Anayedai kutibu kama Babu azuiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anayedai kutibu kama Babu azuiwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by engmtolera, Mar 21, 2011.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  KUTOKANA na kujitokeza kwa mtu mwingine wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro anayetoa dawa ya kutibu magonjwa sugu kama alivyo Mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwaisapile 'Babu', mtu huyo amesitishwa na Ofisa Mtendaji wa Kata kuendelea na huduma hiyo.

  Akizungumza na gazeti hili kwa simu, kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Hilali James (28), alisema endapo Serikali itashikilia msimamo wake wa kuendelea kuisitisha huduma yake, tayari ameoteshwa ndoto kuwa atatokea mtu mwingine ambaye ataendelea kuitoa huduma hiyo.

  James alisema huduma hiyo alikuwa akiitoa katika Kijiji cha Mbomani Chini Kata ya Tarakea wilayani Rombo, ambapo masharti yake ni mtu kutakiwa kunywa vikombe viwili kwa wakati mmoja na hairuhusiwi kurudia.

  Mbali na kunywa, alisema alioteshwa ndoto kuwa atapokea Sh 500, ambazo kati ya hizo, Sh 200 ni kwa ajili ya matumizi yake ya kuwalipa wafanyakazi, na Sh 300 za kuwasaidia yatima na watu wasiojiweza.

  Akizungumzia magonjwa yanayotibiwa na dawa yake, alidai inatibu shinikizo la damu, kisukari pumu, saratani, figo, Ukimwi na magonjwa ya tumbo.

  Alidai tayari watu wapatao 100 wamekwisha inywa dawa hiyo na kupata uponyaji.

  Kijana huyo mwenye mke na watoto wanne, alibainisha kuwa awali alikuwa fundi wa baiskeli, na kwamba chanzo cha kuanza kutoa dawa hiyo ni kutokana na kuoteshwa ndoto na Yesu Kristo usiku na mchana.

  Alisema mti aliooteshwa kuutumia hadi sasa hajaufahamu jina lake, na kuwa ulikuja katika ndoto na hajawahi kuuona tangu kuzaliwa kwake.

  Alisema yeye kuibuka baada ya Mchungaji Mwaisapile si tatizo kwa sababu, kila jambo lina wakati wake, hivyo wakati huu ni wake.

  Juhudi za kumpata Ofisa Mtendaji aliyesitisha utoaji wa huduma hizo hazikuzaa matunda, kwani simu yake ya mkononi ilikuwa haipatikana.
  HABARI LEO
   
 2. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Nyie simnaamini aliyooteshwa mchungaji? basi na huyo mfateni. na kwa wale mnaomsingizia Yesu kuwa ni mungu jueni kuwa Mchungaji alitokewa na Yesu tu, lakini huyo dogo katokewa na Yesu pamoja na mama yake, halafu dogo hajafanya ubishi kama alivofanya babu.

  Subirini tu mbona mwakahuu tutasikia mengi na hatima ya hayo mtakimbiana wenyewe mnaoamini nguvu za giza.
   
Loading...