Nawapa trick ambayo ni ngumu zaidi ila inalipa zaidi ukifanikiwa kufuata process nzima. Itachukua muda na kama huna ujuzi wa computer itakusumbua sana ila its worth it.
VPN Services hua si za kuziamini, ni bora kua na ya kwako mwenyewe, that way unajua fika kua all traffic inapita kwako tu na si kwa mtu mwingine. Sasa kua na VPN server yako mwenyewe unafanyeje?
1. Register Amazon AWS. Hapa ukijiunga wanakupa mwaka mzima bure kabisa, alafu mwaka unaofuata unapewa 700 hours per month ambayo ni basically mwezi mzima kama unatumia micro instance.
2. Ukisharegister, umepata account, chagua region unayotaka VPN yako iwe, mfano kama unataka US, then chagua US region sehemu yoyote.
3. Tengeneza micro instance, hii hua ina 700hours free usage kila mwezi. Kumbuka una mwaka mzima wa bure kwanza.
Sasa cha muhimu, ukiwa unatengeneza instance, inatakiwa utumie image ya OpenVPN. Hii image ukiwasha instance inakua na openvpn setup moja kwa moja tayari kuweza kutumia.
4. Chukua IP address ya instance yako, weka kwenye browser yako alafu ifungue. Nenda ufanye settings
5. Weka username na password, tengeneza account mpya, unaweza kuitumia wewe, ndugu zako pia bila shida.
6. Download OpenVPN kwenye computer na simu zako zote
7. Download profile kutoka kwenye instance yako
8. Tumia VPN yako mwenyewe, full protected na bure mwaka wa kwanza mzima, mwaka wa pili unaweza jiunga upya kupata bure mwaka mwingine kama una roho ngumu kulipa au kama hauna shida unalipia kama mimi $5 kwa mwezi bei ndogo sana.