Kamera ya Globu ya Jamii imemnasa mdau huyu akikimbilia Kivuko cha MV. Magogoni (hakipo pichani) kilipokuwa kinaanza kuondoka kuelekea Kigamboni.Pamoja na kuwepo kwa tangazo kubwa kabisa la Tahadhari la kutokimbilia Kivuko pale pembeni,lakini mdau huyu aliendelea na mbio zake mpaka kwenye kivuko.