Ngoja tuheshimiane mjini,watu walikua na mapesa ya dhambi wakawa na dharau wanaweza kuwasha gari wanalandalanda mjini kutafuta wanawake na hawajali ni mke wa mtu wala nini wanabeba tu kwa kiburi cha pesa,wapo watu wa namna hiyo mijini,hii hua ina maanisha siyo pesa za jasho wakazionea uchungu,wamezipata kiujanja ujanja ndo mana hazina maana kwao.wamebeba sana wake za watu na kuwaonea wasiyo na fedha kwa kuwapa manyanyaso kede kede.najua wakibanwa na pesa zao zikaminywa ni kweli kutakua na hali ngumu kiuchumi huku chini pia,ila kwa dhambi zao acha waminywe ili tuheshimiane mjini.kwa vile sina uwezo tu wa kukutana na Rais uso kwa uso,ningempa mkono wa hongera kwa kazi nzuri ya kiutume.ngoja tutoke Misri twende Kaanani.SHIKAMOO MAGUFURI