaka akatwe kodi.

Lakini wakati wabunge wanadai hivyo wao wenyewe wamekuwa wagumu kutaja posho na mshahara wanaolipwa.Kuna kipindi gazeti la mwananchi liliandika juu ya kuongezwa mshahara na posho zao lakini wabunge wengi walikuja juu na kudai kitendo hicho kinawagombanisha na wananchi wao.

Sasa kwa nguvu ileile waliyotumia kutaka rais ataje mshahara wake ni vema na wao wakawa wawazi tujue ni kiasi gani cha posho na mshahara wanaopata na pia kama wanakatwa kodi inavyostahili.
 

Attachments

  • ANAYEJUA POSHO NA MISHAHARA YA WABUNGE ATUWEKEE.docx
    11.3 KB · Views: 39
Back
Top Bottom