Umeshasema ana miaka 18 na kamaliza secondary huyo hana udogo labda kama ulikuwa unamtaka na jamaa kakunyang'anya tonge mdomoni.
Suz mbona hujasema mapema wazalishaji tumejaa tele humu lol!... aje azae na mie natafuta mtoto!!!
Habar zenyu wanathnker ninaomba mnisaidie jaman ninarafik yangu wa karbu anaumri 30 na anauwezo na kila ki2 na ananisaidia katka biashara zangu. Mara ya mwisho baada ya kuona hana jins akaniambia anataka kuzaa na msichana ilimrad awe na mtoto wakat anaendelea kutafuta mke taratibu. Na mm kwakuona umri wake kwel umekwenda nikamkubalia wazo hilo. Sasa tatzo linakuja amejenga mazoea na msichana mdogo (ambaye ni rafiki wa mdogo wangu wa kike pia) 18 ambae amemaliza form 4 hv juz na ameniambia anataka kuzaa nae. Mimi huyo msichana ananiheshimu kama kaka yake baada ya jamaa kujakuniambia anataka kumzalisha yule msichana hatuelewan kabisa baada ya mimi kumpinga kias kwamba kampiga marufuku yule msichana kuja home. Alafu pia kamkataza kuongea na mdogo wangu je wanathnker nifanyeje nimuokoe huyu mdogo wangu?
Miaka kumi na nae wa karne hii ni mtoto?labda vile hajamaliza kusoma.....anafanya nini kwa sasa?? isije kuwa hajafanya vizuri form four,amekata tamaa,na huyu mwanaume ana take advantage anataka kumuharibia? mwambie asikubali kuwa mashine ya kuzalisha watoto na mwanaume asiyempenda.......!!!!
mshauri huyo msichana asubiri kidogo ila uamuzi wa mwisho utabaki kuwa wake na si wa kwako.....!!!
Vyombo vya dola hawatafanya lolote binti ana zaidi ya 18 na huyu jamaa anataka mtoto kwahiyo hamna uwezekano wa yeye kutowajibika kwa mama/mtoto hayo ya ndoa ni mengine....toa taarifa kuhusu fataki huyo kwa vyombo vya dola na mashirika ya kutetea haki za watoto
amelaniwa huyooooo!!!
kama kakosa kabisa mwambie aje azae na mie natafuta mtoto!!! kuliko amuharibie mwanafunzi maisha yake alafu badae atafute mke wa kuoa je hiyo ni akili au matope?????
We nawe! Ulitakiwa kumshauri aoe tu na awajibike kwa familia yake. 30 years inamtosha kabisa kuchukua majukumu ya kifamilia. Siamini kama kuna mwanamke anayependa kuzalishwa tu alafu baba asichukua jukumu lake.
Kama upo sirias, toa taarifa kuhusu fataki huyo kwa vyombo vya dola na mashirika ya kutetea haki za watoto
Hapo kwenye red " anataka kumfanya binti wa watu kiwanda cha kuzalisha mtoto kwanini hajasema anataka binti wa kuoa na kuzaa nae mtoto" au huyo binti amemwambia anataka kuzaa hataki kuolewa
Hiyo naipinga kabisa sawa binti 18, lakini huyo kaka sio kama anampenda yeye anataka mtoto tu , then atafute mke wa kuoa. Atamharibia future huyo binti na kumwacha na maumivu. Si atafute mke fasta kama ana kiu ya mtoto. Dadake akifanyiwa hvyo atajisikiaje? Kwan binti hana mpango wa kujiendeleza??Hata kama hana sio kumfyatulia mtu mtoto tu kwa sababu huyo kaka anataka mtoto.
Kwanza wewe alipokuomba ushauri wa kutaka kuzaa, wewe ulifikiri atazaa na nani? Na kwanini liwe tatizo kwa kuwa uanataka azae na rafiki wa dada yako? Kwahiyo unataka kusema kuwa kama angetaka kuzaa na mdogo wa mathalani (Pretty) ingekuwa pouwa tu? Kama ningepata contacts za huyo jamaa ningemwambie amzalishe dada yako kwa kuwa wewe huna huruma na dada za wenzio ila uchungu wa kunyang'anywa tonge. period