anatamani afanye maamuzi magumu

Eversmilin Gal

JF-Expert Member
Feb 5, 2012
778
269
jamani nimepokea simu ya rafiki yangu akaniambia anatamani afanye maamuzi magumu lakini yuko kwenye dilemma anataka aachane na mume wake dilema iko kwenye mwanaye bado hajaweza kujitegemea anajisahau anajiko**lea mara nyingine anajin**e hajaweza kuongea vizuri huyo rafiki yangu ambaye tupe jina la Q ni binti mdogo tu miaka 25 ameolewa na an amtoto mmoja amebahatika kusoma mpaka form six na badaye akasoma certificate IFM ya insurance bada ya kumaliza hiyo cert hakuweza kuendelea tena na masomo wala hakufanya kazi akawa mama wa nyumbani huku mumewe akimuanbia atamtafutia kaz na atamuendeleza mume wake ni marketin manager ofisi moja hapa mjini hatakiQ afanye kazi anataka awe mama wanyumbani kiukweli ukimuangalia q amebadilika hana confidence ni miaka minne yupo tu ka mama wa nyumbani hata ndugu zake anashindwa kuwaface hana rafiki zaid ya mimi anajifungia ndani hatoki wala hatembelei mtu ameniomba ushauri amechoka kua golkipa anataka ondoke na mimi nkaona niwashikirishe maGreat thinker nilisahau kusoma kote kasomeshwa na mama na mume w ake hamheshimu mama yake hata kidogo please naombeni msaidie kama unaona ni hadithi usichangie
 
kwani akiamua kujiendeleza shule je?
kumshauri amuache mume now ana mtoto mdogo na hajawahi jitegemea
ni ngumu sana...

ushauri avumilie hukuanajiendeleza shule
na akitaka kumuacha mume ahakikishe amepata kazi kwanza

mpe pole
 
Yeye huyo rafiki yako ndiye chanzo cha tatizo. Kwanza alitakiwa akae na mume wake wapange future zao mfano waamue kama ni shule kwanza zaidi au kazi kwanza. Kama angemkatalia sema kazi anaweza kutafuta watu wakawashauri. Kosa jingine ni la yeye kumtegemea mume amtafutie kazi, kwani yeye hajui kusoma magazeti? Atafute kazi kivyake vyake,
 
mume wake ndo alitaka amzalishe fasta na alimuahidi pindi atapojifungua ataendelea lakini badaye alibadilika mpaka mtoto wake afikishe miaka mitatu
 
kwani akiamua kujiendeleza shule je?
kumshauri amuache mume now ana mtoto mdogo na hajawahi jitegemea
ni ngumu sana...

ushauri avumilie hukuanajiendeleza shule
na akitaka kumuacha mume ahakikishe amepata kazi kwanza

mpe pole

Nitahahakisha amepata pole yako The boss kweli anatia huruma hata kujiendeleza huko cdhani kama mume wake atamruhusu kwani mpaka leo hii hajaply chuo chochote ndo maana anasema afanye maamuzi magumu ya kuondoka
 
jamani nimepokea simu ya rafiki yangu akaniambia anatamani afanye maamuzi magumu lakini yuko kwenye dilemma anataka aachane na mume wake dilema iko kwenye mwanaye bado hajaweza kujitegemea anajisahau anajiko**lea mara nyingine anajin**e hajaweza kuongea vizuri huyo rafiki yangu ambaye tupe jina la Q ni binti mdogo tu miaka 25 ameolewa na an amtoto mmoja amebahatika kusoma mpaka form six na badaye akasoma certificate IFM ya insurance bada ya kumaliza hiyo cert hakuweza kuendelea tena na masomo wala hakufanya kazi akawa mama wa nyumbani huku mumewe akimuanbia atamtafutia kaz na atamuendeleza mume wake ni marketin manager ofisi moja hapa mjini hatakiQ afanye kazi anataka awe mama wanyumbani kiukweli ukimuangalia q amebadilika hana confidence ni miaka minne yupo tu ka mama wa nyumbani hata ndugu zake anashindwa kuwaface hana rafiki zaid ya mimi anajifungia ndani hatoki wala hatembelei mtu ameniomba ushauri amechoka kua golkipa anataka ondoke na mimi nkaona niwashikirishe maGreat thinker nilisahau kusoma kote kasomeshwa na mama na mume w ake hamheshimu mama yake hata kidogo please naombeni msaidie kama unaona ni hadithi usichangie

Amtumie mwanawe kama silaha ya mazungumzo na mumewe ili amkidhie haja yake. Hata hivyo Waswahili husema kumi nenda uje si sawa na moja iliyo kibindoni. Kazi tunafanya ili tupate maisha mazuri na iwapo anatimiziwa kila kitu na mumewe ni muadilifu anataka nini tena? Ana uhakika gani na huko nje anakoona kuwa kuzuri, anaweza akakosa mwana na maji ya moto. Wanawake wengi waliowekwa nnyumbani kindowa wanadanganyika na mashamsham ya wenzao bila kujuwa kuwa wanalazimika kufanya hivyo ili kuungaunga maisha.
Suwala la kupata marafiki si muhimu, iwapo atamfanya mumewe rafiki na kumpenda. Panapo mapenzi ya kweli kunaweza kukaleta tija baadae mumewe akafunguka na tabia hiyo anayoiona inamkondesha.
 
Nitahahakisha amepata pole yako The boss kweli anatia huruma hata kujiendeleza huko cdhani kama mume wake atamruhusu kwani mpaka leo hii hajaply chuo chochote ndo maana anasema afanye maamuzi magumu ya kuondoka

ataondoka kwenda wapi?
huko kuna uhakika wa maisha na mtoto?
 
Dah... Haya maisha ni ya kukaa na kumtegemea mwanaume kweli jamani? Maisha ya sasa ni kusaidiana.. Na asikwambie mtu kazi inaleta heshima ndani ya nyumba.. Aaache kujibweteka atafute kazi huyo rafiki yako.. Na kuhusu kumuacha mumewe asithubutu kabisaa.. Aongee nae tuu kwa heshima na ustaarabu wataelewana... Leo hii akimuacha mumewe kesho huyo mumewe atakuja JF kutafuta mke mwingine.. Hasara kwa nani?
 
mume wake ndo alitaka amzalishe fasta na alimuahidi pindi atapojifungua ataendelea lakini badaye alibadilika mpaka mtoto wake afikishe miaka mitatu

Kwa kuzingatia hapo kwa red, mi nashauri awe na subira hadi mtoto afikishe huo umri. Then, aongee na mumewe kuhusu kama shule au kazi. Kama mume hataki afanyekazi ya ofisini basi amuwezeshe awe mjasiriamali. Ila chonde chonde, mshauri aendelee kuvumilia tu kwa sasa.
I can understand kwanini unamuona amebadilika hivyo, ni wanawake wachache sana wenye elimu zao wanakubali kuwa mama wa nyumbani hata kama unamtimizia kila kitu.
 
Loh. Jamaa ni mtu wa mfumo dume! Na pia sioni kabisa kuwa anamjali
mwenzi wake. Nilitarajia kuwa angepashwa kumsikiliza kuwa nae anataka nini katika maisha yake.

Command ya nini kuwa mpaka mtoto afikishe miaka mitatu?. Mtoto ni wa kwao wote wangeweza
kujadiliana kwa pamoja wafanyaje kuhakikisha kuwa mtoto anapata huduma ili mkewe nae ajiendeleze
au atafute kazi kwani kufanya hivyo ni kwa faida ya familia. On my views jamaa ashauriwe, sioni kuwa afanyavyo ni sawa. Itasaidia kuepusha hizo hisia za mke za kutaka kuondoka. Mazingira yoyote yanayojitikeza katika familia wote mume na mke wanapaswa kuuvaa uhusika.
 
mume wake ndo alitaka amzalishe fasta na alimuahidi pindi atapojifungua ataendelea lakini badaye alibadilika mpaka mtoto wake afikishe miaka mitatu
Asiachane naye. Yeye atumie network yake kutafuta kazi, then aanze kufanya kazi, suala la kazi ni maisha yao
 
ataondoka kwenda wapi?
huko kuna uhakika wa maisha na mtoto?

The Boss
Are you really implying there can never be life without her husband au Mtoto bila baba hawezekani??........:frown:!!!!!!

Eversmillin gal

The way I see it sooner or later itabidi afanye tu maamuzi magumu apende asipende maana from the sounds of it she extremely unhappy if not depressed!. Ila mamii in this life, wanaume sio wa kuendekezwa ( in my chagga accent)kapisaaa. "Ohh sitaki mke wangu afanye kazi", "Baby kwanini usikae tu nyumbani na mtoto mpaka kakue", ohh blah blah blah.............~urgh. Mwambie achakarike na kutafuta hiyo kazi if that's what she wants,au kama ni shule akajiunge aje home na slip ya fees na sio kung'ang'ana seating doing nothing awaiting unfulfiled promises za 5 years ago!
 
Kuna mahali nilimsoma @ gfsonwin akisema miaka saba ya kwanza ya ndoa huwa ni migumu sana.
Mhusika katika hii mada bila shaka ndo ndoa yao iko katika awamu hii ngumu.
Mwambieni a take heart,for she is not alone,na kiukweli mama yake mzazi anatakiwa ampe binti yake moyo sio na yeye kukoleza moto eti mkwe anamdharau.
 
Dah... Haya maisha ni ya kukaa na kumtegemea mwanaume kweli jamani? Maisha ya sasa ni kusaidiana.. Na asikwambie mtu kazi inaleta heshima ndani ya nyumba.. Aaache kujibweteka atafute kazi huyo rafiki yako.. Na kuhusu kumuacha mumewe asithubutu kabisaa.. Aongee nae tuu kwa heshima na ustaarabu wataelewana... Leo hii akimuacha mumewe kesho huyo mumewe atakuja JF kutafuta mke mwingine.. Hasara kwa nani?

Mtoto kashafikisha miaka mitatu na anapelekwa day care anarudi kila siku jion saa 12 anabaki amelala tu ndani can u imagine
 
Loh. Jamaa ni mtu wa mfumo dume! Na pia sioni kabisa kuwa anamjali
mwenzi wake. Nilitarajia kuwa angepashwa kumsikiliza kuwa nae anataka nini katika maisha yake.

Command ya nini kuwa mpaka mtoto afikishe miaka mitatu?. Mtoto ni wa kwao wote wangeweza
kujadiliana kwa pamoja wafanyaje kuhakikisha kuwa mtoto anapata huduma ili mkewe nae ajiendeleze
au atafute kazi kwani kufanya hivyo ni kwa faida ya familia. On my views jamaa ashauriwe, sioni kuwa afanyavyo ni sawa. Itasaidia kuepusha hizo hisia za mke za kutaka kuondoka. Mazingira yoyote yanayojitikeza katika familia wote mume na mke wanapaswa kuuvaa uhusika.

Kwa ninavyomjua huyo mwanaume ni dikteta wa maamuzi wala hashauriki
 
Mwambie akae na mumewe aongee nae kuwa amechoka kukaa nyumbani na kuwa golikipa.

Kama hatashindwa kumsikiliza, afanye maamuzi magumu hakuna njia nyingine.
 
naamin hii ni ndoa iliyofuata tarartbu zote za kidini au kiserikali,binafsi sishauri ktk kuvunja ndoa kwa kosa lolote hili(nina sababu)..halafu mambo yanazungumzika,love has never failed any one..........haijarishi amejarbu mara ngap,still i can see a very good future na hii ndoa yes afanye uamuz na uamuz mgum ni kulinda ndoa.all the best!!!!!!
 
Huyu dada ana kihoro na kiroho papo hapo, yaani kuwa mama wa nyumbani ndio ivunje ndoa?

Kwanza mume kafanya kosa gani la kustahili ndoa kuvunjwa?????

Sasa kama yeye mwenyewe hajiamini, mumewe atamwamini vipi hadi amsomeshe???

Huyu binti anaonekana kuku wa kizungu angekuwa wa kienyeji elimu ya form six ni kubwa mno kufanya 'tukio' la kujiingizia kipato si lazima kuajiriwa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom