Anayedaiwa Kuingiza Sh. Milioni 7 kwa Dakika Kizimbani

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,266
33,039

Mtuhumiwa Mohamed Yusuph Ally anayedaiwa kuingiza milioni 7 kwa dakika akipelekwa rumande.

MFANYABIASHARA anayedaiwa kukwepa kodi na kuingiza shilingi milioni 7 kwa dakika amesomewa mashitaka 199 leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar kisha kupelekwa rumande.

Watuhumiwa hao wakipelekwa rumande.

Mtuhumiwa huyo aitwaye Mohamed Yusuf Ally alisomewa mashitaka hayo likiwemo la kugushi na kuwasilisha taarifa za uongo kwa kamishna wa TRA akidaiwa fedha zaidi ya shilingi bilioni 15 za Kitanzania.

Watuhumiwa wakitolewa eneo la mahakama.

Mtuhumiwa huyo akiwa na wenzake watatu hawakutakiwa kujibu chochote kwa sababu kesi hiyo ni ya uhujumu uchumi.

Hakimu aliyekuwa akisikiliza shauri hilo, Huruma Shaidi aliiahirisha na akasema itatajwa tena Julai 25 mwaka huu

Habari na picha: Denis Mtima

CHEKI VIDEO HAPA

chanzo.Anayedaiwa Kuingiza Sh. Milioni 7 kwa Dakika Kizimbani
 
Attachments

  • Anayedaiwa Kuingiza Sh. Milioni 7 kwa Dakika Kizimbani.jpg
    Anayedaiwa Kuingiza Sh. Milioni 7 kwa Dakika Kizimbani.jpg
    201.1 KB · Views: 98
  • Watuhumiwa hao wakipelekwa rumande.jpg
    Watuhumiwa hao wakipelekwa rumande.jpg
    45 KB · Views: 98
  • Watuhumiwa wakitolewa eneo la mahakama..jpg
    Watuhumiwa wakitolewa eneo la mahakama..jpg
    51.6 KB · Views: 92
Ngoja tuheshimiane mjini,watu walikua na mapesa ya dhambi wakawa na dharau wanaweza kuwasha gari wanalandalanda mjini kutafuta wanawake na hawajali ni mke wa mtu wala nini wanabeba tu kwa kiburi cha pesa,wapo watu wa namna hiyo mijini,hii hua ina maanisha siyo pesa za jasho wakazionea uchungu,wamezipata kiujanja ujanja ndo mana hazina maana kwao.wamebeba sana wake za watu na kuwaonea wasiyo na fedha kwa kuwapa manyanyaso kede kede.najua wakibanwa na pesa zao zikaminywa ni kweli kutakua na hali ngumu kiuchumi huku chini pia,ila kwa dhambi zao acha waminywe ili tuheshimiane mjini.kwa vile sina uwezo tu wa kukutana na Rais uso kwa uso,ningempa mkono wa hongera kwa kazi nzuri ya kiutume.ngoja tutoke Misri twende Kaanani.SHIKAMOO MAGUFURI
 
Du bongo bwana,watu wanaujanja ujanja sana,ila awamu hii wataisoma namba kwa Mhesh JPM
As long as rushwa itaendelea kuwepo nchini, watu wa namna hii watapata tu, kwa kile kinachoitwa ushaidi hautoshelezi .
 
Ngoja tuheshimiane mjini,watu walikua na mapesa ya dhambi wakawa na dharau wanaweza kuwasha gari wanalandalanda mjini kutafuta wanawake na hawajali ni mke wa mtu wala nini wanabeba tu kwa kiburi cha pesa,wapo watu wa namna hiyo mijini,hii hua ina maanisha siyo pesa za jasho wakazionea uchungu,wamezipata kiujanja ujanja ndo mana hazina maana kwao.wamebeba sana wake za watu na kuwaonea wasiyo na fedha kwa kuwapa manyanyaso kede kede.najua wakibanwa na pesa zao zikaminywa ni kweli kutakua na hali ngumu kiuchumi huku chini pia,ila kwa dhambi zao acha waminywe ili tuheshimiane mjini.kwa vile sina uwezo tu wa kukutana na Rais uso kwa uso,ningempa mkono wa hongera kwa kazi nzuri ya kiutume.ngoja tutoke Misri twende Kaanani.SHIKAMOO MAGUFURI
Wenye pesa ni wenye pesa tu. Hawa matajiri wakubwa pesa zao hazipo hapa, zipo panama.

Sukari imeshinda, ataweza mengine.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom