Nsibhwene
JF-Expert Member
- Dec 8, 2016
- 293
- 217
Hivi majuzi Prof. Maghembe, Waziri wa maliasili na Utalii alitoa tamko kuhusu ukomo wa usafirishaji wa mkaa unaotokana na miti. Katazo hilo lilitaka ifikapo julai mwaka 2017 haitaruhusiwa kusafirisha mkaa kutoka wilaya moja kwenda nyingine. Julai ndio hiyo inakaribia, Je maandalizi yakoje wana jamvi, maana tusijekuona kama ni agizo ni jipya hasa litakapoanza kutekelezwa.