Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 21,441
- 38,124
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, limemtia mbaroni mtu mmoja anayetuhumiwa kuhusika na tukio la ugaidi jijini Kampala, Uganda, ambapo watu takribani 73 waliuawa baada ya ukumbi waliokuwa wakiutumia kutazama mechi ya fainali ya kombe la dunia kwa njia ya runinga kulipuliwa kwa mabomu, mapema Julai, mwaka huu.
Mtuhumiwa ambaye anadaiwa kuwa ni raia wa Somalia, alikamatwa juzi eneo la Sombetini jijini hapa.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kushukiwa na raia mwema ambaye alifikisha taarifa kituo cha polisi na baadaye polisi kufanikisha kumtia mbaroni baada ya kufanya operesheni ya kumnasa.
Kwa mujibu wa habari za kipolisi ambazo Nipashe ilizipata jana zilisema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa Septemba 11 eneo la Sombetini ambako alikuwa ameweka makazi ya muda .
Taarifa hizo zilidai kuwa baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo ambaye alitambuliwa kwa jina la Abudaumaki Majidi alichukuliwa chini ya ulinzi wa polisi na kufikishwa hadi makao makuu ya polisi mkoani hapa.
Timu ya wapelelezi ya jeshi la polisi mkoani hapa, ilimfanyia mahojiano ya saa 24 lakini awali hawakuweza kupata ushirikiano kutoka kwake.
Hata hivyo, timu hiyo ya upelelezi ilibaini kuwa mtuhumiwa huyo anashirikiana na kikundi cha Al-Shabab ambacho kinausika na matendo mengi ya kigaidi nchini Somalia na kwingineko.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Basilio Matei, alithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kwamba alisafirishwa jana kwenda Dar es Salaam.
"Ni kweli tumemkamata ila kesi yake itakuwa makao makuu ya Jeshi la Polisi Dar es Salaam, tumemsafirisha chini ya ulinzi wa jeshi la polisi lakini ngoja nikwambie lakini bado hatujapata ushahidi kamili wa kujitosheleza ndio sababu tukaamua kumpeleka makao makuu ya Jeshi la Polisi Dar es Salaam kwa mahojiano zaidi," alisema Kamanda Matei.
CHANZO: NIPASHE
Wakuu niliwahi kutoa angalizo kuhusu hili dubwana EAC na free movement nikaseama hali ya amani Tanzania itakuwa mbaya iwapo tutaruhusu free movement bila kuzingatia suala la ulinzi na usalama.Kenya ina mpaka mkubwa na nchi ya Somalia ambayo silaha zinauzwa kama pipi wasomali wanaweza kuleta balaa zao hapa Tanzania tusipokuwa makini.