Can I interest you na bidhaa kutoka Zola kwa kushirikiana na Solar sister?
Kwa ulivyotaja kuhusu TV nafikiri itakufaa package ya dlight X2000.
Katika package hii utapata TV, redio ndogo, tochi ndogo yenye uwezo wa kumulika umbali wa viwanja vitano vya mpira, utapata taa za muundo wa bulb nne, utapata na taa moja ya muundo wa tube light.
Taa hazivunjiki.
Unaweza kukadiria mwanga unaoutaka.
Unapata na warranty kwa hii bidhaa utakayonunua.
Unapata panel na contorl box ya kuwasha na kuzima mtambo mzima.
Taa zake zina waya ambao una sehemu za kuweza kuunga taa zingine. Namaanisha kwamba, taa itatakiwa kuchomekwa kwenye control box, lakini ikatokea unataka kuongeza taa badala ya kuchomeka kwenye control box unaweza kuchomeka katika sehemu maalumu ya taa nyingine.
Isipokua hii taa uliyochomeka katika taa nyingine itakua controlled na hii taa kuu ambayo imechomekwa kwenye control box.
Sijajua eneo ulilopo ila kama utakua eneo zuri unaweza kulipia kidogo kidogo.